Askofu Bagonza: Msajili wa vyama Jaji Mutungi sio mtu sahihi kuandaa kikao cha wadau wa siasa Tanzania

Natoa onyo mapema, atakaempinga Bagonza awe na sababu, ajibu hoja kwa hoja, habari za Bagonza apewe jimbo na Chadema agombee au aache kuchanganya dini na siasa hatutaki kuziona hapa, tabia za walio-graduate kwa kukariri madesa hapa sio mahala pake, hili sio jukwaa la kukariri majibu.

"Afanye kama mama, asilazimishe kufanya kama watangulizi wake, na tabia za mama ni usikivu, anaependa kuleta watoto wake mezani pamoja, huyu kashtaki mama yule kanifinya anawaleta pamoja, ndio sifa ya mama" - Askofu Bagonza.

Kwa kauli hiyo ya Bagonza hapo juu;

- Kwanza ameondoa ile biashara ya kulazimisha kuvaa viatu vya mwingine hata kama havikutoshi, kama vya mtangulizi wako vilikuwa vikubwa, weka store, chukua saizi yako vivae utembee kwa amani.

- Pili, ameonesha kiongozi akiwa madarakani hatakiwi kufuata mawazo ya wengine, afuate mawazo yake na atende kulingana na vile anavyoona inafaa, hapa habari ya system isiwe kisingizio.

Katiba yetu inampa Rais mamlaka ya kifalme na kimalkia kufanya apendavyo, basi ni vyema atumie mamlaka hayo kufanya kwa namna ya kuwafurahisha na kuwaliwaza watanzania bila kujali itikadi zao.

Tatu, kauli hiyo pia inaonesha kufuata mawazo yako sio udhaifu, ni uamuzi wako, na kila mwanadamu ana utashi wake, kilicho muhimu kwako sio lazima kiwe muhimu kwangu. Habari ya kusema mimi ni Rais mwanamke hapa haina nafasi, hakuna asiejua yeye ni mwanamke na ndie Rais wetu.

Achape kazi, aache sheria ifuate mkondo wake, usawa na haki viwepo kwa wote ilimradi sheria ifuatwe.

Kusema yeye ni Rais mwanamke kwa wengine tutaichukulia kama udhaifu kwake, hajiamini; na hii "psychologically" ndio sababu ya yeye kuvunja sheria kwa makusudi ili kutuonesha ubabe wake, ajipandishe; hapana hatushindani, muhimu atumie busara na hekima, huku weledi ukimuongoza kwenye kutimiza majukumu yake, kwani akifanya hivi ndio thamani yake halisi itaonekana.
 
Nashauli Chadema mpeni huyu mzee kadi ya chama ya heshima ya chama.
Naona anapenda sana siasa.
 
Back
Top Bottom