Askofu Bagonza aamua kumtetea Prof Kabudi, asema yuko sahihi katoka jalalani

Askofu hivi huko kondoo wako wanapata malisho kweli? kama na wewe unafatilia mambo kama hizo...Taifa lina mambo mengi ya kujadili
 
Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge.

Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa.

Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

=======

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
Hahahahah Pascal number two
 
Wala profresa hahitaji hata kuwa na business kuishi pension inatosha.Huyo askofu wako mwongo halafu huwa anajitia yeye jasiri haogopi kusema ukweli.Unataka nikuhakikishie kuwa huyo askofu ni mwoga kusema ukweli na ni muongo? Haya wewe askofu Bagonza askofu usiyeogopa kusema ukweli tutajie majina ya hao maprofesa wastaafu waliochoka kimaisha.Na wameichoka Kivipi?.Tutajie majina baba askofu jasiri usiyeogopa kusema ukweli.
Nadhani hujamuelewa mtoa mada,unaweza ulamsoma tena please
 
Umeandika vizuri but huna data. Maprof/Walimu wa vyuo vikuu wote walikuwa wanalipwa PPF/PSSF ambayo kimsingi ILIKUWA ndogo kutokana na formula/kikototoo tumika kushinda walipwao PSPF/LAPF. Japo wao huenjoy marupurupu MENGI sana na salary ya kawaida. Hili liliwafanya kuishi maisha mazuri wawapo utumishini na duni wakishastaafu wkt watumishi wengine wa LAPF/pspf hutajirika baada ya kustaafu.
Lugha iliyotumika sio ya kiaskofu.Kazi mojawapo ya askofu ni kulea watoto wanaoshinda majalalani kuwalea kwenye nyumba za kulelea watoto wenye mazingira magumu.Huwezi kebehi aliyetokea jalalani.

Sana sana utampa Pole kwa kuishi maisha magumu nk anyway ni askofu wa kilutheri wao huwa hawana tabia ya kulea watoto wa mitaani wala majalalani kama wa katoliki.

So he can say anything.Kuhusu maprofesa wKistaafu kwa huwa na maisha magumu ni uongo.

Hivi anajua pension ya profesa aliyestaafu kuwa analipwa pesa nyingi tu ambazo hata mshahara alionao askofu bagonza haufikishi hata robo ya anachopokea professor mstaafu Kila mwezi kama pension?.

Kama kaona kuna professor kachoka ni tu sababu ya life style yake.Kama anashinda kwenye kunywa gongo lazima akongoroke.

Askofu anadhani maprofesa waganga njaa kama yeye anayeacha madhabahu na kukimbilia siasa.
 
Dah! Mimi nimeelewa sana. Sasa nawaza nifanye nini nifikie uwezo huu wa kufikiri na kutenda kama baba Askofu. KAMWENE BABA ASKOFU, MWANDIKO WAKO TUMEELEWA
Naona wachache sana wamemuelewa Baba Askofu..
Waziri Kabudi akisoma hii lazima ampigie simu Baba Askofu kumpa sikitiko lake..
Baba Askofu kapiga sehemu inayoumiza...kufafanua ni kufanya uchonganishi.
 
Msome vizuri baba askofu. Inawezekana haujamwelewa
Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge.

Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa.

Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

=======

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
 
Askofu hivi huko kondoo wako wanapata malisho kweli? kama na wewe unafatilia mambo kama hizo...Taifa lina mambo mengi ya kujadili
Hawapati huoni muda mwingi anautumia kutafiti watu wanaokunya.Kuwa yupi anakuja kinyesi Cha ukubwa gani na kwa sababu gani anakunya kinyesi kikubwa.Analipwa bure mshahara wa kanisa service yake haina value for money.Wanamlipa kwa kazi ya Uaskofu yeye Wala Yuko kwenye Mambo yake.Mpigeni chini huyu waumini Wala msimwogope.Wachungaji na wainjilisti wa hiyo dayosisi ongozeni uasi wa kumkataa huyu askofu
 
Back
Top Bottom