The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 3,612
- 9,269
Mahuburi ya Askofu Josephat Gwajima Jana katika mkesha wa mwaka mpya kanisa GCTC - UFUFUO NA UZIMA yalikuwa too philosophical, indirectly yakiwalenga watesi wake - CCM, Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake...
Soma pia PreGE2025 - Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!
Ni wenye bahati ya hekima wachache wanaweza kuelewa maana yake...
Kwa wasio elewa, naomba niwarejeshe kidogo ktk hotuba zake kadhaa alizofanya huko nyuma wakati kanisa lake liko kwenye tishio la kufutiwa usajili...
Aliwahi kusema na kuwaambia na kuwashauri wenzake ndani ya CCM na serikali. Msingi wa ushauri wake ulijengwa ktk Neno la Mungu lisemalo;
Mithali 29:1-2 SUV
"....Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua..."
"....Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua..."
Kwa kutumia neno hili la Biblia akawashauri hivi wenzake kwa mdomo wake;
"...Naishauri serikali yangu chini ya Mh. Samia Suluhu Hassan na chama changu - CCM kuwa naiona hatari mbele iwapo tutaendelea na uchaguzi huu tukiwa ktk mgawanyiko huu bila kuweka mambo fulani sawa. Si vyema kuingia kwenye uchaguzi wakati CHADEMA wenzetu wakiwa nje. Kwani CCM inaogopa nini iwapo tuna wanachama 13,000,000 nchi nzima? Mbona Kikwete na Magufuli walifanya uchaguzi na CHADEMA na CCM kushinda? Tuwape CHADEMA minimal reforms Kisha tuingie nao kwenye uchaguzi na CCM itashinda. Mtoeni Tundu Lissu gerezani na tatizo la utekaji likomeshwe. Kama tutaendelea hivi, CCM italia kilio ambacho hakuna wa kukipoza na mpaka mtanitafuta tena ili niseme neno jingine..."
Achilia mbali kumwelewa, hata kusikilizwa hakusikilizwa...!
Na Jana ktk mkesha wa mwaka mpya anarejelea ushauri wake ktk namna ya hekima ya kimbingu akitumia scenario ya mtume Paulo ktk Biblia (Matendo ya Mitume sura ya 27) dhidi ya nahodha na viongozi wengine wa Meli waliokuwa wagumu kusikiliza ushauri na mwisho meli yao kuvunjwa vunjwa na tufani na kupoteza mali yote waliyokuwa wamebeba ndani ya mali...
Hata hivyo, pamoja janga hili mtume Paulo anawaambia wote waliokuwa ndani ya meli maneno haya;
Matendo ya Mitume 27:25 SUV
".....Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa..."
".....Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa..."
Askofu Josephat Gwajima baada ya kama miezi sita kuionya serikali, CCM na Rais Samia, amerudi tena leo na kurejelea maneno yake na kusisitiza kwa Neno la Mungu anatuambia hivi;
"...Basi, wanaume wa Tanganyika na Zanzibar, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu ya kwamba yatakuwa vilevile kama nilivyoambiwa..."
Maana yake hii ni kuwa, Itakuwa vile vile kama alivyowaambiwa, kwamba ni lazima yawapate CCM, Samia na Serikali yake kama Mungu alivyomwambia. Na sasa Tanzania mpya imekuja..
♦Tazama na sikiliza YouTube video clip hiyo mpaka mwisho♦