Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,978
- 30,327
View: https://youtu.be/QsiMwgOP9oY?si=_eQ7wQ-cstcloAz7
ASKOFU HUYU ANATOA HISTORIA YA UONGO
Huyu Askofu anaehutubia wananchi na kueleza historia ya uhuru wa Tanganyika hana anachojua kuhusu hiyo historia anayodhani anaijua.
Tuanze na Father Walsh na suala la Mandate Territories ati Nyerere kaelezwa na huyu.
Suala la Mandate Territories lilijadiliwa ndani ya TAA na TAA Political Subcommittee kutokana na wito wa Gavana Edward Francis mwaka 1949 akiomba mapendekezo kutoka kwa Waafrika ya vipi Tanganyika itawaliwe.
TAA Political Subcommittee ilikuwa na wajumbe hawa: Mufti Sheikh Hassan bin, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando na John Rupia walijadili suala la Mandate Territories na kuwasilisha mapendekezo serikalini 1950.
Mshauri wa kamati hii alikuwa Wakili kutoka Moshi jina lake Earle Seaton.
Atakae kupata zaidi asome kitabu cha Cranford Pratt, "The Critical Phase in Tanzania 1945 - 1968," Cambridge University Press, London, 1976 pp 29 - 31.
Anaweza pia kusoma, Annual Report of the Secretary of TAA 1951 (Sykes Papers).
Huyu Secretary ni Abdulwahid Sykes.
Anaweza pia kusoma mswada wa Dr. Vedasto Kyaruzi, "The Muhaya Doctor."
Anaweza pia kumsoma Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," Chato and Windus, London, 1965.
Hayupo Nyerere wala Father Walsh.
Kumtia Nyerere katika historia hii ni kumfedhehesha na hili si jambo jema kwani hakuwapo katika duru za siasa za wakati ule Tanganyika.
Habari za wazee na Jumbe Tambaza ni hadithi kajitungia huyu Askofu.
Hayo mengine nayakalia kimya kwani ni upuuzi na matusi kwa wazee wetu na matusi hunyamaziwa hayajibiwi.