Askofu adaiwa kusambaratisha ndoa ya muumini - Huu ni Uzushi!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
HabariLeo wameandika habari ya uongo

Nimesoma habari yenye kichwa cha habari habo juu, kwa bahati nzuri mimi nafahamu vizuri huo mvutano ninasikitika sana kwamba gazeti kubwa kama habari leo limeshindwa kupata ukweli na kuamua kuchapisha shutuma za uzushi.

Katika Story gazeti linasema limeongea na elisha (mlalamikaji) na Mchungaji (mlalamikiwa), Je gazeti limeongea na mke wa elisha kusikia anasemaje?

Elisha alimuacha mke wake kwa utashi wake mwenyewe, na mkewe ameteseka sana, na amekuwa akisaidiwa na waumini pamoja na ndugu zake wengine, (hata mke wangu mtarajiwa amemsadia), sasa hizo habari za mchungaji kumpangia chumba zinatoka wapi?

Huyu mtu anaishi mbagala na wala sio mkoani, gazeti limeshindwa kumtafuta, kumtembelea kwake kuona anaishi vipi na kumfanyia mahojiano?

MIMI SIO MSHIRIKA WA TAG lakini naifahamu vizuri hiyo story na ni UONGO mtupu! nilitegemea gazeti muweze kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuchapisha hizi shutuma, ingawa katika story yenu mnasema ni shutuma lakini kwa sababu hazina ukweli ndani yake si haki hata kidogo kuzichapa.
 
Shutuma, maana yake kuwa hiyo habari haijathibitishwa... Kwa hiyo inawezekana kuna ya kweli na yasio ya kweli.

Ni sawa sawa na neno Mtuhumiwa.
 
Mtoa mada you are a great thinker bcos umetoa hoja + vidhibitisho.
 
Shutuma, maana yake kuwa hiyo habari haijathibitishwa... Kwa hiyo inawezekana kuna ya kweli na yasio ya kweli.

Ni sawa sawa na neno Mtuhumiwa.

Kama hawana uhakika hakuna haja ya kuandika!

Mtuhumiwa anapitia mahakamani ambako anathitika kama mhalifu au atasafishwa, sasa huyu Mhiche alosingiziwa hivi atasafishwa lini?
 
HabariLeo MMECHEMKA SANA, na ni bahati kwangu mimi ninaijua hiyo story yote kwa hiyo najua kuwa ni uongo, sijui ni story ngapi nimesoma na si kweli ila kwa kutokujua nimejikuta naziamini, HabariLeo wamenipa mashaka sana kwa kweli
 
Kama amesingiziwa, bila shaka anaweza kwenda mahakani ili jina lake lisafishwe, ama sivyo Habari leo waombe radhi kwa kuandika habari za uongo, na kuliaibisha kanisa.
 
Jumapili iliyopita Gazeti 'kubwa' la habari leo waliandika habari iliyolenga kumchafua askofu msaidizi wa TAG ndugu Mhiche na Kanisa kwa ujumla, habari ilikua na heading "Askofu adaiwa kusambaratisha ndoa ya muumini'' ile habari ilikua imejaa uongo mwingi, nilikuja humu jamvini nikaelezea namna naifahamu hiyo story na nikaeleza kuwa kilichoandikwa na HabariLeo kilikua uongo mtupu.

Leo Gazeti limeandika katika ukurasa wake wa kwanza likimuomba radhi askofu na Kanisa kwa sababu 'eti' baada ya kufanya uchunguzi wa kina wamegundua zile shutuma zilikuwa uzushi.

Kitendo cha HabariLeo kuomba msahama ni cha kiuungwana lakini bado nina shida mbili.

1. Si kweli kwamba HabariLeo walijua kuwa hizo habari ni uzushi, Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba HabariLeo walijua kabisa kwamba zili shutuma 'eti kanisa lakubwa na kashfa ya ngono' ulikua ni uongo na bado wakaendelea kuzichapa, HILI NI KOSA KUBWA!

2.Ni jukumu la gazeti kupata ukweli wa story kabla ya kuchapisha gazetini, usumbufu uliosababishwa kwa askofu mhiche na kanisa la TAG hauwezi kufutika tu eti kwa habari leo kuandika kuomba msamaha leo wakati uzushi umeenea kwa wiki nzima, UELEDI (Professionalism) unailazimisha HabariLeo kuwa na uhakika na kila wanachoandika, habari ile ingeandikwa na magazeti ya udaku labda isingekuwa na damage kubwa namna ile. Kuchapa Habari afu 'kama wanavodai wao' kufanya uchunguzi badae ni KOSA KUBWA ZAIDI.

Najua Askofu Mhiche amesamehe, na hii ni kutokana na imani yake, lakini Uzembe kama huu sitegemei HabariLeo mtauacha upite kimya kimya, nasubiri kusikia hatua zilizochukuliwa kwa wale waliohusika kutoa habari ya uongo kwa kiasi hiki, habari ambayo hata angepewa mtoto wa form two kufanyia uchunguzi angebaini kwamba kulikua hakuna chembe ya ukweli
 
Mbona mada iko juu juu au ndo wewe mhusika nini, weka mambo hadharani tukusaidie.
 
HabariLeo wameandika habari ya uongo

Nimesoma habari yenye kichwa cha habari habo juu, kwa bahati nzuri mimi nafahamu vizuri huo mvutano ninasikitika sana kwamba gazeti kubwa kama habari leo limeshindwa kupata ukweli na kuamua kuchapisha shutuma za uzushi.

Katika Story gazeti linasema limeongea na elisha (mlalamikaji) na Mchungaji (mlalamikiwa), Je gazeti limeongea na mke wa elisha kusikia anasemaje?

Elisha alimuacha mke wake kwa utashi wake mwenyewe, na mkewe ameteseka sana, na amekuwa akisaidiwa na waumini pamoja na ndugu zake wengine, (hata mke wangu mtarajiwa amemsadia), sasa hizo habari za mchungaji kumpangia chumba zinatoka wapi?

Huyu mtu anaishi mbagala na wala sio mkoani, gazeti limeshindwa kumtafuta, kumtembelea kwake kuona anaishi vipi na kumfanyia mahojiano?

MIMI SIO MSHIRIKA WA TAG lakini naifahamu vizuri hiyo story na ni UONGO mtupu! nilitegemea gazeti muweze kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuchapisha hizi shutuma, ingawa katika story yenu mnasema ni shutuma lakini kwa sababu hazina ukweli ndani yake si haki hata kidogo kuzichapa.

sasa mbona na wewe umefanya hayohayo yaliyofanywa na hilo gazeti. Heading yako ni kuwa Askofu asambaratisha ndoa ya muumini wake, hapo nimeona umetaja mtuhum alimuacha mkewe je kwanini alimuacha? hebu elezea hapo. katika imani ambayo ni basic ya kikristo huwa hakuna taraka, kwahiyo mpaka bwana elisha anamuacha manake kuna tatizo kubwa alilibaini katika ndoa yake sasa kamuulize kuyo demu wako unayetarajia kumuoa akueleze kwa nini huyo mwanamke aliachwa na wakati imani yenu haiwaruhusu.
Halafu pia ujue Askofu naye ni binadam kushawishika kwake ni kitu cha kawaida, kwahiyo kama aligonga iwekwe wazi tu ili atubie.
 
ungesoma ungeelewa, hiyo ilikua title ya story lakini kuthibitisha sikua nimekurupuka gazeti liliomba radhi wiki chache baadae
 
Sasa wewe kinakuhuma nini ? Au we ndo askofu unajifanya mtu mwingine tukukane kisutu asubui
 
Back
Top Bottom