Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

VIJIWENI hakuna mtu anabishana juu ya DED na DC na CAG na DG-PCCB

Vijiweni hatujui wala hatujali kujua DED ni nini wala DG-PCCB ni nani

Wewe Askofu unakaa kijiweni, kijiwe gani?

Kwanza hutakiwi kukaa kijiweni tangia hapo.
Kijiweni kwetu hiyo ndio agenda
 
Usinitishe we mangi
Haya sasa mzee wa kuongea ushuzi katika ubora wako nafikir message sent km cyo delivery
Kawaite tena wenzako USSR,Patriot na mje na kashfa yenu ya ukabila kaongea Bagonza sa hvi mara kada wa cdm,Toa tena na sifa nyngine ya baba Askofu...
 
[Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
Huu msemo Ni w hekima Koko ya kibinadamu iliyojaa uongo wa kiaskofu

Labda niulize Askofu akiteua mtu au kamati hiyo mtu au kamati inawajibika kwa Nani?

Na huyo mtu anaanzaje kumdanganya Askofu aliyemteua?

Na je akimteua Hakuna terms of refference za kazi za huyo aliyemteua mpaka afanye kazi za kujipendekeza ambazo hazimo kwenye terms of refference za kazi zake?
Kujipendekeza Ni nini? Kama Askofu alete definition hapa
 
Huu msemo Ni w hekima Koko ya kibinadamu iliyojaa uongo wa kiaskofu

Labda niulize Askofu akiteua mtu au kamati hiyo mtu au kamati inawajibika kwa Nani?

Na huyo mtu anaanzaje kumdanganya Askofu aliyemteua?

Na je akimteua Hakuna terms of refference za kazi za huyo aliyemteua mpaka afanye kazi za kujipendekeza ambazo hazimo kwenye terms of refference za kazi zake?
Kujipendekeza Ni nini? Kama Askofu alete definition hapa
Kwa akili zako za kiccm lazima uwe na mtazamo huo..
Ndio maana katiba mpya inahitajika.
 
mbona ni kawaida viongozi wa dini kuingilia kati migogoro ya kisiasa
Kimsingi mnakosea kuandika title ya Bagonza kwenye issue za kisiasa, Askofu Bangoza anaongea sana mambo ya kisiasa kwa mafumbo kama Bagonza na sio hiko cheo cha uaskofu.
 
Kijiweni kwetu hiyo ndio agenda

Hicho ni kijiwe cha Chato, Mbezi Beach na Masaki, wanakoishi the bourgeois class.

Vijiwe vingine vyote nchi nzima tunazumgumzia sukari imefichwa au serikali imebana bei elekezi, Corona imepita au tunaishi nayo, hela ya Mkuu kwenda TFF ilitoka Ikulu kweli au tumepigwa changa la macho, na pia hela aliyochangia kwaya kule kanisani Chato ni ya serikali au ya kwake binafsi na ana mfuko mrefu kiasi gani, kama alivyouliza Nyerere.

Hakuna maaskofu wala maimamu kijiweni kwetu maana kiswahili chetu hapa ni kichafu sana kwa maskio ya watiwa mikono, wala hatumuongelei na hatumjui Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Stakishari Majumba Sita yupo, hayupo, ni nani, anafanya nini, kumzidi nini DC. We couldn't care less.
 
CAG na TAKUKURU

Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na uhusiano kama nani zaidi kati ya Askofu na Mtendaji Kata, Nabii na Sangoma fulani, rubani wa ndege na dereva wa Bajaji au ungo.

Sasa kuna mjadala kuhusu nani zaidi kati ya CAG na TAKUKURU? Inahusu uchunguzi wa fedha za CHADEMA. Mmoja kasema vizuri alipobainisha kuwa kuna mambo ya Takukuru yasiyokuwa ya CAG. Ningeongeza, kuna mambo ya CAG yasiyokuwa ya Takukuru. Mmoja anatafuta wizi zaidi na mwingine anatafuta matumizi mabaya yenye harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Nina matatizo mawili na suala zima:

1. Natamani uhuru (independence) aliyo nayo CAG wangelikuwa nayo TAKUKURU. Nawaomba wasinipige mawe. Kama wanao uhuru, basi mimi nawaombea zaidi. Kwamba, kwa utendaji wa sasa, tunaona Takukuru ni sehemu ya mfumo ule ule unaolalamikiwa na umma. Yaani ni halali mtu kujiuliza Takukuru wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati. Kadhalika, Takukuru wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti! Lakini ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa.

2. Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua Takukuru. Kinadharia pia, Takukuru wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza. Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili, siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Well, nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza. Ndipo ninapojitutumua na kusema, kama tuna dhamira ya kupambana na kuzuia rushwa katika taifa letu, tufanye matatu:

1. Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa. Anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Niwe wazi zaidi; wakati mwingi tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza sana katika kuwadanganya waliotuteua. Mioyo ya watu inaficha mengi.

2. Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo. Nitaambiwa "hayo yote tumeyashika tangu utoto". Tunapungukiwa na nini?

3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.

Hoja yangu ni tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu. Wengi wanasema hiyo ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, padipohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu.

Wenye mawe rusheni, lakini mjue kuwa mada inahusu rushwa. Kurusha jiwe ni sawa na kukiri wewe ni mla rushwa au unashiriki kuilea.
Naunga mkono hoja kiongozi !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewahi Iona kadi Yake?
Huyu Askofu Bagonza na Niwermugizi Ni mabaki ya Lowasa yaliyobaki chadema Hawa hawakuwa wanasiasa kabla ila Lowasa alipoanza harakati zake Ni katika waliopewa maburungutu ya pesa za Lowasa wikuwa viongozi wengi wa dini waliolamba pesa za Lowasa wakaona siasa so ndio hii !!! Wakaacha madhabahu wakawa wanaimba pambo za Mabadiliko Lowasa,Lowasa mabadiliko!!! Badala ya kuimba pambio za Mungu

Wenzao wengi wameachana na Siasa na kurudi madhabahuni Hawa wawili Askofu Niwermugizi na Bagonza Bado wanaota hela za wanasiasa wa Chadema wakingoja kwa Subira kuwa iko siku zitakuja Tena kupitia chadema badala ya kumsubitia Yesu kuwa atakuja Tena duniani kuwachukua wateule wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom