Askofu Gwajima: Kawe tuna barabara za urefu wa KM 1400 sawa na Dsm - Kigoma tumepewa fedha ya km 130 tu hii haikubaliki!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,932
141,897
Mbunge wa Kawe baba askofu Gwajima amesema jimbo lake la Kawe lina barabara zenye urefu wa takribani kilomita 1400 sawa na umbali wa kutoka DSM hadi Kigoma lakini Tarura wamepewa bajeti ya kukarabati kilomita 130 tu.

Gwajima amesema hii haikubaliki na kuwataka watu wa Tarura kujiongeza kwani wao wanahitaji kupewa fungu kubwa la fedha za ukarabati kuliko Tanroads.

Gwajima alikuwa akichangia hotuba ya Rais Magufuli bungeni jijini Dodoma leo.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mlimchagua mtu muuongo anayemdanganya hata Mungu wake, alafu mtegemee afanye vya maana kama mbunge.

Rais wangu Magufuli naye anapenda sana kudanganywa, hebu tuangalie TEAM YAKE: GWAJIMA MBUNGE NA GWAJIMA WAZIRI WA AFYA, MAKONDA, POLEPOLE, BASHIRU, KABUDI, SIRRO nawe msomaji ongezea uwajuao.
 
Huyu Gwajima wito wake ni kumtumikia Mungu huko alikoingia siko kabisa, kazi ya kuhubiri injili haijaisha anakimbilia siasa
 
Mlimchagua mtu muuongo anayemdanganya hata mungu wake, alafu mtegemee afanye vya maana kama mbunge.

Rais wangu Magufuli naye anapenda sana kudanganywa, hebu tuangalie TEAM YAKE: GWAJIMA MBUNGE NA GWAJIMA WAZIRI WA AFYA, MAKONDA, POLEPOLE, BASHIRU, KABUDI, SIRRO nawe msomaji ongezea uwajuao.
Neno kuchagua mnawapa lawama bure wananchi wakati kura ziliibwa, ukumwona Mdee na begi la kura?
 
Back
Top Bottom