Askofu Bagonza: Kutoka kijiwe cha Polisi Wastaafu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
KUTOKA KIJIWE CHA POLISI WASTAAFU..

Siyo kila nikisikiacho huwa nakiweka katika ukurasa wangu. Leo nilitembelewa na Polisi wastaafu. Wamesafiri kuja kunipa pole. Walipobisha hodi nikaweka mikono nyuma nikisubiri waweke pingu. Badala yake wakashusha kreti ya soda kunihani msiba.

Baadaye soga likanoga na mmoja wao akajenga hoja hizi:

1. Hakuna ubishi kuwa baadhi ya wananchi wanabambikiwa Kesi na Polisi. Rais SSH aliishalikemea hili.

2. Chadema wamekuwa wahanga wakubwa na namba 1 hapo juu. Kasoro hii inazaa chuki ktk nchi.

3. Mbowe kupanga kulipua vituo vya mafuta mwezi Agosti 2020 na akaachwa hadi Julai 2021 ni kumkosea adabu JPM aliyefariki mwezi Machi 2021.

4. Wananchi hawana shida sana kwa Mbowe kushtakiwa. Wana shida kwa kujua mwisho wa siku ataachiwa huru baada ya kuteswa na kupotezewa muda wake. Angekuwa na DHAMANA wala usingeona kelele hizi.

5. Watu wote wanabambikiwa kesi humuita Rais kuingilia kati. Baadhi yao wameachiwa. Huruma ya Rais haiwezi kumfikia kila mtu. Uhuru alio nao Rais unatakiwa katika taasisi.

6. Rais SSH anatakiwa kuanza upya. Hili ni eneo gumu lakini linawezekana. Afikirie yote au baadhi ya haya:

I) Avunje na kuunda upya Baraza la Mawaziri.

Ii) Avunje au aunde uongozi mpya wa bunge (unprecedented but possible)

III) Aitazame tena ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali

iv)Abadilishe miwani yake anayovaa na kuitazama upya timu yake ya usalama (security advisors team).

v) Atangaze uhuru wa habari na uhuru wa shughuli za Kisiasa.

Baada ya kuwasikiliza kwa makini nikakubaliana na ukweli kuwa hekima inaongezeka ukistaafu.
Polisi wastaafu wameniongezea hamu ya kustaafu ili niwe na hekima kama yao.

FE6B891B-972E-4944-AA41-2C85E3B13AD9.jpeg


Askofu Bagonza
 
UJUMBE KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, SERIKALI, JESHI LA POLISI, VYAMA VYA CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NA VINGINEVYO.

Sisi viongozi wa kiroho kutoka madhehebu yote ya dini nchini tupatao 24,000 kutoka Wilaya na Mikoa yote ya Tanzania chini ya Kamati yetu ya Kitaifa ya pamoja kwa Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, wawakilishi wao tunakutana leo kwenye Kongamano la Dua Kijiji cha Bagamoyo, kilichopo Madale, Dar es Salaam kwa ajili ya Dua.

Pamoja na kazi yetu ya kufanya Dua ya kuiombea nchi yetu na Taifa letu, wajibu wetu pia ni kuonya, kukemea vitendo viovu, kutoa ushauri muhimu kama huu wa leo kwenu ninyi tuliowataja hapo juu. Kumbukeni kuwa mbele zake Mungu Mwenyezi, aliye Mungu wa wote wenye mwili, hakuna mkubwa wala mdogo, mwenye nguvu wala dhaifu, Rais wala Mjumbe wa Nyumba Kumi. Sisi sote tunamhitaji Mungu kwa ulinzi, afya na nguvu!

Hivi karibuni, tumeshuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa viongozi wa Serikali unaokwenda sambamba na uporaji wa mali za umma, maneno ya vitisho yasiyozingatia Sheria, umri, maadili ya uongozi, na kiburi cha vyeo. Mbaya zaidi, mambo hayo yanaligawa Taifa kwa kasi kubwa. Aidha vitendo vya kutowasikiliza wenye nchi vimerudi kwa kasi pia. Watu wanapiga kelele kulalamikia tozo kubwa kwenye Gesi na simu lakini wananchi hawajasikilizwa. Wamesema kupanda kwa Gesi kunahatarisha misitu kutokana na matumizi makubwa ya mkaa. Hili limekuwa butu kujibiwa. Hii ni ishara mbaya. Kama mwenye nchi hasikilizwi, anasikilizwa nani?

Tumesikia kauli kali zinazochochea hasira upande wa pili. Kauli hizi zinatoka kwa IGP Simon Sirro kwamba viongozi wanasiasa [wa CHADEMA] na wanachama wao wasiende Mahakamani siku ambayo Mheshimiwa Mbowe atafikishwa Mahakamani. Hili ni moja ya mambo yanayodhihirisha mmomonyoko wa maadili ya weredi wa kazi.

IGP Simon Sirro ameingilia mhimili usio wake kwani Mahakama inao utaratibu mzuri wa kutafuta eneo kubwa ili wananchi wanaofika kusikiliza wapate nafasi hiyo. IGP Simon Sirro alipashwa kushauri kwa kusema; Ndugu zangu, tupo kwenye mazingira ya ugonjwa wa Corona, hivyo tunawaomba mchukue tahadhari kwa kwenda wachache Mahakamani huku mkiwa mmevaa barakoa, badala ya kutoa matamko ya kuwaua na kuwavunja miguu.

Tumbuke Wosia wa Mwalimu Nyerere usemao: 'Moyo kabla ya Silaha'. Vitedo vyote vinavyolalamikiwa na Watanzania kuhusu Jeshi la Polisi vinatokana na kukikuka Wosia wa Mwalimu Nyerere. Ushauri wetu kwa IGP Sirro ni kuwa alirudishe Jeshi la Polisi kwa Wananchi ili liwe ni Jeshi la kulinda raia na mali zao na siyo Jeshi la kuua raia wasio na hatia na kuvunja miguu yao. Kwa kuwa yeye ni Mkristo, atakuwa anajua kwamba Mungu Mwenyezi ni Mungu wa Haki. Tazama, wote washikao upanga wataangamia kwa upanga (Mathayo 26:52). Hata wale wanaowatuma wengine kutumia silaha, watambue kuwa ipo siku ya kesho. Tunatarajia kuwa ujumbe, ushauri na maonyo haya yatazingatiwa na wote tuliowataja hapo juu.

Tunaagiza kuwa Waraka huu usambazwe ili kila Mtanzania ausome kwa lengo la kulinda ustawi wa nchi yetu.

Ni sisi Viongozi wa Dini nchini Tanzania:
Askofu William Mwamalanga
Sheikh Alhaji Abubakar Muhidin Ramadhani
Sheikh Salleh Mussa
Askofu Aizeck Mgaya Kimweri
Padre Dr. Maxwell Furahisha

Nakala kwa: Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - kwa usambazaji
 
Tunataka aman Chadema tunataka haki wao watuache tujazane hapo mahakamni kisha waangalie kama tutafanya hizo fujo wanazozitabili basi watuvunje hii miguu kama alivyoahidi bwana siro
 
Inashangaza na kusikitisha sana jinsi maccm walivyo tayari kufanya kila aina ya udhalimu na dhuluma ikiwemo MAUAJI ili tu kung’ang’ania madaraka.

Tunajenga taifa moja, uhasama,uonevu,chuki,visasi tusivipe nafasi.
 
Mkuu..watawala washenzi sana hawa..
Lakini siku yao inakuja..
Wala haipo mbali.
Kweli wanampa Mbowe kesi ya ugaidi.. ???
Shenzyyyy sana hawa.
 
Back
Top Bottom