Askari watuliza ghasia za wananchi katika msafara wa Raisi

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
820
1,335
jiwe11.jpg

Askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia maarufu FFU, wakidhibiti eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam leo baada ya wananchi wenye hasira kurushia mawe masafara wa Rais Kikwete. PICHA;ROMI

Msafara wa Rais Jakaya Kikwete leo umepigwa mawe na wananchi wenye hasira eneo la Tegeta Namanag jijini Dar es Salaam.

Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni imekiri kupigwa mawe kwa msafara wa Rais Kikwete wakati msafara huo ukielekea Bagamoyo kutoka jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela amesema kuwa anashikilia baadhi ya wananchi waliodaiwa kurushia mawe msafara wa Rais Kikwete.

Kenyela amedai kuwa wananchi hao walipatwa na hasira baada ya kubomolewa nyumba zao kiholea na tajiri mmoja jijini anayedaiwa kubomoa nyumba hizo ili aweze kujenga kituo cha mafuta eneo hilo.

SOURCE :Taarifa ya Habari ya TBC1 saa mbili usiku, tarehe 30/June/2012 ,IKULU imetoa taarifa kukanusha kua msafara wa Rais haukupigwa mawe na haukusimama popote zaidi ya kusimama kwa Mh. Wasira.
 
Mijitu mingine sijui imeshakunywa? kichwa na utumbo tofauti.
 
liwalo na liwe siku watu wataufumua na rocket launcher, si liwalo na liwe halafu tunawa dump mabwepande!
 
Sasa uongo upi umekanushwa?
Taarifa ya ikulu ya kukanusha iko ap?

Habari ya leo saa mbili tarehe 30/June/2012 TBC1 imetoa taarifa kukanusha kua msafara wa Rais haukupigwa mawe na haukusimama popote zaidi ya kusimama kwa Mh. Wasira.
 
Mzalendokweli naona jamaa kakurupuka tu kuanzisha uzi.

Sikurupuki dogo....katika habari ya TBC tar 30/6/2012 saa mbili usiku IKULU imetoa taarifa za kukanusha tukio kama hilo na kusema msafara huo haukusimama popote zaidi ya kusimama kwa Mh Wasira ambapo ****** alienda kutoa pole za msiba
 
Title na content tofauti, Viroba@work
 
Sasa ikulu imekanusha uongo gani huo wakati wewe mwenyewe umeweka picha za tukio? Au wewe ndiye unayekanusha uongo wa ikulu kwa kuweka picha za tukio?
 
Sikurupuki dogo....katika habari ya TBC tar 30/6/2012 saa mbili usiku IKULU imetoa taarifa za kukanusha tukio kama hilo na kusema msafara huo haukusimama popote zaidi ya kusimama kwa Mh Wasira ambapo ****** alienda kutoa pole za msiba
Ulikurupuka ndio mana haya maelezo hayapo kwe mada.
Edit uongeze haya unayoeleza sasa.
 
Sasa ikulu imekanusha uongo gani huo wakati wewe mwenyewe umeweka picha za tukio? Au wewe ndiye unayekanusha uongo wa ikulu kwa kuweka picha za tukio?

Asante Radhia , tufanye mimi ndio nakanusha uongo wa ikulu kwa kuthibitisha kua msafara ulishambuliwa kwa mawe na kuwalizimu kusimama kwa mda
 
Halafu wenzako wanakuambia umekurupuka, wewe unabishabisha tuu!
Duuuuh Radhia Sweety naona leo umekuwa mkali kwa wanaochangia bamia za chalinze sijui na mrenda.... Punguza basi watu wengi wako keroroooo, by the way its midnite

ki ukweli Mirindimo habari yako wengi hatukuielewa hasa wale wenye aleji na taarifa za Tbc 1, ungetuambia kuwa ikulu inametengua ukweli kuwa uongo. Asante Radhia umemsaidia mtoa mada kidogo kueleweka.
 
Back
Top Bottom