Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
MUHIMU WA KUWA NA HISTORIA YA KWELI YA UHURU WA TANGANYIKA
Kaandika aliyeandika:
"Lakini bado katika kuunganisha vugu vugu la ukombozi, utapungukiwa sana maarifa ukishindwa kujua Mwl. Nyerere ndo alikuwa Master Planner."
Nimejitahidi kumjibu kumueleza ukweli wa historia ya ukombozi:
Kweli Nyerere ndiye Master Planner?
Uko ushahidi au maneno matupu?
Hebu iangalieni historia ya harakati kuanzia mwanzo Kleist Sykes (1894 - 1949)alipokutana na Dr. Kwegyir Aggrey 1924?
Mnawajua waasisi wa African Association 1929?
Mnajua mchango wa Hamza Mwapachu (1913 - 1962) baada ya WWII alipoanza kuwakusanya vijana wasomi kuleta mabadiliko ndani ya TAA?
Kati ya vijana hawa ni Paul Bomani na Julius Nyerere.
Unaujua mchango wa Abdul Sykes (1924 - 1968), Hamza Mwapachu na Schneider Abdillah Plantan kuleta uongozi mpya TAA 1950?
Katika kipindi hiki kuanzia 1949 unaujua mchango wa madaktari watano: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Michael Lugazia na Dr. Wilbard Mwanjisi katika harakati za TAA?
Hili kundi la madaktari likijiita "Action Group," na historia yao ipo katika mswada, "The Muhaya Doctor," alioandika Dr. Kyaruzi baada ya uhuru.
Unaweza kusoma yaliyomo katika mswada huo katika kitabu cha Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," (1965).
Kuna mapendekezo ya katiba yaliyoandikwa na TAA Political Subcommittee na kupelekwa kwa Gavana Edward Twining 1950.
Mnawajua wajumbe wa kamati hiyo?
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Mshauri wa TAA Political Subcommittee kuhusu ukoloni wa Muingereza alikuwa Earle Seaton.
Mnaujua mchango wake katika suala la UNO na katiba ya TANU?
Mnaujua uzito wa mapendekezo yaliyokuwa ndani ya waraka huo?
Unaweza ukausoma katika kitabu cha Cranford Pratt, "Critical Phase in Tanzania."
Yako mengi ya kueleza.
Katika hayo hapo juu yupo Nyerere?
Sasa wapi unakutana na Nyerere na ukamjua?
Nyerere unakutananae 1952 nyumbani kwa Abdul Sykes TAA Act. President na Secretary.
Je, kaja na mpango wowote wa kuanzisha chama cha siasa?
Hakuwa na mpango wowote.
Master Planner atakuwaje ikiwa hana plan?
Earle Seaton, Hamza Mwapachu na Abdul Sykes