Askofu aeleza historia ya uongo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266

View: https://youtu.be/QsiMwgOP9oY?si=_eQ7wQ-cstcloAz7

ASKOFU HUYU ANATOA HISTORIA YA UONGO

Huyu Askofu anaehutubia wananchi na kueleza historia ya uhuru wa Tanganyika hana anachojua kuhusu hiyo historia anayodhani anaijua.

Tuanze na Father Walsh na suala la Mandate Territories ati Nyerere kaelezwa na huyu.

Suala la Mandate Territories lilijadiliwa ndani ya TAA na TAA Political Subcommittee kutokana na wito wa Gavana Edward Francis mwaka 1949 akiomba mapendekezo kutoka kwa Waafrika ya vipi Tanganyika itawaliwe.

TAA Political Subcommittee ilikuwa na wajumbe hawa: Mufti Sheikh Hassan bin, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando na John Rupia walijadili suala la Mandate Territories na kuwasilisha mapendekezo serikalini 1950.

Mshauri wa kamati hii alikuwa Wakili kutoka Moshi jina lake Earle Seaton.

Atakae kupata zaidi asome kitabu cha Cranford Pratt, "The Critical Phase in Tanzania 1945 - 1968," Cambridge University Press, London, 1976 pp 29 - 31.

Anaweza pia kusoma, Annual Report of the Secretary of TAA 1951 (Sykes Papers).

Huyu Secretary ni Abdulwahid Sykes.

Anaweza pia kusoma mswada wa Dr. Vedasto Kyaruzi, "The Muhaya Doctor."

Anaweza pia kumsoma Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," Chato and Windus, London, 1965.

Hayupo Nyerere wala Father Walsh.

Kumtia Nyerere katika historia hii ni kumfedhehesha na hili si jambo jema kwani hakuwapo katika duru za siasa za wakati ule Tanganyika.

Habari za wazee na Jumbe Tambaza ni hadithi kajitungia huyu Askofu.

Hayo mengine nayakalia kimya kwani ni upuuzi na matusi kwa wazee wetu na matusi hunyamaziwa hayajibiwi.
 
Mzee siku ukifa ukakuta uislam ikuwa dini ya uongo utajisikiaje
Mdukuzi,
Usililete hili hapa si mahali pake.

Mimi nimesomeshwa historia ya uhuru wa Tanganyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na nilkiwafahamisha walimu wangu kuwa ina kasoro.

Waliponisaili niwaeleza kuwa wazee wangu ndiyo waliounda African Association 1929 na nikawaeleza mengi.

Niliamua kuandika kitabu na sasa ni kitabu maarufu.
Leo watu wanaisoma upya historia ya TANU na historia ya Mwalimu Nyerere.

Hivi punde kuna mtu kwa ujinga tu alionao kawatukana hawa waliokuwa katika picha hiyo hapo chini.
Nimeandika makala fupi kumuelimisha:

MAELEZO MAFUPI KUHUSU PICHA YA DUA SHAMBANI KWA CHAUREMBO MTONI 1956

Kuna kijana kawatukana waliokuwa katika picha ukimtoa Julius Nyerere na John Rupia.
Hakika kakosa adabu.

Lakini dharau hii kwake imekuja kwa kuwa hakusomeshwa historia ya watu hawa.
Nimeamua kumweleza kwa kifupi historia ya baadhi ya hawa wazalendo.

Nimemuasa kijana jizuie na maneno yasiyopendeza kwani hao katika picha baadhi yao ni babu na baba zetu na watu walio na heshima kubwa katika historia ya Tanganyika.

Katika hiyo picha yupo hao hapo chini:

1. Dossa Aziz rafiki wa Mwalimu Nyerere na mfadhili wa TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
2. Mwalimu Thomas Plantan mtoto wa Chief Mohosh, Mzulu kutoka Shangaan na Imhambane.

Thomas Plantan alikuwa Rais wa AA/TAA hadi 1950 alipopinduliwa na vijana.

3. Sheikh Haidar Mwinyimvua Mjumbe Halmashauri Kuu ya TANU na mmoja wanachama wa mwanzo wa TANU 1954.

4. Omar Londo mwanachama shupavu wa TANU 1954 na amepewa mtaa kwa heshima ya mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

5. Abdulwahid Sykes baba yake, Kleist Abdallah Sykes ndiye aliyeasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 na ndiye aliyeandika historia ya African Association.

Mswada alioandika ni Seminar Paper imehifadhiwa East Africana Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Abdul Sykes ndiye aliyempokea Mwalimu Nyerere Dar-es-Salaam na kati ya waasisi 17 wa TANU kadi yake ya TANU ni No. 3.

6. Mwinjuma Mwinyikambi Mjumbe Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe 120.
7. Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958.

8. Rajabu Diwani kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU 1954.
9. Muhsin Mende kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU.

10. Sheikh Mohamed Mattar akijulikana zaidi kama Maalim Mattar mwalimu shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika akisomesha Qur'an.

11. Ali Mwinyi Halwa maarufu Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika ).

Alifuatana na Abdul Sykes kwenda Nansio, Ukerewe kuonana na Hamza Mwapachu kujadili kumwingiza Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA 1953 kisha iundwe TANU 1954.

12. Said Chaurembo Mjumbe wa TAA Political Subcommittee 1950.

Wengine kama Julius Nyerere na John Rupia kwa makusudi nimewaacha kwani wanafahamika vyema."

1693858180825.png
 
Pamoja na yote hayo kuna agenda ya siri iliyojificha nyuma ya unayoandika,agenda ya udini,kuonyesha kuwa uhuru ukiletwa na waislam pekee
Mdukuzi,
Ingekuwa ni agenda ya siri nisingejitokeza hadharani kwa picha sauti, makala na vitabu.

