mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 821
- 1,343
Askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia maarufu FFU, wakidhibiti eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam leo baada ya wananchi wenye hasira kurushia mawe masafara wa Rais Kikwete. PICHA;ROMI
Msafara wa Rais Jakaya Kikwete leo umepigwa mawe na wananchi wenye hasira eneo la Tegeta Namanag jijini Dar es Salaam.
Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni imekiri kupigwa mawe kwa msafara wa Rais Kikwete wakati msafara huo ukielekea Bagamoyo kutoka jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela amesema kuwa anashikilia baadhi ya wananchi waliodaiwa kurushia mawe msafara wa Rais Kikwete.
Kenyela amedai kuwa wananchi hao walipatwa na hasira baada ya kubomolewa nyumba zao kiholea na tajiri mmoja jijini anayedaiwa kubomoa nyumba hizo ili aweze kujenga kituo cha mafuta eneo hilo.
SOURCE :Taarifa ya Habari ya TBC1 saa mbili usiku, tarehe 30/June/2012 ,IKULU imetoa taarifa kukanusha kua msafara wa Rais haukupigwa mawe na haukusimama popote zaidi ya kusimama kwa Mh. Wasira.