Askofu Josephat Gwajima akamatwa Uwanja wa Ndege wa Dar


barafu

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Messages
6,280
Likes
25,798
Points
280
barafu

barafu

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2013
6,280 25,798 280
Leo mchana askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima amekamatwa Airport wakati akitua toka Nje ya nchi alikoenda kwa matibabu.

Duru za habari zinanyetisha kuwa Askofu Gwajima alishuka na ndege ya Kenya Airways iliyokuwa inatoka Nairobi kuja Dar ambapo baada ya kushuka alitaka kuunganisha na chopa yake kuingia mjini kupitia Sea Cliff.

Mpaka sasa Askofu yupo chini ya ulinzi na wafuasi wake na wasaidizi wake wamethibitisha kuwa walikuwa na taarifa za kuja kwa Askofu wao leo na ndege ya Kenya Airways lakini hawajamuona,na habari walizozipata ni kuwa mara baada ya kushuka vyomba vya Usalama vilimkamata sbb walikuwa wakimtafuta kwa muda mrefu.

Waumini wake na wasaidizi wake wanaendelea kufuatilia kujuwa kiongozi wao anashikiliwa katika kituo kipi cha polisi.Hizi habari zimezua "taharuki" hapa Ubungo kanisani kwake na waumini wapo katika makundimakundi kujadili hatima ya Askofu wao
==========

Habari zaidi...


MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka na kutiwa mbaroni na jeshi la polisi.

Mchungaji Gwajima alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu), majira ya saa moja asubuhi. Alikuwa akirejea nchini kutokea matibabu nje ya nchi.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema, Mchungaji Gwajima alikamatwa wakati akijiandaa kuondoka uwanjani hapo. Alipelekwa kwenye kituo kikuu cha polisi cha Kati.

Wakili wa Gwajima, Peter Kibatala amethibitishia mwandishi wa habari hizi kukamatwa na kuhojiwa kwa mchungaji huyo machachari nchini.

Hata hivyo, Kibatala hakusema, sababu zilizosababisha Mchungaji Gwajima kukamatwa na kuhojiwa.

“…ni kweli Gwajima alikamatwa na polisi akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Baada ya kukamatwa alifikishwa kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya mahojiano ameeleza Kibatala.

Anasema, “baada ya kuhojiwa kwa muda mfupi, jeshi la polisi liliamua kumuchia Mchungaji Gwajima, hadi hapo litakapomhitaji.”

Wakati Kibatala akigoma kueleza kilichosababisha jeshi la polisi kumkamata na baadaye kumhoji Mchungaji Gwajima, taarifa za ndani ya jeshi hilo zinasema, kiongozi huyo wa kiroho amekamatwa kutokana na tuhuma za uchochozi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mchungaji Gwajima anatuhumiwa kutoa kali za uchochezi akiwa kanisani kwake, pale alipodai kuwa Rais John Magufuli, anahujumiwa na baadhi ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waumini wa kanisa lake mwezi uliyopita, Mchungaji Gwajima alimtuhumu rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, kugoma kumuachia uenyekiti wa chama Magufuli.

Akadai kuwa kitendo hicho kinadhoofisha utendaji kazi wa kiongozi huyo mkuu wa serikali na kinasababisha CCM kusheheni mapepo.

Tangu kutoa kauli hiyo, viongozi wajuu wa jeshi la polisi, wamekuwa wakidai kuwa wanamtafuta mchungaji huyo, ingawa baadhi ya watu wanasema, “alichokifanya Gwajima kina mkono wa Ikulu.
 
mpenda pombe

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
1,260
Likes
441
Points
180
mpenda pombe

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
1,260 441 180
Source?
 
Ta Kamugisha

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Messages
3,241
Likes
1,296
Points
280
Ta Kamugisha

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
Joined May 17, 2011
3,241 1,296 280
Mbona wengine wanakamatwa? Hacha akamatwe, kwani yeye ni nani asikamatwe
 
1

1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
5,339
Likes
2,975
Points
280
1

1954

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
5,339 2,975 280
Wanaacha kutafuta majambazi yanayoua watu wanahangaika na viongozi wa dini
Hivi majambazi yakoje na ambayo hayakamatwi, yamefananaje ili tuwe tunajihami mapema....nauliza tu jamani...
 
NullPointer

NullPointer

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Messages
3,480
Likes
719
Points
280
NullPointer

NullPointer

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2011
3,480 719 280
Huyu jamaa waumini wake utasema extremes wa isis, sipendi sana watu wanao~take advantage ya imani ya watu kufanya mambo yao binafsi, huyu jamaa kanisani kwake ndo sehemu ya kufanyia siasa, very stupid, japo anapiga sana hela za wajinga.
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,181
Likes
9,922
Points
280
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,181 9,922 280
Mbona wengine wanakamatwa? Hacha akamatwe, kwani yeye ni nani asikamatwe
Kuna mtu kasema asikamatwe? Povu jiiiingi kama Family Detergent ya Mama Chiku! Hebu soma signature yako:" WEAK PEOPLE REVENGE, STRONG PEOPLE FORGIVE AND INTELLIGENT PEOPLE IGNORE"
 
Polisi jamii

Polisi jamii

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Messages
2,527
Likes
1,106
Points
280
Polisi jamii

Polisi jamii

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2013
2,527 1,106 280
Vibaka wanatutesa mtaani na hawadakwi wala nini ila mtu asiyetishia amani anakamatwa faster
 
Rich Pol

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Messages
7,777
Likes
3,592
Points
280
Rich Pol

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2013
7,777 3,592 280
Wanaacha kutafuta majambazi yanayoua watu wanahangaika na viongozi wa dini
Kiongozi wa dini ndiyo ahubiri siasa kanisani?? Asajiri kanisa liwe chama halali cha siasa aone kama atafuatwa fuatwa tena
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,181
Likes
9,922
Points
280
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,181 9,922 280
Hivi majambazi yakoje na ambayo hayakamatwi, yamefananaje ili tuwe tunajihami mapema....nauliza tu jamani...
Swali la kijinga kabisa. Sikiliza vyombo vya habari utapata majibu
 

Forum statistics

Threads 1,237,681
Members 475,675
Posts 29,297,247