Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza aitaka NEC isitumike kudhulumu Watanzania

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,499
51,092
*Lwakalinda Kalikawe Bagonza kaandika hivi:*

NEC WAHURUMIENI WANANCHI
NEC WAHURUMIENI VIONGOZI.

Kuna jambo haliko sawa. Kama liko sawa, basi kuna jambo haliko sawa ndani yangu.

1. Ni mzigo na adhabu kubwa kwa Wananchi kuongozwa na kiongozi ambaye hawakumchagua. Ni kuwatesa wananchi, ni kuwadharau, na kuwadhalilisha. Tuliwakataa wakoloni kwa sababu walitutawala bila sisi kuwachagua. Desemba 9 kila mwaka ni muhimu kwetu kwa sababu tunakumbuka siku tulipoamua kuchagua Viongozi na watawala wetu.

2. Ni mzigo mzito kwa kiongozi kuwaongoza watu ambao hawakukuchagua. Ni dharau na mateso kwake kulazimika kuwaongoza watu ambao hujui kama wanakupenda au hawakupendi kwa sababu hawakupiga kura kukuchagua.

Yote mawili hapo juu ni uchokozi. Tume inawachokoza wananchi kwa kuwalazimisha kuongozwa bila kuchagua. Ni kuwachokoza Viongozi kwa kuwalazimisha kuongoza bila ridhaa ya wananchi. Uchokozi haujawahi kuwa na matokeo mazuri.

Vigezo vya mtu kugombea vinafahamika kikatiba: Raia, umri, dhamana ya chama, kutohukumiwa kifungo, kutohukumiwa kukwepa kodi, muda wa kurejesha fomu nk. Haya hayahitaji wiki kuyaamua

Viongozi wetu uteuliwa/upendekezwa na vyama na kuchaguliwa na wananchi. Tume imeanzisha kundi jipya la Viongozi wanaoteuliwa na tume. Jimbo liitwalo TUME liko mkoa gani? Kata iitwayo TUME iko wilaya gani?

Tulifanya hivyo serikali za mitaa na sasa tunataka kufanya hivyo kwenye bunge. TUNAKOSEA. Hatutakuwa na uhalali wa kudai utii na Maendeleo kwa watu waliolazimishwa kuongozwa na watu wasiochaguliwa. Hatutakuwa na uhalali wa kudai matokeo chanya kwa Viongozi tuliowalazimisha kuongoza bila kuchaguliwa.

Hata baadhi ya mifumo ya kidini isiyochagua Viongozi kidemokrasia hailazimishi muumini kuikubali. Ni kwa mujibu wa Imani, si Sheria.
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe was Uamsho,maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.

Kukemea dhambi ndio kazi zao.. Watu wakinajisi chama chetu au mifumo yetu ya kiutawala wametenda dhambi na lazima viongozi wa dini wawakemee.. Wanajua haki huinua taifa lazima waongee shetani ashindwe.
 
Huyu baba Askofu ana historia ya kumnyanyasaji kisaikolojia msomi Magufuli tangu alipokuwa Katoke Seminary
Tangu wakati wa Corona
Na wakati huu wa Uchaguzi mkuu
Historia gani wakati mtu analaani maovu yanayotendeka wakati huu, tendeni haki kwa wapinzani sanduku la kura litaamua, wacheni huo uhuni wenu wa kuchagulia watu viongozi wasiowataka.
 
Kura inaweza kuhesabika kuwa ni MKATABA kati ya wapiga kura na mgombea/wagombea.

Huwezi kudai maendeleo kwa mtu ambaye hukumchagua, kwa maana hakuna mkataba baina yenu.

Kitendo cha kupitisha wagombea bila mchakato wa sanduku la kura ni kuwaamuru kwenda kumtumikia aliyetaka wawe katika nafasi hizo na siyo wananchi.

Lakini hawasikii.
 
Back
Top Bottom