NI UZUSHI: Serikali ya Eritrea haikutoa amri ya wanaume kuoa wake wawili

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,015
2,191
Zile habari zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba serikali ya Eritrea imetoa amri kuwa wanaume wa nchi hiyo wanatakiwa kuoa wake wawili na wakikiuka watakabiliwa na kifungo jela, ni za uongo na uzushi mkubwa.

Ishu hiyo ilizushwa na mtandao maarufu wa SDEKenya ambao unafahamika kwa kuandika story za uongo na zisizoaminika kwa lengo la kupata 'attention' kwa kuwa si mara ya kwanza kuzusha mambo makubwa ambayo baadae hufahamika kuwa si ya kweli.

Mtandao huu wa SDEKenya ndio uliozusha kuwa Rais Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi na kuifanya ikulu ya Dar es Salaam ikanushe uzushi huo.

Ukweli ni kwamba sheria ya Eritrea hairuhusu wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja na kwamba kama mwanaume akifanya hivyo anaweza kufungwa jela miezi 6 au 12..

Here is what the new 2015 Eritrean penal code specifically states on Polygamy & marriage..
#Eritrea is a nation of law

CZqCVZEUcAA_g90.jpeg
CZqCVZEUcAA_g90.jpeg


==========

Eritrea yakerwa na habari ya wake wawili

Habari ya mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili, ambayo imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo.

''Hata mwendawazimu katika mji mkuu wa Asmara atajua kwamba habari hii sio ya kweli'', afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea Kenya ameiambia BBC.

Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kitengo cha gazeti la The Standard la Kenya cha Crazy Monday.

Baadhi ya watu wametoa maoni yao katika mtandao wa Twitter kwamba wako tayari kusafiri hadi Eritrea ili kutafuta wanawake wa kuoa.

''Jarida la Crazy Monday ambalo huchapishwa na gazeti la Standard hujulikana sana kwa stori zake za udaku, likiwa ni mpango wa kutaka kuwavutia vijana," anasema Mathias Muindi wa BBC Media Monitoring.

Lakini hilo halijazuia taarifa hiyo kuripotiwa katika mataifa ya Nigeria hadi Afrika Kusini huku wengine wakisema kuwa ni ukweli.

Habari hiyo inasema kwamba ili kuhakikisha kuwa kuna wanaume walio wachache nchini humo wanaokidhi mahitaji ya wanawake walio wengi, kufuatia vita kati ya taifa hilo na Ethiopia mwaka 1998-2000, kila mwanamume lazima aowe wake wawili la sivyo afungwe jela.

Lakini afisa wa ubalozi wa Eritrea aliyezungumza na BBC amesema idadi ya wanawake na wanaume inakaribiana.

Waziri wa habari nchini Eritrea Yemane Gebremeskel alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kwamba habari hiyo ni ya uvumi, sio ya kweli na inakera.


Chanzo: BBC Swahili
 
Mimi hata kama sio kweli lakini nimeipenda naomba na huku kwetu Tanzania ije hiyo sheria ya kuoa wake wawili
 
Hii sasa itawekwa kwenye kundi la habari mbaya....Vijana wengi walishaanza michakato ya kuhamia huko wengi watapigiana simu utasikia...Mwana lile dili limebumburuka mwana mwambie mshua acheni na ile ishu ya pasport....Polen.
 
Dah! Nimepata hasara , nilishafika pale mpakani kati ya Kenya na Ethiopia. Nikapata taarifa kwamba si kweli ni uzushi.Sasa muda huu nipo hapa Masabit narejea nyumbani.
 
Back
Top Bottom