Askari walinda Amani wa JWTZ wauawa Darfur

mkuu this is beyonds idiot badilika kumbuka waliokufa ni kaka zetu, vijana wenzetu huko walipokua awakuwa na bendera ya magamba bali ya taifa ni lazima tufike mahala tutambue utaifa kwanza na pia jiulize kama ndugu yako angekuepo usingeandika ujinga huu muombe sana mungu wako.

Mimi ni CHADEMA hadi kifo, lakini nimehuzunishwa sana na maoni ya baadhi ya jamaa humu eti "kupongeza" mauaji ya vijana wetu. Huu si uzalendo hata kidogo kwani waliouwawa kule ni watanzania wenzetu.
Inawezekana kweli miongoni mwao wamo CCM lakini ninavyoelewa mimi wamo pia wapenzi wa vyama pinzani kama CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, nk. Uthibitisho wa hilo ni kwamba upinzani ulipata kura nyingi zaidi ya CCM ndani ya makambi ya JWTZ na maeneo ya kuishi askari Polisi (Barracks).z
Ni kweli CCM wanakosea sana kuwatumia Polisi kama tawi lao katika kutekeleza maovu yao, lakini hufanya hivyo kwa siri tena wakiwatumia vibsraka wachache waliomo.
CCM wamechemsha upande wa Jeshi (JW)maana makamanda na askari hawako sambamba katika hili la kutumika na CCM.
Kinachotokea Mtwara si unazi wa CCM bali ni utekelezaji maamuzi potofu lakini halali ya serikali yenye rekodi mbovu kabisa katika utekelezaji wa haki za raia wake, inayothubutu kuagiza, tena kupitia bungeni Polisi kufanya jinai dhidi ya raia wasiyoitarajia hatia. Dawa ya hili ni kuiondoa serikali hii ya waganga tumbo na vibwetere ifikqpo 2015. RIP comrades
 
It's pain a lot frnds when its come abt nationality let's put away our differences and look up ts cyo kujifanya uzalendo wa chama nakuanza kutoa mbovu jeshi ni la wananchi na si serikali so tuwe na uchungu nalo tukiskia wanapata majanga kama Haya Poleni sana makamanda kwa kuwapoteza mashujaa wetu wakiwa Kati ya moja ya kazi za kijeshi
 
Kwenye vita kufa ni kawaida mbona uganda wana idadi kubwa ya wanajeshi miaka yote na wanakufaga amsemi au wao ndo wanastaili kufa
 
Poleni sana wanajeshi wetu lakini mtabaki kuwa mashujaa kwani mlikuwa mnalinda amani ya maisha ya wengine so mmekufa kwaajili ya nafsi za watu wengine
 
Nachukua nafasi hii kuwapa pole familia za wahanga hao natafakari maisha yao ya baadae baada ya vifo vya wazazi wao, watoto ndio wataathirika zaidi ,mwanamke anaweza kuolewa tena na mwanaume anaweza kuoa tena lakini watoto je? Serikali ichukue jukumu la kuwasomesha watoto wote wa marehemu hao ili ndoto zao zitimie, Mungu wa rehema kuu awarehemu watu na,wafiwa wote
 
Kwa wanaojua shughuri za jeshi hii habari ni ya kusikitisha lakini si ya ajabu. Unafahamu maana ya ambush! Tena kwa watu ambao ni peace keepers ambamo huwa wanakuwemo polisi,waalimu,mafundi bomba,umeme nk!. Nikupe mfano mmoja wa zamani. Chief Mkwawa wa Wahehe alipanga na kufanya ambush moja kubwa na labda iliyofanikiwa kuliko zote kwa jeshi mahili na lenye zana hatari na imara. Katika ambush ya Chief Mkwawa aliweza kuwaua wajerumani wengi akiwemo kamanda wao mkuu Emily Zelewisky 'Nyundo'. Kwenye ambush haujui adui anatokea upande upi,ana silaha gani na wapo wangapi!. Wakati unawaza hayo na sababu yeye alishapanga hujuma zake mapema,ni rahisi kukupa madhira.Marekani pamoja na jeshi imara wameshafanyiwa ambush kadhaa Iraq,Afghanstan n.k.na kote ziliwapa madhira makubwa.Nilichotaka kusema katika tukio hilo tusiwalaumu askari wetu wala tusibeze uwezo wao.Jeshi letu bado ni imara na ndio maana kwa miaka zaidi ya mitano hakukuwahi kutokea vifo kwa kushambuliwa bali ni ile ajali ya gari iliyotumbukia mtoni tu ambayo walikufa wawili.