Ingekuwa agenda ya siri nisingekubali kualikwa TBC1, AZAM na kwengine kwingi kuzungumza kuhusu historia ya siri.

Sijapatapo kuseme uhuru ulkipiganiwa na Waislam pekee.

Mimi ndiye nililyeandika historia za watu kama Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, Joseph Mutahangarwa, Dr. Michael Lugazia, Dr. Willibard Mwanjisi, Patrick Aoko, Dome Okochi Budohi, Denis Phombeah, Steven na Peter Mhando na wengine wengi.

Kabla ya kuwaandika wazalendo hawa hakuna aliyekuwa anawajua ila watu wachache sana.
 
Bila dini ya Kikristo Tanganyika ingekuwa bado inatawaliwa na mkoloni.
Ukristo umewafanys wakristo wengi kudanganywa na kufuata wazee wa kanisa badala ya kusoma biblia wenyewe na kuuona ukweli
 
Mzee siku ukifa ukakuta uislam ikuwa dini ya uongo utajisikiaje

Mbona biblia imethibitisha pia uislamu ndiyo dini ya kweli ? Usifuate wazer wa kanisa , Soma biblia with the open mind
 
Biblia iandike uislam uliokuja miaka 600 + baadae

Uislamu upo tokea Adam , mitume wote walikuwa waislamu . Huisomi biblia unawasikiliza Wachungaji makanisani pamoja na wazee wa kanisa, Hao ni matapeli wachumia Tumbo
 
Uislamu upo tokea Adam , mitume wote walikuwa waislamu . Huisomi biblia unawasikiliza Wachungaji makanisani pamoja na wazee wa kanisa, Hao ni matapeli wachumia Tumbo
Mtume mwamedi ni nani katika uislam?
 
Uislamu upo tokea Adam , mitume wote walikuwa waislamu . Huisomi biblia unawasikiliza Wachungaji makanisani pamoja na wazee wa kanisa, Hao ni matapeli wachumia Tumbo
Hapo ndio mnaponyesha kuwa waislam hamna common sense vitu vidogo tu mnashindwa,
 
Hapo ndio mnaponyesha kuwa waislam hamna common sense vitu vidogo tu mnashindwa,

Imani ya Kuamini Kuwepo Kwa Mwenyezi Mungu Mmoja Asiyekuwa na Mshirika (Monotheism)​

Kamusi iitwayo "Webster's New World Dictionary" imelitafsiri neno "Monotheism" kuwa ni imani kuwa kuna Mungu Mmoja tu"

1. Uyahudi, Ukristo na Uislamu zote zinadai kuwa zinaamini na kufuata imani hii. Imani hii ilihimizwa sana na Nabii Musa katika kifungu katika Biblia kinachoeleweka kama "Shema" au shema ya imani ya kiyahudi:
"Sikieni, enyi Israel: Bwana Mungu wetu ni Mungu Mmoja tu" (Marko 12:29)

Alipokuja Nabii Muhammad (saww) takriban miaka 600 baada ya Yesu, alileta ujumbe huo huo:

"Na Mola wenu ni Mungu mmoja tu: hakuna Mungu mwingine isipokuwa Yeye". (Qur'an 2:163)

Ukristo umeondoka kwenye imani ya umoja (upweke) wa Mwenyezi Mungu na umepotea kwenye utata na mkorogano wa Utatu Mtakatifu: Vipi Mwenyezi Mungu anaweza kuwa mmoja wakati unamjumuisha Yesu na Roho mtakatifu?
 
Naona mzee anapambana kuwasifia wazee wanywa gahawa, Wala tende na halua

Papasa

Unajikuta umekua mwamposa peleka hizo porojo zako kuleeeeee

Vijana eti wamesoma hawa ? Hizi ndio hoja ??

Elimika zaidi

Mungu wa Upendo

Fikra ya kwanza kubuniwa na Paulo na ambayo hutumika mara nyingi katika Ukristo kuhusiana naYesu ni Upendo na Mungu.

Kwa mujibu wa wakristo, upendo wa Mungu umekuwepo tu kwa sababu ya kusulubishwa na kufa kwa Yesu - alama ya upendo wa Mungu ni msalaba, kwa mujibu wa Wakristo. Kwa mujibu wa namna yao ya kufikiri, Mungu alitupenda mno hata akamtuma mwanae wa pekee ili apate mateso na hatimaye afe ili amwokoe mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi.

Je, Mungu Aweza Kufa?

Tukiendelea na dhana yenye kutatanisha kwamba Mungu wa Wakristo anaweza tu kusamehe dhambi ndogo kwa kusababisha dhambi kubwa - dhambi ya kumtoa Yesu ili auliwe - dhambi ya kuua, tunalazimika kujadili mada ya uungu ili tuweze kuijadili mada hii. Mungu ni wa milele, alikuwepo tangu na tangu na atakuwepo milele na milele: Hakuumbwa; Hawezi kufa; n.k.

Kama Yesu ni mtoto wa Mungu, kama wakristo wanavyodai, hii ingemfanya na yeye kuwa Mungu pia, ingewezekanaje yeye, kama Mungu, afe msalabani kama wanavyodai?

Ikiwa "mwili wake wa ubinadamu" ndio ulikufa, hii italeta maana kwamba alikufa kama mtu mwingine yeyote. Na kama ni hivi - imani yote ya kuwa Yesu aliteswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanaadamu, itakuwa haina msingi wowote - kwani damu ya mtu wa kawaida haiwezi kuwa fidia ya dhambi za mtu mwingine.
 
Umechagua sehemu unazozipenda na zinazokaribia kuendana na ukitakacho.Very selective! Fabrications tupu!
 
Back
Top Bottom