Askofu Amani apingwa vikali-Mbulu

Katika hali mbaya tulinayo ya kiuchumi,kuna Maaskofu ambao wanatumia vibaya pesa za waumini na kuongeza mzigo wa michango. Askofu Amani wa jimbo katoliki la Moshi ambae ni msimamizi wa kitume katika jimbo katoliki la Mbulu amegonga mwamba na kupingwa vikali na halimashauri ya walei na maparoko alipokuwa akitafuta ridhaa ya kupitisha michango ya sherehe za kumsimika Askofu mpya wa Mbulu. Matumizi ya sherehe iyo ambayo ni million 360 yalipingwa vikali kwani ni makubwa mno na hayana ufafanuzi unaoeleweka.

Watu wengi walihoji kuhusu matumizi hayo katika kikao cha Halimashauri ya walei,maparoko na Askofu ambapo Askofu Amani alishindwa kutoa majibu yanayoeleweka.

Mwisho akasema tutatumia utaratibu wa bungeni wa ndio na hapana katika kupitisha hii michango,alipouliza mnapitisha hii michango wote waliitikia kwa kusema HATUTAKI..majibu hayo hajawahi kutokea katika historia ya jimbo la Mbulu.

Ifahamike kuwa kuna gari ambalo lipo bandarini limenunuliwa kisirisiri kwa ajili ya jimbo pasipo kuwashirikisha waumini wakati huo kuna magari yakutosha kwa ajili ya jimbo. Hayo ni matumizi mabovu ya pesa za waumini. Waumini wamechoka kuburuzwa na viongozi wasiojali maslahi ya jimbo .

Unaongea habari ya KKKT au KANISA KATOLIKI?
Nijuavyo hayo uliyoyasema hayawezi tokea ktk kanisa KATOLIKI!
 
Back
Top Bottom