Askofu Bagonza aamua kumtetea Prof Kabudi, asema yuko sahihi katoka jalalani

S

saidi kindole

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2012
Messages
223
Points
500
S

saidi kindole

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2012
223 500
Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge.

Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa.

Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

=======

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
 
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Messages
2,687
Points
2,000
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2013
2,687 2,000
Nimecheka sana hapo kwenye mtoto mtiifu kunya kinyesi kikubwa. Sasa si kinyesi cha yule mtiifu zaidi mwenye tako kubwa kitakuwa kinajaa karai zima?! Maana kwa msambwanda ule ni ishara kwamba hayupo anaeshiba kama yeye.
 
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
7,001
Points
2,000
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
7,001 2,000
Bagonza ana akili kubwa ukienda na akili kiduchu unaweza usielewe hatukani mtu kwa maneno ya kamusini ni kwa uelewa wa juu, sasa utafikiria anashabikia kumbe changanya na za mbayuwayu
 
Yamakagashi

Yamakagashi

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
7,737
Points
2,000
Yamakagashi

Yamakagashi

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
7,737 2,000
Hahaha sasa Askofu mbona kama anamnanga Propesa Kabudi eti mtoto mtiifu hunya kinyesi kikubwa "na kwamba kaamua kujitoa akili kumtetea Kabudi

Baba Askofu umeeleweka vyema.
 
The golden

The golden

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Messages
725
Points
1,000
The golden

The golden

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2018
725 1,000
Askofu bwana nimeishia kucheka tu. Nimekuelewa sana mtumishi unajua kutumia elimu yako vizuri.

Haaa haaa, mtoto mtiifu unakunya kinyesi kikubwa.
 
Mindi

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Messages
2,325
Points
2,000
Mindi

Mindi

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2008
2,325 2,000
Wala profresa hahitaji hata kuwa na business kuishi pension inatosha.Huyo askofu wako mwongo halafu huwa anajitia yeye jasiri haogopi kusema ukweli.Unataka nikuhakikishie kuwa huyo askofu ni mwoga kusema ukweli na ni muongo? Haya wewe askofu Bagonza askofu usiyeogopa kusema ukweli tutajie majina ya hao maprofesa wastaafu waliochoka kimaisha.Na wameichoka Kivipi?.Tutajie majina baba askofu jasiri usiyeogopa kusema ukweli.
Aisee wewe kweli punguani! Pensheni ya profesa inatosha? kama ingekuwa hivyo, maana yake profesa anauwezo wa kuishi peponi kwa kutegemea mshahara wake tu, maana pensheni ni sehemu tu ya mshahara wa mtu. Kitu ambacho si kweli. Ingekuwa hivyo, maprofesa wasingejiuza kwa kufanya risechi zisizokuwa na kichwa wala miguu, kupiga hela kwenye vyuo, nk. nakuhakikishia kwamba ukiona profesa ana maisha mazuri (ya peponi), basi ujue ana mradi fulani anausimamia, kama Profesa Mukandala mwenye REDET, iliyokuwa inapata mamilioni kutoka nje; au ana madaraka chuoni yanayomuwezesha kuingia mikataba inayomnufaisha, nk. marehemu profesa Shayo (Mungu amweke pema PEPONI) mbona alikuwa na madaladala tu yalipochakaa hakuwa na chochote ispokuwa kijiji cha sayansi ambacho kilimfanya asimamie fedha kutoka makampuni na mashirika enzi hizo. baada ya ubinafsishaji habari hiyo yote kwisha, akaishia kwenye siasa na huko alikuwa na Mark Two moja ndiyo anazunguka kupiga kampeni. alikuja kuponea kufundisha SAUT, mpaka mauti yalipomkuta. Nina mifano ya maprofesa wengi tu, ila kutaja majina ya watu siyo jambo zuri sana. kimsingi hali mbona inajulikana sana tu.
 
E

Essien jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Messages
398
Points
1,000
E

Essien jr

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2018
398 1,000
Wala profresa hahitaji hata kuwa na business kuishi pension inatosha.Huyo askofu wako mwongo halafu huwa anajitia yeye jasiri haogopi kusema ukweli.Unataka nikuhakikishie kuwa huyo askofu ni mwoga kusema ukweli na ni muongo? Haya wewe askofu Bagonza askofu usiyeogopa kusema ukweli tutajie majina ya hao maprofesa wastaafu waliochoka kimaisha.Na wameichoka Kivipi?.Tutajie majina baba askofu jasiri usiyeogopa kusema ukweli.
Binti povuu hili la foma au omo?? Haya kwa niaba kabudi kachoka kifikra, lipumbavu wengine unawajua jazia
 
Lyamber

Lyamber

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Messages
7,905
Points
2,000
Lyamber