Nimeona kwenye cnn,wameuwawa 7,nashangaa kwanini wote ni watanzania.Wanasema ilkuwa ambush na ni kwa mara ya kwanza kwa peace keepers kuuwawa wengi kwa mkupuo mmoja ama shambulizi moja.Inadaiwa kuwa walikuwa outnumbered.
 
R.I.P askari wetu jaman.. japo haijajulikana ni wangapi lakini ni kweli kuna alieuawa au waliouawa! hivyo sote kwa pamoja tunasikitika sana kuyasikia hayo maafa.
 
You don't need peacekeepers in places where there is no peace to keep. I guess you need peace enforcers instead.
.

You are right BUT in matters like this you don't just pick your commandos and invade the place. It needs SPECIAL UN resolution to send peace enforcers. And that is what we are waiting for....
 
SO sad....... R.I.P Brothers IMG_2206.JPG
 
Futa kauli au jipange kutupa habari za uhakika. Iweje unaskia alafu iwe News Alert. Toka nje; shuwaiin"!

Fununu ni habari pia...la kuzingatia je fununu hii ina uzito...kwa jinsi ilivyo lina uzito...jambo lolote linalotokea huanza kwa kusikia au kuona (Milango ya Fahamu) .... ili ufahamu jambo laazima hayo yafanyike ... kwa DAFUR kuona ni vigumu ..... lililobakia ni kusikia...!
 
Hakuna asiyejua umuhimu wa JWTZ,Na kwa kweli watu walíipenda JWTZ zaidi hata ya Polisi,na siku zote wanajeshi wameonekana kama kimbilio na ukombozi,hata Polisi akikumbiza unakimbilia miguuni mwa Mjeshi na unakuwa salama...tunawapenda na kuwashangilia,mahali palipo na fujo wakija polisi kumi na SMG raia wanakuja na mapanga na marungu,lakini wakija JWTZ watatu bila silaha..hata raia mwenye gobore anajificha uvunguni...

Pengine si kwa uwoga,bali kwa heshima tuliowajengea!!hilo ndo jeshi la Sarakikya,Twalipo na Msuguli... Kizazi cha kina Abdulhaman Shimbo kikateleza, kikajiweka upande wa CCM waziwazi wakati wa uchaguzi,kisikumbuke kuwa kuna Watanzania wa CCM,NCCR,CHADEMA,CUF,TADEA,DP nk...mapenzi ya wananchi kwa jeshi lao yakaanza kupungua,sasa yule Shimbo aliyelaumiwa baadae anakuwa Balozi,tena ktk nchi inayojenga bomba la gesi kule Mtwara,kule ambapo kuna Wanajeshi wanafanya kazi ya FFU bila raia kuambiwa kuwa FFU imeshindwa kazi ndo mana JWTZ inaenda...hawa JWTZ kwa kipigo wanaweza kuwa hatari zaidi..mana Polisi wanajifunza haki za binadamu wanapokuwa mafunzoni wanatupiga hivi,Vipi kuhusu JWTZ wasiofungua hata kurasa za "Human Rights Charters"....

Nilitembelea Mtwara, Newala katika vijiji vya Mahuta,Kitangari mpaka Tandahimba!!...CCM inatakiwa ijitafakari juu ya kuwatumia JWTZ badala ya FFU!!.. Wananchi wamepunguza imani kwa JWTZ kutokana na CCM kuliingiza ktk siasa
 
Watu wanajua umuhimu wa jeshi stop lecturing, cha msingi jifikirie kwanini watu hao hao wanadhihaki jeshi lao. Jeshi letu lijichunguze na kujisafisha.
We kama kitu hukipendi unaacha kusoma lakini huna mandotory ya kuniambia niache kuzungumza! Ni mamluki wachache sana wenye chuki na jeshi letu na kamwe mamluki hao hawawezi kuwakatisha tamaa!
 
