Askofu Bagonza: Rais Samia kabadilisha mwandishi wa hotuba?!

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Nimemsikia Rais Samia Suluhu akiwahutubia mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini. Hotuba yake imepiga hatua moja mbele. Rais Samia “ameishavua nguo lakini anaogopa kuoga maji”. Ama maji yana moto sana au ni baridi sana. NAMPONGEZA mwandishi wa hotuba. NAMPONGEZA Rais kwa kuwa mwaminifu wa kilichoandikwa. Pamoja na pongezi hizo, Rais akipenda azingatie haya:

1. Mabalozi alioongea nayo jana ndio aliwauliza WHO ARE YOU? Bila shaka sasa anajua WHO ARE THEY?. Asirudi nyuma. Kwao na mabalozi ni Mtaa wa MTAKUJA. Tunatibiwa kwao, hawatibiwi kwetu.

2. Rais amesema “Sauti za Watanzania Zimesikika kupitia Uchaguzi”. Ni asilimia 2 tu zilimkataa Rais wetu. Sasa nauliza, MARIDHIANO na DIALOGUE ni vya nini?

3. Ili sauti hizo ziweze kusikika ilibidi watu wengine wazuiwe kugombea. Ilibidi vyama vingine vifungiwe kufanya kazi. Ilibidi chama tawala kiende likizo na “vyombo” viongoze badala ya “kuongozwa”. Kama kuna mtu anamsahaulisha Rais wetu ukweli huu, hamtendei haki na analichukia taifa letu.

4. Rais amesema “Tulichofanya Tarehe 29 Oktoba kilikuwa muhimu”. Siku hiyo vilitokea viwili vikubwa. Watu waliandamana wakavuruga uchaguzi. Cha pili watu walikufa wengi. Serikali inaogopa kusema wangapi na waliofika wanaogopa kusema. Umuhimu wa tulichofanya siku hiyo ni upi?

5. Rais amesema kilichotokea siku hiyo “Watanzania sivyo tulivyo”. Hawa waliofanya ni wa taifa gani?

6. Rais ametoa pole kwa kukata internet na ameomba radhi. Akaahidi kuwa jambo hilo halitarudiwa tena. VEMA. Lakini kukatika kwa internet kuliruhusu mambo mengine kufanyika. Kuna vifo, kuna vilema, kuna hasara za kiuchumi. Mwandishi wa hotuba awakumbuke hawa safari ijayo. Uhai ni bora kuliko internet.

7. Taifa letu ni kubwa sana. Si rahisi kuliongoza kwa mfumo mmoja usio na ukaguzi (checks and balances). Ikiwa hata rais anaweza kudhibitiwa na mfumo, waliobaki wana nafuu gani? Mabalozi wanajua haiwezekani. Kama rais anataka “Maendeleo Endelevu”, afanye kisichotegemewa na kisichoweza kutamkwa na washauri (Mzee Mpango na Rafiki yangu Majaliwa). Extra ordinariness is needed because we messed extra ordinarily!

8. Watu wanaotetea HAKI hawako huru mitaani. Ama wako kaburini, Safe House, Nje ya nchi au Mahabusu. Namshauri Rais afanye “uasi”. Afungulie walio mahabusu na Safe House. Arudishe walio ukimbizini (Mabalozi wanawajua kwa kuwa ndio wamewapa ukimbizi). Waliokufa watajwe tumalize matanga. Rais atashangaa atakavyokubalika hata kama hatakuwa salama. Mlinzi wa kweli wa Rais ni wananchi. Kwa sasa wananchi WAMENUNA. Zingatia.

9. Mh. Rais ajue: Hatua zilizochukuliwa Oktoba 29, kuna watu hawaonekani. Ni jukumu lake kutoa hesabu. Namsihi akubali kuna kitu AKIKWENDA SAWA. Awajue, awape pole, nao awaahidi kuwa haitatokea tena. Familia zionyeshwe walipo au walikotupwa. Taifa litapona na Rais atapona. Taifa gonjwa haliwezi kuwa na Rais mzima. Kama hajui, basi sasa ajue kuwa ANAUMWA kwa sababu Taifa linaumwa.

10. Ugonjwa wa Taifa unaongezwa na watendaji wanaomdanganya Rais. Kundi la pili ni la machawa. Makundi haya 2 yanaharibu jitihada za rais kuliponyesha taifa. Eti Mheshimiwa Rais, ili kukukosoa wewe inabidi mtu awe tayari kukaa jela miezi 6? Wewe ni malaika? Serikali yako ni sawa na Mungu? Usitafute mchawi.

Wajaluo sijawasahau: Ninaandaa shindano la Mjaluo mweupe wa mwaka 2026. Mshindi atazawadiwa Kamongo mwekundu.
 
Asante baba askofu nondo tupu
Cc mkuu Pascal Mayalla
JokaKuu
Kalamu
Kiranga
 
Was it necessary to mention luos at the end of this writing?
Wanaomuharibia samia ni wasaidizi wake, huku mitaani umaarufu wake umepungua hadi 10%, hakuna chema atafanya ili kurudisha imani ya watanzania kwake, na watanzania wamejutia sana kuwa na rais mwanamama,,
 
Samia ana uwezo mdogo sana wa kiakili na ndo maana kila akifungua mdomo wake anaishia kujikanganya tu.

She is a piece of shit.
Nadhani ambao hawana akili kabisa ni wasaidizi wake wanaemruhusu azungumze hivyo
 
Back
Top Bottom