Lyamber

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2012
7,905 2,000
Kwa andiko aliloliandika Bagonza hakika huyu mtu ametolewa jalalani ukimlinganisha na ma professa wenzake kama jamaa alistaafu 2016 na uwakili wa viti maalumu alipewa 2009 mana yake ni kwamba uzoefu ni wa miaka 7 tu ukitoa ile kesi ya mgombea binafsi sidhani kama kuna kesi ameshawahi kufungua..na kushinda huyu bwana hivyo ninkweli alikua ana hard time sana kitaani
 
Mdodos

Mdodos

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
298
Points
250
Mdodos

Mdodos

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
298 250
... hoja ya msingi ni kutolewa sijui kuokotwa "jalalani". Kama mtu wa level ya profesa kaokotwa jalalani, je, sisi maskini walalahoi mbumbumbu wajinga sijui tunaishi wapi! Ndio maana hoja inajengwa kwamba za Kabudi ni zaidi ya shukrani; huenda ana ajenda zake nyingine.
That defines our education system and productivity.Yaana pamoja na uprofesa wooote still asingeteuliwa Hali yake ingekua mbaya Sana.Elimu yetu bado sio mkombozi.kbsa
 
Gide MK

Gide MK

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Messages
6,496
Points
2,000
Gide MK

Gide MK

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2013
6,496 2,000
Lugha iliyotumika sio ya kiaskofu.Kazi mojawapo ya askofu ni kulea watoto wanaoshinda majalalani kuwalea kwenye nyumba za kulelea watoto wenye mazingira magumu.Huwezi kebehi aliyetokea jalalani.

Sana sana utampa Pole kwa kuishi maisha magumu nk anyway ni askofu wa kilutheri wao huwa hawana tabia ya kulea watoto wa mitaani wala majalalani kama wa katoliki.

So he can say anything.Kuhusu maprofesa wKistaafu kwa huwa na maisha magumu ni uongo.

Hivi anajua pension ya profesa aliyestaafu kuwa analipwa pesa nyingi tu ambazo hata mshahara alionao askofu bagonza haufikishi hata robo ya anachopokea professor mstaafu Kila mwezi kama pension?.

Kama kaona kuna professor kachoka ni tu sababu ya life style yake.Kama anashinda kwenye kunywa gongo lazima akongoroke.

Askofu anadhani maprofesa waganga njaa kama yeye anayeacha madhabahu na kukimbilia siasa.
Kama kitu hujui ni bora kukaa kimya kuliko kuongea ukaonekana mjinga
 
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
10,232
Points
2,000
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
10,232 2,000
That defines our education system and productivity.Yaana pamoja na uprofesa wooote still asingeteuliwa Hali yake ingekua mbaya Sana.Elimu yetu bado sio mkombozi.kbsa
... huyo mjanja Mkuu! Analitetea "jimbo" lake!
 
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
17,571
Points
2,000
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
17,571 2,000
Nakuaminia Baba Askofu. Jimbo la tumboni si mchezo,na hapo kwenye mtoto mtiifu hukata gogo la ukweli ndiyo umemaliza yote.
 
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
17,571
Points
2,000
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
17,571 2,000
Lugha iliyotumika sio ya kiaskofu.Kazi mojawapo ya askofu ni kulea watoto wanaoshinda majalalani kuwalea kwenye nyumba za kulelea watoto wenye mazingira magumu.Huwezi kebehi aliyetokea jalalani.

Sana sana utampa Pole kwa kuishi maisha magumu nk anyway ni askofu wa kilutheri wao huwa hawana tabia ya kulea watoto wa mitaani wala majalalani kama wa katoliki.

So he can say anything.Kuhusu maprofesa wKistaafu kwa huwa na maisha magumu ni uongo.

Hivi anajua pension ya profesa aliyestaafu kuwa analipwa pesa nyingi tu ambazo hata mshahara alionao askofu bagonza haufikishi hata robo ya anachopokea professor mstaafu Kila mwezi kama pension?.

Kama kaona kuna professor kachoka ni tu sababu ya life style yake.Kama anashinda kwenye kunywa gongo lazima akongoroke.

Askofu anadhani maprofesa waganga njaa kama yeye anayeacha madhabahu na kukimbilia siasa.
Na wewe ni propesa tu kama huyo mwenzako.
 
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2011
Messages
1,018
Points
1,500
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2011
1,018 1,500
Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge.

Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa.

Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

=======

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi cathedrawa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
Siamini kama ni wewe, ila kama ni wewe, jitahidi pia kuboresha kanisa lako hapo cathedral linatia aibu. Si kanisa la hadhi ya jimbo. Umekalia porojo tuu maendeleo hakuna.
 
Mtafiti77

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Messages
658
Points
1,000
Mtafiti77

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2011
658 1,000
Sasa, ina maana mtoto asiyemtiifu anakunya mavi madogo kwakuwa hali akashiba? Hizi falsafa jamani, duh!
 
Forum statistics

Threads 1,304,794
Members 501,517
Posts 31,527,218
Top