Askofu Bagonza: Kumpenda Mungu huku tukiwatesa na kuwadharau Wanadamu ni Ibada ya Sanamu

Askofu Bogonza kuelekea Sikukuu ya Krismasi amesema haya, "Kumpenda Mungu huku tukiwatesa na kuwadharau Wanadamu ni Ibada ya Sanamu na Mungu hawezi kuwa upande wetu hata kama tunamuimba kila siku na Kula viapo kwa jina lake"

Sent using Jamii Forums mobile app
Bagonza ni shetani aliefugwa kanisani, sijui waumini wake wanakwama wapi. Binafsi ningeshahama na kanisa na kubadilisha imani
 
Swali ni lile lile, una uthibitisho ni yeye?.
Hao ni law enforces tuu wanatekeleza majukumu yao, au kuna watu kati tuu ndio wanaofanya madudu haya.

Mimi mwenyewe baada ya kuuliza lile swali siku ile pale Ikulu, contacts zangu zote za consultancy serikali zilifutwa ikiwemo kuzuiwa kufanya Saba Saba na Nane Nane na TBC wakagoma kupokea Programs zangu ikielezwa ni " amri kutoka juu".

Watendaji wa serikali wakisikia tuu ni amri kutoka juu, wala hawaulizi, wao wanajua ni juu kule tuu.

Kuna rais wa nchi fulani ya kiafrika kila akifanya press conference kuna mwandishi fulani free lancer, ana maswali magumu. Maswali ya mwandishi huyo yalikuwa yanachangamsha sana press conferences za rais huyo.

Siku rais akiitisha press conference anauliza kama huyo mwandishi yupo, ili ajiandae vizuri. Kuna siku huyo mwandishi aliuliza swali fulani gumu sana, rais akashindwa kujibu maswali yake, akamwambia unajua wewe mwandishi una nikera sana!.

Press conference iliyofuata yule mwandishi hakuwepo, press conference ikawa boring.

Press conference iliyofuatia rais akauliza kama huyo mwandishi yupo, akaambiwa bado hajafika. Kwenye hiyo press conference ambayo ilikuwa live, rais akatangaza live kuwa haendelei na press conference hadi huyo mwandishi aletwe, akaagiza akaletwe.

Ndipo head wa Special Branch akamnongoneza rais kuwa tangu siku ile rais aliposema huyu mwandishi anamkera, pale pale Special Branch walimtake care and by now he is no more!, he just vanished into thin air kama Azory Gwanda na Ben Saanane wetu. Kiukweli rais akasikitika sana na kuuliza who ordered that?. Ndipo rais akasema japo ni kweli maswali ya yule mwandishi yalikuwa magumu but he was the only sensible and fearless journalist na rais akasema kiukweli alikuwa anampenda sana awepo and he is missing him!.

Msikute hata issue ya Lissu, usikute ile siku rais Magufuli aliposema tuu wasaliti huwa wanafanywa nini vitani, wasiojulikana wakaingia kazini kumshughulikua msaliti wa vita vya kiuchumi, while in reality Magufuli mwenyewe knows nothing.

Hata issue yangu hiyo amri kutoka juu sio juu kule ni hao hao watu kati.

Hivyo tusimlaumu rais kwa kila kitu kuna vitu vingine sio yeye kabisa na hajui chochote!.

Mnaweza kushangaa hata issue ya Eric Kabendera wala rais Magufuli haijui, hii issue ya huyu jamaa pia haijui, ila pia rais Magufuli ni mtu mwenye huruma sana na upendo sana!, just imagine aliwasamehe hadi wabakaji wa minors, kina Babu Seya, akawasamehe mafisadi, wahujumu na watakatishaji fedha. Huruma inaweza kumuingia haswa kwa mateso ya Eric Kabendera na jinsi mama yake anavyoteseka, hivyo inaweza kushangaa soon akamwelekeza DPP kuzifuta hizo kesi zote zisizo na kichwa wala miguu, zikiwemo kesi zote zinazowakabili viongozi wa upinzani.
P
1.Baada ya huyo Rais uliyemtolea mfano kuwaambia Watu wake kwamba yeye aliposema "anamkera" hakumaanisha anamchukia kiasi cha kutaka auawe, kuna Mwandishi mwingine aliuawa na hao watu wa Rais au tukio hili liliwafundisha tabia halisi ya Rais wao?
2.Wewe ni Realistic kama unavyotamba, je,walipokwambia ni amri kutoka juu ulijuaje siyo kutoka juu kabisa bali ni katikati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huwezi kumpenda Mungu wakati jamaa yako uliye jirani naye una mchukia

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Bottom line ni kwamba kila kiongozi anawekwa na Mungu. Awe mzuri au mbaya Mungu ndiye unayejua. Tunaweza kumhukumu kumbe anafanya mapenzi ya Mungu kutunyoosha ili tuweze kumtafuta Mungu.
Nionavyo mimi ulichosema kina ukweli mkubwa Sana. Kwamba Mungu alimwambia nabii Samweli akamtie mafuta Sauli awe Mfalme wa Israel kwa sababu walitaka kuwa na Mfalme. Hii ilikuwa Ni baada ya watu kuelimishwa juu ya tabia na matendo ya huyo Mfalme. Lakini cha kushangaza hatimaye Mungu alimkataa Mfalme Sauli, ndipo Shetani akaingilia kati na kuweka makao yake moyoni mwa Mfalme huyu. Matokeo yake ni ukatili wa kutisha hadi kuwaua watumishi wa Mungu Makuhani akiwemo Kuhani mkuu.
Kwa ukatili huu wa serikali ya awamu ya tano, je, roho inayouongoza si ile iliyomwongoza Sauli kweli!!?
 
Mimi ni realist, kwenye mazuri nasifu.
Jee una uthibitisho wowote wa uovu au hisia tuu?.
P
Pascal Acha ushetani. Acha kuwaTomaso wakati makovu ya Bwana Yesu yako wazi mbele yako. Hivi Lisu na mamia waliotoweka si ushuhuda unaoishi wa ushetani wa Utawala huu!!? Unataka nini zaidi, au unapigania ukuu wa wilaya/Afisa tawala!!!?
 
Ma realist wanasimama kwenye kweli, kama mtu anafanya vizuri maeneo fulani, kuna ubaya gani kumsifu na kumpongeza kwa mazuri hayo?.

Naendelea kusisitiza




P
Hivi hebu tukumbushe, mzee pale magogoni alisema 'mayala' maana yake ni nini?
 
Back
Top Bottom