Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima amlaumu Halima Mdee kwa mafuriko ya Dar-es-Salaam siku ya leo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,388
Mwandishi: Kusaidia kwenye hii janga, sijui ungependa kutuambiaje?

Gwajima: Kwanza hii hali ni hali ya kusikitisha sana, ni hali ya hatari, mbaya na hali ya kuhuzunisha kwelikweli na mimi hata siamini mtu anaweza kuruhusu wananchi, binadamu wakawa na hali ya maisha hii.

Kwa miaka kumi na mitano mtu ni mbunge wa jimbo hili, maeneo haya Basihaya, Chasimba, Chachui mafuriko wananchi wanaelea, kila mwaka wananchi wananunua vitu vinakwenda na maji, ni hali hatarishi kwa kwa maisha ya wanadamu.

Je yeye anaishi hapa? Je yeye anafanya kazi hapa? Wananchi wanakula wapi sasa hivi? Kwa mfano sasa hivi magodoro yameloana, vitanda vimeshaondoka.

Sasa kwa miaka 15 mbunge alafu anasema nataka tena, unataka watu wafe? Kwa hio ni jambo la kuhuzunisha, niwape pole wananchi na niombe tushirikiane tumalize tatizo hili na litamalizika.

==========


 
Hahaa! Sasa hao Ngwajima hata vitambulisho vya kura vitakuwa vimechukuliwa na hayo mafuriko.
 
Huyo Gwajima ametumia mafuriko kufanya kampeni, anamlaumu Mdee hajatengeneza miundombinu kwani Mdee ndie huwa anakusanya kodi?

Kwanini asimlaumu yule anayesema kila mara mkichagua wapinzani sitawaletea maendeleo wakati yeye ndie kiongozi wa serikali inayokusanya kodi?

Aache kuona watu wajinga, hizo kampeni feki hazimfikishi popote.
 
Gwajima hataiona bunge na kukaa mle ndani Milele sawa na malaya na wakata viuno watakavyokosa kuona ufalme wa Mungu kwa kula kondoo
 
Kakosa hoja huyu mzinzi. Kwani Halima ndiye alipaswa kujenga miundombinu ya barabara? Anakusanya kodi Halima?

BTW, mafuriko yametokea Kawe tu?
 
huyu bwana kama angekuwa ni mwanafunzi wa Yesu lazima angeitwa YuDa Iskariote sio kwa utopolo huu

eti mbunge kashindwa kutengeneza miundombinu
hii hali ya kutokuelewa mambo madodo kama haya naona itakuwa imechangiwa na hali yake ya kusoma form 4 kwa miaka minane
 
Hiyo ndio siasa, matatizo yote kama ambavyo sisi tuna mtupia Magufuli, wana Kawe matatizo yao yote yameletwa na Halima.
 
Gwajima bhana!!! Hizo lawama peleka TARURA na kwa Mkurugenzi,Mbunge siyo mkusanya mapato.Kazi Yale nikuwa semea bungeni na mahalii popote ila kabla hujasema vyema Ukajua unachokisema
 
Hivi jangwani si kwa Zungu, vipi mafuriko hayatokei siku hizi?

Haya ni maeneo yapo ama below sea level au mapito ya maji kutoka milimani, hawa wote wanapigika kwa uasilia wa maeneo yenyewe, hali ya kawe beach ni mbaya sana, kwa bahati tuu ni maeneo ya mchanga. Wabunge au Rais kwa nchi zetu hizi ambazo zina scarce resources lazima wakubali kubeba lawama.
 
Back
Top Bottom