Askari wetu wanajifunza sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wetu wanajifunza sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ral, Jun 1, 2011.

 1. r

  ral Senior Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  WAFANYABIASHARA ndogondogo zaidi ya 300 eneo la Manyema, Manispaa ya Moshi, wamefunga barabara ya Manyema inayotokea Mbuyuni kueleka Mtaa wa Viwanda kwa muda wa saa nne, baada ya uongozi wa manispaa kubomoa vibanda vyao zaidi ya 100.

  Walifunga barabara hiyo kwa kuchoma moto magurudumu ya magari na kuzuia watu kupita, huku wakirushia mawe magari ya mizigo yaliyokuwa yakipita na kusababisha gari la Mkuu wa Upelelezi (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro, aina ya Toyota Land Cruiser kuvunjwa kioo cha mbele.

  Barabara hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inatumiwa na magari makubwa ya mizigo, ilifungwa kuanzia saa 12.15 alfajiri hadi saa 5:00 asubuhi, huku wakizuia watu kupite na kusababisha usumbufu kwa wafanyakazi waliokuwa wakielekea kazini kutokea kata za Pasua, Bomambuzi na maeneo jirani.

  Baadhi ya wafanyabiashara hao, Godlizen Joseph na Peter Lukumai, walisema manispaa hiyo imewahamisha kutoka Soko la Mbuyuni miezi miwili iliyopita, lakini cha kushangaza wameanza tena kuwafukuza eneo
  hilo bila taarifa.

  “Awali walipotuhamisha hawakutwambia tusijenge vibanda … leo wanadai
  walisema tuweke tu meza, ilhali tayari tumejenga kwanza kwa gharama kubwa kama mimi nilitumia Sh200,000 leo nimekuta kimebomolewa na hakuna kilichookolewa,” alisema Joseph.Naye Lukumai alisema manispaa iliwagawia maeneo hayo baada ya kulipa Sh120,000 kila eneo la kuweka kibanda na kwamba, alitumia Sh100,000 kugharimia ujenzi wa kibanda.

  Lukumai alisema kutokana kuvunjwa kwa vibanda hivyo usiku bila taarifa, ameibiwa mali ambazo ni nguo zenye thamani ya
  Sh570,000 .

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alisema alipata taarifa kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa hiyo akitaka msaada wa askari.“Kweli kuna vurugu nimepata taarifa kutoka kwa mkurugenzi akitaka nimpe askari, lakini sikutoa askari wangu maana nimeona ni kuvunja
  uhusiano na wananchi na polisi,” alisema.

  Ng’hoboko alisema manispaa walipotoa eneo hilo waliwaona wafanyabiashara hao wakijenga, iwapo walikuwa hawaruhusiwi wangewakataza wakati huo siyo kusubiri vimekamilika na kuomba msaada wa polisi kuvibomoa.

  “Siwezi kupeleka askari wangu na risasi za moto kwa wananchi hao, hii ni kuvunja uhusiano mzuri uliopo kati ya polisi na wananchi,manispaa iliona muda wote vibanda vinajengwa na wakawa kimya iweje leo wanawabomolea?” alihoji Ng’hoboko.


  Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadeta Kinabo, alisema wameamua kuvunja vibanda hivyo baada ya wafanyabiashara kukiuka makubaliano waliyoafikiana; ya kuweka meza siyo kujenga vibanda eneo
  hilo.

  Source: Mwananchi

  Hapo kwenye red
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Huyo mama ni Gamba gumu. Tusubiri cha moto atakiona
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Walau huyu Kamanda ametumia akili. Tena hao viongozi wa manispaa ndio wanaotakiwa kukamatwa. Wanawapelekapeleka wananchi kama hisia zao zinavyowatuma tu? Leo tuwahamishe kesho hisia zao zinawaambia tuwabomolee, halafu tuwaitie polisi. Ujinga gani huu?
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mkurugenzi wa Manispaa anponyimwa polisi wanaoishi katika manispaa yake - hapo ipo kazi. Hakuna utawala wa pamoja huko Moshi.
   
