Waziri Kabudi: Tanzania haijazuia Maandamano wala Mikutano ya Kisiasa!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
profkabudi.JPG

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi amesema Serikali haijazuia maandamano na mikutano ya kisiasa isipokuwa wanaandaa utaratibu rafiki utakaotumika pasipo kuvunja sheria za nchi.

Kabudi amesema kuwa inatambua umuhimu wa mikutano ya siasa na pindi utaratibu utakapokamilika watatangaza mfumo mpya.

“Maandamano na mikutano ya kisiasa haijazuiwa nchini ila inaratibiwa na imewekewa utaratibu. Ndio maana ninasema haijazuiwa. Hakuna jambo linalofanyika bila utaratibu. Tunasoma sura ya pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kuhusu haki za binadamu bila kusoma ibara ya 30 iliyoweka mipaka ya wewe kufaidi uhuru wako,” alisema.

Alitaja mipaka iliyowekwa kuwa ni mtu kutoingilia uhuru na haki ya mwingine, maagizo ya umma, usalama na afya.

Waziri huyo amesema mipaka hiyo imewekwa pia katika uhuru wa kuabudu na imani ambapo mtu anatakiwa kuifuata anapotumia uhuru wake.

Ameongeza kusema kuwa hakuna uhuru usio na mipaka ambao kuepusha ghasia kwa watu wengine na mipaka hiyo haipo Tanzania pekee bali mataifa mengine pia.

Amefafanua kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi pekee Kusini mwa Jangwa la Sahara yenye Sheria ya Vyama vya Siasa baada ya kurejea katika mfumo wa vyama vingi ambayo imeweka wajibu na majukumu huku vihakikishiwa ruzuku kwa vile vinavyoshinda ubunge na udiwani inayotokana na kodi za wananchi.

Kuhusu maandamano, amesema lazima kuwe na utaratibu ikiwamo kujulikana kwa mahali na siku ya kuyafanya.

Alisema kuna nchi zimeweka utaratibu maandamano ni Jumamosi tu ili siku za wiki watumishi wafanye kazi na kwa nchi za Ulaya maandamano yanafanyika nje ya mji.

Kuhusu utaratibu wa kufuatwa ili kuandamana, alisema Sheria ya Usalama Barabarani imeweka mwongozo.

“Ukiisoma vyema hata magari ya harusi yakizidi 10 inabidi ukaombe ruhusa trafiki kwamba leo mimi mtoto wangu atakuwa anaoa nitakuwa na magari kama 20 hivi,” alisema.
 
Kabudi acha kudanganya watu nchi hii hakuna uhuru wa kufanya siasa kwa chama chochote isipokuwa CCM.

Shaka na Chongolo wanazunguka nchi nzima lakini Mbatia anazuiwa hata mkutano mkuu wa chama chake, Chadema hawaruhusiwi hata kufanya jogging na upuuzi mwingine mwingi.

Kama walisema hajui diplomasia mimi nasema anataka kudanganya wahisani tuu.
 
Hatuhitaji maandamano ya kisiasa.

Tunahijati maji, umeme, ajira na uchumi mzuri.

Huko kuandamana mkaandamane wenyewe.
 
Basi andamana
 
Usiandamane, sio lazima.
Kaa nyumbani usubirie hayo maji na huo umeme.
Hatuhitaji maandamano ya kisiasa.

Tunahijati maji, umeme, ajira na uchumi mzuri.

Huko kuandamana mkaandamane wenyewe.
 
Hatuhitaji maandamano ya kisiasa.

Tunahijati maji, umeme, ajira na uchumi mzuri.

Huko kuandamana mkaandamane wenyewe.
Endeleza pambio za kuletewa ukame na Giza wanakijani ua pambio mlikuwa mkiwaimbia pindi mkiwa meshiba namefurahi pekee
?
 
Uyaratibu Rafiki umeandaliwa Kwa ajili ya CCM tu ***** zao
 
Kabudi acha kudanganya watu nchi hii hakuna uhuru wa kufanya siasa kwa chama chochote isipokuwa CCM.

Shaka na Chongolo wanazunguka nchi nzima lakini Mbatia anazuiwa hata mkutano mkuu wa chama chake, Chadema hawaruhusiwi hata kufanya jogging na upuuzi mwingine mwingi.

Kama walisema hajui diplomasia mimi nasema anataka kudanganya wahisani tuu.
Unapoteza tu muda kumjibu huyu babu wa jalalani. Mweke kwenye ignore list
 
Hatuhitaji maandamano ya kisiasa.

Tunahijati maji, umeme, ajira na uchumi mzuri.

Huko kuandamana mkaandamane wenyewe.
Kwa miaka 6+ mmezuia hayo maandamano na mikutano ya wenzenu mkiwa na kauli mbiu yenu hiyo hiyo, je katika miaka yote hiyo katika hayo uliyoyasema mmeweza kuyapata?
 
Kwa miaka 6+ mmezuia hayo maandamano na mikutano ya wenzenu mkiwa na kauli mbiu yenu hiyo hiyo, je katika miaka yote hiyo katika hayo uliyoyasema mmeweza kuyapata?
Mimi nawakumbusha tu, kuwa kenge sio msikivu.
 
Back
Top Bottom