Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Kama watakuwa na huo uthubutu🤝🤝🤝,ila naomba wakimaliza kwa wanasihasa nawaelekeza sehemu mbili ambazo wakiweza nitaanza kwenda msikitini maana watakuwa Ni wajumbe wenye mioyo iloyo shushwa.
Sehemu hizi mbili wengi wameenda kupagusa ila wakirudi hujui waliko pitia.
1.Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,idara ya maji inajihusisha na wizi ama rushwa.
Kwa Kila mwananchi walipofunga bomba la maji ,maji yanatoka Mara mbili kwa wiki ila bili ya maji ikija Ni elfu 12000 kwa mwezi.
Hatujui pesa inayopelekwa idara ya maji na kwa Nini garama zao Ni kubwa kupindukia.

2.Kuna chama Cha walimu CWT sijui wanamahusiano gani na wakurugenzi nchini na maafsa utumishi Hadi hazina kitengo Cha mishahara.
Wanakata watu ambao hata sio wanachama wao,hii jeuri sijui wanajiamini Nini?.
Mtu anakatwa na chama kingine ila CWT wanaingilia na kukata tena hata mhusika hajajiunga na chama hicho wao wanakata tu.

Kama Kuna takukuru nchini kweli ivalie njuga haya mambo mawili,wengine tupo huku vijijini namna ya kuwafkia hao wakubwa Ni ngumu.

Wanajamvi,kuta mbili hizo Happ,wahusika ingieni kazini
 
  • Thanks
Reactions: Pep
"Wengi wanasema ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, panapohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
 
Mapambano dhidi ya rushwa hayatakiwi kuangalia rangi, dini, chama au dini ya mtuhumiwa.
Misingi ya mapambano ni lazima iwe haki na kweli kwa uwazi.
Hata hivyo, makundi ya kisiasa huwa hayana haki na ukweli bali maslahi ya kundi kwa gharama yoyote.
 
CAG na TAKUKURU

Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na uhusiano kama nani zaidi kati ya Askofu na Mtendaji Kata, Nabii na Sangoma fulani, rubani wa ndege na dereva wa Bajaji au ungo.

Sasa kuna mjadala kuhusu nani zaidi kati ya CAG na TAKUKURU? Inahusu uchunguzi wa fedha za CHADEMA. Mmoja kasema vizuri alipobainisha kuwa kuna mambo ya Takukuru yasiyokuwa ya CAG. Ningeongeza, kuna mambo ya CAG yasiyokuwa ya Takukuru. Mmoja anatafuta wizi zaidi na mwingine anatafuta matumizi mabaya yenye harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Nina matatizo mawili na suala zima:

1. Natamani uhuru (independence) aliyo nayo CAG wangelikuwa nayo TAKUKURU. Nawaomba wasinipige mawe. Kama wanao uhuru, basi mimi nawaombea zaidi. Kwamba, kwa utendaji wa sasa, tunaona Takukuru ni sehemu ya mfumo ule ule unaolalamikiwa na umma. Yaani ni halali mtu kujiuliza Takukuru wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati. Kadhalika, Takukuru wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti!😂 Lakini ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa.

2. Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua Takukuru. Kinadharia pia, Takukuru wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza. Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili, siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Well, nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza. Ndipo ninapojitutumua na kusema, kama tuna dhamira ya kupambana na kuzuia rushwa katika taifa letu, tufanye matatu:

1. Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa. Anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Niwe wazi zaidi; wakati mwingi tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza sana katika kuwadanganya waliotuteua. Mioyo ya watu inaficha mengi.

2. Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo. Nitaambiwa "hayo yote tumeyashika tangu utoto". Tunapungukiwa na nini?

3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.

Hoja yangu ni tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu. Wengi wanasema hiyo ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, padipohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu.

Wenye mawe rusheni, lakini mjue kuwa mada inahusu rushwa. Kurusha jiwe ni sawa na kukiri wewe ni mla rushwa au unashiriki kuilea.
Bagonza na wenzake wajikite zaidi kuzungumzia mambo yanayoendana na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zao za dini na si vinginevyo.,
 
CAG na TAKUKURU

Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na...

VIJIWENI hakuna mtu anabishana juu ya DED na DC na CAG na DG-PCCB

Vijiweni hatujui wala hatujali kujua DED ni nini wala DG-PCCB ni nani

Wewe Askofu unakaa kijiweni, kijiwe gani?

Kwanza hutakiwi kukaa kijiweni tangia hapo.
 
VIJIWENI hakuna mtu anabishana juu ya DED na DC na CAG na DG-PCCB

Vijiweni hatujui wala hatujali kujua DED ni nini wala DG-PCCB ni nani

Wewe Askofu unakaa kijiweni, kijiwe gani?

Kwanza hutakiwi kukaa kijiweni tangia hapo.
Aisee..
Shule zifunguliwe tu.
 
Bagonza na wenzake wajikite zaidi kuzungumzia mambo yanayoendana na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zao za dini na si vinginevyo.,
Mjinga wewe sio kila mtu ataona dhuluma atakaa kimya muuweni mtekeni basi Kama anawakera mnaipindisha Sheria viongozi wa chumia tumbo Kama mzee wa upako watakaa kimya ila wateule wa kweli wa bwana watasimama hata kufa.
 
Mjinga wewe sio kila mtu ataona dhuluma atakaa kimya muuweni mtekeni basi Kama anawakera mnaipindisha Sheria viongozi wa chumia tumbo Kama mzee wa upako watakaa kimya ila wateule wa kweli wa bwana watasimama hata kufa.
Hakika akili yako haina akili.
 
Hakika akili yako haina akili.
Mtekeni bagonza si anawakera ? Mnaipindisha Sheria kwasababu za uchaguzi katibu mkuu wenu aligundua madudu kibao ccm mbona hamkupeleka cag tena nyie ccm mnaiba hela za uma kwa nguvu ya dola leo mnaisumbua chadema tena kwa vihela vyao wanavyochangiana wenyewe. Toeni boriti kwenye macho ya CCM mtaona vibanzi kwenye macho ya chadema ila kwa mnayoyafanya Sasa mtafanya hata jwtz idharauliwe maaana hujo meja jenerali mnamtumia vibaya kupindisha Sheria kwasababu za uchaguzi Wana wanajua na huko MTAANI wanachi wanaelimishwa mipango yenu ovu.
 
Mtekeni bagonza si anawakera ? Mnaipindisha Sheria kwasababu za uchaguzi katibu mkuu wenu aligundua madudu kibao ccm mbona hamkupeleka cag tena nyie ccm mnaiba hela za uma kwa nguvu ya dola leo mnaisumbua chadema tena kwa vihela vyao wanavyochangiana wenyewe. Toeni boriti kwenye macho ya CCM mtaona vibanzi kwenye macho ya chadema ila kwa mnayoyafanya Sasa mtafanya hata jwtz idharauliwe maaana hujo meja jenerali mnamtumia vibaya kupindisha Sheria kwasababu za uchaguzi Wana wanajua na huko MTAANI wanachi wanaelimishwa mipango yenu ovu.
Kojoa ulale bro
 
Aisee..
Shule zifunguliwe tu.

Ndio, na makanisa yafunguliwe na wewe urudi kuhudumu.

ASKOFU unakaa kijiweni kubishania DC na DED, teja gani la kijiweni linataka kusikia habari za Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kumzidi nguvu Mkuu wa Wilaya?????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom