Askofu Josephat Gwajima akamatwa Uwanja wa Ndege wa Dar

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,816
Leo mchana askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima amekamatwa Airport wakati akitua toka Nje ya nchi alikoenda kwa matibabu.

Duru za habari zinanyetisha kuwa Askofu Gwajima alishuka na ndege ya Kenya Airways iliyokuwa inatoka Nairobi kuja Dar ambapo baada ya kushuka alitaka kuunganisha na chopa yake kuingia mjini kupitia Sea Cliff.

Mpaka sasa Askofu yupo chini ya ulinzi na wafuasi wake na wasaidizi wake wamethibitisha kuwa walikuwa na taarifa za kuja kwa Askofu wao leo na ndege ya Kenya Airways lakini hawajamuona,na habari walizozipata ni kuwa mara baada ya kushuka vyomba vya Usalama vilimkamata sbb walikuwa wakimtafuta kwa muda mrefu.

Waumini wake na wasaidizi wake wanaendelea kufuatilia kujuwa kiongozi wao anashikiliwa katika kituo kipi cha polisi.Hizi habari zimezua "taharuki" hapa Ubungo kanisani kwake na waumini wapo katika makundimakundi kujadili hatima ya Askofu wao

==========

Habari zaidi...


MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka na kutiwa mbaroni na jeshi la polisi.

Mchungaji Gwajima alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu), majira ya saa moja asubuhi. Alikuwa akirejea nchini kutokea matibabu nje ya nchi.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema, Mchungaji Gwajima alikamatwa wakati akijiandaa kuondoka uwanjani hapo. Alipelekwa kwenye kituo kikuu cha polisi cha Kati.

Wakili wa Gwajima, Peter Kibatala amethibitishia mwandishi wa habari hizi kukamatwa na kuhojiwa kwa mchungaji huyo machachari nchini.

Hata hivyo, Kibatala hakusema, sababu zilizosababisha Mchungaji Gwajima kukamatwa na kuhojiwa.

“…ni kweli Gwajima alikamatwa na polisi akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Baada ya kukamatwa alifikishwa kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya mahojiano ameeleza Kibatala.

Anasema, “baada ya kuhojiwa kwa muda mfupi, jeshi la polisi liliamua kumuchia Mchungaji Gwajima, hadi hapo litakapomhitaji.”

Wakati Kibatala akigoma kueleza kilichosababisha jeshi la polisi kumkamata na baadaye kumhoji Mchungaji Gwajima, taarifa za ndani ya jeshi hilo zinasema, kiongozi huyo wa kiroho amekamatwa kutokana na tuhuma za uchochozi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mchungaji Gwajima anatuhumiwa kutoa kali za uchochezi akiwa kanisani kwake, pale alipodai kuwa Rais John Magufuli, anahujumiwa na baadhi ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waumini wa kanisa lake mwezi uliyopita, Mchungaji Gwajima alimtuhumu rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, kugoma kumuachia uenyekiti wa chama Magufuli.

Akadai kuwa kitendo hicho kinadhoofisha utendaji kazi wa kiongozi huyo mkuu wa serikali na kinasababisha CCM kusheheni mapepo.

Tangu kutoa kauli hiyo, viongozi wajuu wa jeshi la polisi, wamekuwa wakidai kuwa wanamtafuta mchungaji huyo, ingawa baadhi ya watu wanasema, “alichokifanya Gwajima kina mkono wa Ikulu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom