Rais Samia majukumu uliyompa Prof. Kabudi ni sahihi ila kwenye timu ya mikataba mwongeze Prof. Luoga na Mwambe

Jun 21, 2021
34
29
Nakupongeza Mh. Rais kwa kulipa umuhimu swala la mikataba. Mikataba kwa nchi hii iliturudisha nyuma hivyo ni muda sahihi kuirejea hata kama tulishakosea hapo mwanzo. Waswahili husema kutenda kosa si kosa ila kurudia kosa, ni sahihi kabisa kujirekebisha kwa maslahi mapana ya nchi hii.

Mh. Rais, tunatambua manufaa nchi iliyopata kutokana na juhudi za timu yako ya majadiliano ya mikataba. Kazi hii ni kubwa na inawezekana manufaa tuliyoyapata kwenye sekta ya madini, tukayapata kwenye sekta zingine kama maliasili, gesi asilia, viwanda, mali za serikali zilizotelekezwa n.k.

Naunga mkono kurasimisha kitengo cha majadiliano na marekebisho ya mikataba, na ni sahihi kitengo hiki kikasimamiwa na watu makini na wenye uzoefu wa maswala ya mikataba na uwekezaji.

Sitomuongelea Prof. Kabudi kwa kuwa tayari amekabidhiwa jukumu hilo, ili timu iwe na ufanisi na kujiamini, napendekeza Mh. Rais umuongeze Prof. Luoga ambae kwa sasa ni Gavana wa Benki Kuu, Professa huyu ameshiriki katika majadiliano ya marekebisho ya mikataba ya madini akiwa pamoja na Professa Kabudi, lakini pamoja na uzoefu huo, ni wakili mahiri ambae alikuwa mmiliki wa FK Law Chambers, kampuni ya kiwakili iliyofanya kazi nyingi za mikataba kabla ya kupelekwa kuwa Gavana wa Benki Kuu. Ikiwezekana nae awe wa kudumu kwenye timu hii hata kama nafasi ya uGavana atapewa mtu mwingine, ni kwa maslahi mapana ya taifa.

Mtu mwingine anaefaa kuwa mjumbe wa kudumu kwenye timu hii, ni Mh. Geofrey Mwambe, mchumi mbobezi aliepikwa pale Benki Kuu ya Tanzania na kushiriki katika majadiliano ya uanzishwaji upya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mheshimiwa huyu akiwa mkuu wa kitengo cha uwekezaji nchini (TIC), alishiriki kwa kiwango kikubwa kwenye majadiliano ya kurekebisha mikataba ya madini. Kwa kuwa kwa sasa ni Waziri mstaafu, anao muda wa kutosha kuendelea kulitumikia taifa katika nyanja zingine.

Mheshimiwa Rais kama itakupendeza naomba upokee ushauri ili watu hao wakusaidie.
 
Back
Top Bottom