 5. REBEL

  REBEL Senior Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hongera kamanda.mama kinabo namfahamu wakati naishi shanty town,moshi habari zake sio nzuri.
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Manispaa wamekosea kwa kuwavunjia vibanda hao wafanyabiashara..
  Kamanda wa Polisi naye amekosea kwa kutokupeleka vijana wake angalau wakawatulize wafanyabiashara ili kuepusha maafa wanayopata raia wasiohusika. Kumbuka kuna magari ya mizigo yaliyopigwa mawe hapo, sasa wao wana makosa gani? Nadhani hapa ni vita vya Panzi wakati Kunguru Benadeta Kinabo ametulizana Ofisini kwake anapata kiyoyozi..

  Tafakari..
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nampongeza Kamanda Lifan Ngh'oboko. ametumia busara. ni muda mrefu viongozi wa serikali/ccm wamekuwa wakitumia Polisi kuzima vurugu (upheavals) za wananchi zinazotokana na maamuzi yao mabovu plus uzembe. huwezi wabomolea wananchi vibanda vyao usiku na kuharibu mali ilhali uliwaruhusu kuwepo hapo. wanapoinuka kudai/kutetea haki zao unakimbilia polisi kutaka msaada. ni ujinga mkubwa sana wa huyo Ded ambaye apparently yupo kwa maslahi ya ccm. Polisi jiangalieni sana, most always mmekuwa mkitumika as "buffalo soldier"
   
 8. 1

  19don JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  hongera kamanda
   
 9. k

  kiloni JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  utawala wa pamoja =ufisadi wa pamoja
   
 10. n

  ngwini JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Safi sana kamanda
   
 11. P

  Popompo JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33

  unafikiri angepeleka hao polisi ni nini kingetokea?ni vizuri polisi hawakutokea.huyu mama atapata anachopanda!tunamwangalia ole tuamue kuingia barabarani ataujua mji wa moshi vizuri!tuna mambo mengi anafanya ili kuuchafua uongozi wa CDM tunamvutia pumzi sisi wananchi wa manispaa ya moshi!ole wake
   
 12. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  watanzania sasa watatoa adhabu wenyewe kila wakionewa
   
 13. B

  Blessing JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :dance: AISEE HIYO NI TAMU KABISA ----- HOYEEE WAVIJANA WA MOSHI TUMB UP !!!! HUYO BENADETA KINANBO ATAONA CHA MOTO. POMBAVU HUYO MWANAMKE --- AISEE WAVIJANA WA MOSHI MSIMWACHE HUYO DUME LA KIKE NA IKIBIIDI MFANYENI KOLIMBA. YEYE ANJUA SHIDA MNAVYO PATA AU KWA SABABU YEYE ANAKULA KWA UFISADI KWA HIYO ANAONA AMEFIKA SIO. MSIKOBALI KAMBA NI ILE ILE MSIWACHE NA WAKILETA VIYOKOVIYOKO NI KUFA NA KUPONA MSHALE WAVUA GAMBA WENYEWE.

  ALAFU CHOMENI MAPALACE YAO. OOOOOYYYYYEEEEEEEE MAFELA WANGU ------ NORMA TUTAPAMBA NAO HATA KAMA FFU ---- TUKO TAYARI ----- WEKENI MSHALE TAYARI ---- ATUKUPALI ...... PEOPLES PEOPLES PEOPLES P A W A
   
 14. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna wanalojifunza hayan wanayaua ila suala linapokuwa la kisiasa ndo utasikia kuwa ah habati za kiintelijensia mara oh hatuna askari wa kulinda mkutano hivyo usifanyike. mara oh maandamano ni batili na mambo kibso
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Sawa Mkuu,

  Ila chonde chonde msiwashambulie raia wenzenu kwa madai kuwa mnakerwa na Mama Kinabo...
  Kama vipi mfuateni yeye Ofisini kwake mumpe adhabu mtakayoona inafaa, ila siyo kupiga mawe magari ya wasio na hatia..

  CHONDE CHONDE BANDUGU
   
Loading...