Kweli nasikiliza hapa Aljazeera live wamesema wanajeshi waliokufa ni wa Tanzania Confirmed by UN Tanzanian Soldies Died in Darfur
 
Kuwa targeted ninakokuzungumzia ndo uko kwa utaifa.Ama husomi posti na kuielewa?ama hujaona niliposema "miongoni mwa maelfu ya peace keepers"?

Sasa ulichotakiwa kujibu ni kunipa namba ama idadi ya wanajeshi wa Tanzania walioko huko,kwasababu kama wako kwa maelfu,thenhaitashangaza sana.

Again,wako maelfu na ni mchanganyiko kutoka mataifa mbalimbali.Ungetafakari zaidi bandiko langu,ungejuwa sikumaanisha "kuwa targeted kwasababu tu wao ni peace keepers".

Na pia si jambo la kawaida kwenye historia ya UN peace keeping kwa wanajeshi hao kuuwawa kiasi hicho(numberwise)kwenye shambulizi moja.Umeelewa mkuu?
Mkuu wangu jmushi1,
Wewe ni mkongwe hapa jamvini na kwa maana hiyo unafahamu nini maana ya mtu ku-quote specific post...kwamba maelezo yake yatajikita kwenye quoted post; that's is the rule of the thumb! Mimi, post ambayo nili-quote ni hii hapa:
Nimeona kwenye cnn,wameuwawa 7,nashangaa kwanini wote ni watanzania.Wanasema ilkuwa ambush na ni kwa mara ya kwanza kwa peace keepers kuuwawa wengi kwa mkupuo mmoja ama shambulizi moja.Inadaiwa kuwa walikuwa outnumbered.
Hivi kweli mwenye kuijibu hiyo post alikuwa analazimika kutoa idadi ya wanajeshi wa Tanzania waliopo Darfur? Jibu ambalo nilikupa ni lile nililojibu nikiamini msingi wa hoja yako kwamba "WHY Tanzanians" na ndio maana nikajibu kwa sababu eneo ambalo ambush ilifanyika linalindwa na Watanzania lakini ktk post ya pili tukapanua mjadala kwamba labda tujadili kwamba waliokuwa ambushed ni Tanzanians; Je, just kwavile ni Tanzanians or kv tu peacekeepers! Hapa maana yangu kubwa ilikuwa ni moja; kwamba kama wali-ambush kv vile tu waliopo pale ni Watanzania manake ni kwamba kama wangewakuta ni wanajeshi wa taifa lingine basi wasinge-ambush lakini kama shida yao ilikuwa ni ku-attack just peacekeepers, basi nazani yeyote ambae angekuwa ktk mazingira mazzuri ya kuwa ambushed; then angekuwa ambushed tu! Hali hii ya ku-attack just peacekeepers or coz are peacekeepers kutoka particular state ni hali ya kawaida.....peacekeepers wengine huwa wanakuwa attacked simply because wanatoka in particular country na attackers unakuta wana beef ni tht country lakini vilevile kuna wengine wanakuwa attacked si kwa sababu ya origin yao bali, ili mradi upo kwenye peace keeping force; tayari wewe ni adui yao; whether u're black, white, colored or whatever!

Sasa labda ndo turudi kwenye ur new concern ambayo haikuwapo kabisa hata kwa kificho kuhusu idadi ya Watanzania waliopo kule....myself, sifahamu lakini source mbalimbali; hususani magazeti ya leo zinasema ni about 800 troops!
 
Last edited by a moderator:
SO sad....... R.I.P BrothersView attachment 102220

Poleni Watanzania.Wanajeshi wetu wamekufa kishujaa.Mmejitolea kwa ajili ya heshima ya Tanzania na Afrika kwa ujumla na zaidi katika kupigania utu na haki ya kuishi ya wanadamu wengine

Huu ni msiba kwetu watanzania,ni alama ya jitihada za ushindi na harakati za kusimama juu na kuwa mbele sikuzote katika kuiishi ndoto ya umajumui wa Africa.

Wachache wanaojaribu kuliharibu jeshi letu hawajaondoa imani yetu kwenu.

Mungu Ibariki Tanzania,Pumzukeni Mashujaa wetu
 
Back
Top Bottom