Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza: Ujumbe kwa vyombo vya Ulinzi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
KWA VYOMBO VYA ULINZI

Askofu Mkuu Oscar Romero wa El-Salvador ana ujumbe kwa vyombo vya ulinzi tunapoelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28/10/2020. Baba Mtakatifu Papa Francis alimtangaza kuwa Mtakatifu tarehe 14/10/2018. Askofu Romero alizaliwa 15/8/1917 na kufariki 24/3/1980. Alipadrishwa kuwa Padre 4/4/1942 na kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu 1977. Alikufa kwa kupigwa risasi akiwa altareni akiadhimisha misa ya Sakramenti ya Meza ya Bwana. Muuaji wake, kachero wa serikali, aliingia kanisani kupitia mlango wa nyuma ya Kanisa na kumlenga kwa ustadi mkubwa wakati Askofu Mkuu Romero akiwa ameinua juu kikombe (chalice) cha divai kama ishara ya damu ya Kristo.

Baba Mtakatifu Francis alimtangaza Askofu Romero kuwa mfia dini.

Siku hiyo kabla ya kifo chake, alitoa ujumbe huu kwa vyombo vya ulinzi;

"Kaka zetu na ndugu zetu, mmetoka kwetu na mtarudi kwetu. Mnawaua ndugu zenu. Amri yoyote ya kibinadamu inayoagiza kuua ni batili
maana inajiweka juu ya amri ya Mungu isemayo USIUE. Hakuna Askari aliye juu ya Mungu na Askari halazimiki kutii amri iliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Hakuna anayelazimika kutii amri yenye dhambi ndani yake. Imewapasa maaskari kutii dhamiri hai za kimsingi zilizo ndani yao kuliko kutii amri batili.

Kanisa haliwezi kukaa kimya likiona amri za Mungu zinavunjwa na amri za wanadamu zinaheshimiwa, USIUE au USIIBE. KWA JINA LA MUNGU na kwa Jina la watu wanaoteseka na sauti zao kusikika mbinguni, ninawaamuru na kuwasihi, ACHA UKANDAMIZAJI, ACHA MAUAJI, ACHA DHULUMA".

Askofu Oscar Romero anaongea na wote waliokabidhiwa dhamana ya kulinda uhai wetu. Uamuzi wa kumtii Mungu uko katika vidole vilivyo jirani na kitufe kinachoruhusu risasi na mabomu. MSIKILIZE MUNGU PEKE YAKE.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Askofu Bogonza hudumia kondoo wako, mambo ya vyombo vya ulinzi kwako ni makubwa hujui kitu

Vyombo vya ulinzi ndio vinawapa waumini wako wasaa wa kutafuta sadaka wakuletee jumapili

Bila Amani, usingepata sadaka hapo kanisani kwako
 
But Askofu kama kweli Wewe ni mshauri Kwanini unapenda kuegemea Chadema tu?

Unamaanisha Chadema ndio hawakosei ?

Mbona hukemei ushoga ambaye mgombea wa chadema Aliwatetea ?
 
Askofu Bogonza hudumia kondoo wako, mambo ya vyombo vya ulinzi kwako ni makubwa hujui kitu

Vyombo vya ulinzi ndio vinawapa waumini wako wasaa wa kutafuta sadaka wakuletee jumapili

Bila Amani, usingepata sadaka hapo kanisani kwako
Hapa tutaheshimiana endapo mabeberu wakituletea silaha wachukue madini yote halafu sisi na hao wazee wa Mavi 8 tukutane kwenye kambi ya wakimbizi
 
Askofu Bogonza hudumia kondoo wako, mambo ya vyombo vya ulinzi kwako ni makubwa hujui kitu

Vyombo vya ulinzi ndio vinawapa waumini wako wasaa wa kutafuta sadaka wakuletee jumapili

Bila Amani, usingepata sadaka hapo kanisani kwako
Vyombo vya ulinzi havileti amani amani huletwa na wananchi, wananchi wakiamua askari huweka silaha chini.
BIA SIYO MAJI.
 
Duniani kuna serikali za ki Binadamu, na serikali za kibinadamu huendeshwa kibinadamu

Lakini kuna pahala panaitwa Mbinguni au Kwa jina lingine ni katika Ufalme wa Mungu, na katika Ufalme huo ndiko iliko Haki

Duniani hakuna Haki, ukishupuza shingo kuvunja sheria zilizopo Kwa kigezo cha mtu haruhusiwi kufanya hivi na vile Kwa sababu Mungu kasema, utakwenda na maji huku unajiona!

Tukumbuke, Hapa no duniani na lolote linaweza kufanyika, Mhimu ni kuheshimu sheria zilizopo
 
Back
Top Bottom