Askari wa usalama barabarani wakimpiga raia

Hivi unajua mtu anayepigwa anapigwaje???

Umeshawahi kuona mtu anatandikwa wewe???

Huyo mtu amepigwa,au anavutwa vutwa shati??

Huyu hajapigwa labda hujui mtu anapigwaje???
Kwa mtazamo wako wanachokifanya hiki ni sahihi? Pendekezo langu kwa serikali somo la sheria liwe la lazima kwa ngazi zote za elimu
 
Sawa, Ila inawezekana alianza Kwa kumpiga makofi Kabla ya picha kuchukuliwa!
Pengine alivyoona anachukuliwa picha ndipo akaamua kumbuluta !
Yote yanawezekana!
So kama jama nae alianza kumpiga huyo askar..
Sote hatujui timbwili limeanzia wap... In short hajapigwa ila kadhalilishwa kama hakua mkorof
 
Kitendo cha kumgusa raia ni kosa, kitendo cha kumvuta namna ile ni kosa!
Ni udhalilishaji!
WaTZ wengi mnatia huruma aisee?!
Yani kitendo hicho Wewe hujui Kama ni kosa ?
Na ndo maana wenzenu wanatumia udhaifu wenu wa kuto jitambua Kwa kuwafanyia watakavyo!

Kumgusa raia ni kosa.labda askari ana short ya umeme.

Hatujui mazingira ya yeye kuvutwa maana video nayo imerekodiwa kipande,ila si kuvutwa tu hata vichwa utapigwa inategemea umelikoroga kiasi gani.

Daima timiza wajibu wako uwe na haki kudai haki yako.
 
So kama jama nae alianza kumpiga huyo askar..
Sote hatujui timbwili limeanzia wap... In short hajapigwa ila kadhalilishwa kama hakua mkorof
Kwamba askari anaweza kukuchomoa ktk gari tu na kuanza kukuburuza ,mbona sijawahi kukutana na askari wa hivi??
 
Mimi ninaona huyo askari mwingine ameingiza mkono kwenye ghala ya raia, sijui anatafuta risasi au anakagua uimara wa silaha.
 
Hii video ililetwa jana asubuhi halafu wahariri wakaipoteza baada ya wachangiaji kama watano hivi.
 
Hii ni ya dunia nzima, hakuna anayependa kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Khali kadharika hakuna askari anayetoa amri ya kukamata kisha akabishiwa na kunywea dunia nzima huyo askari atakuwa hafai kuwa askari.

Kwa kufanya hivyo hakuna atakayekubali kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi ,hayo mengine ni mbwembwe za sheria, sijui kumpiga MTU. Tuwe wa kweli huyo kapigwaaa!

Huyo kalainishwa kuoneshwa hii ni Police Force.
 
Hujakutana nao kwenye anga zao hata uwe nani wakiamua wanakudunda tu kama ni kesi baadae na sina mfano wa kesi yyte aliyewashitaki na akashinda akafidiwa

No haipaswi kuwa hivyo! Kama wanafanya hivyo wanakosea! Tupo hapa ku bring awareness ! Awareness is empowering !
Hawapaswi kufanya kazi Kwa mazoea !
Kama walikuwa wanakosea wanapaswa kujirekebisha !
Askari lazima ajue kuwa ipo tofauti ya ku deal na raia mwema zidi ya mtuhumiwa!
Kuna vigezo ambavyo vinapaswa kutambuliwa (identified) ili kuweza kujua Mtu flani sasa amekuwa mtuhumiwa au la!
Lakini cha ajabu baadhi ya askari wamekuwa wakiwa treat watu kana Kwamba ni watuhumiwa ingawa Hata mtuhumiwa ana haki zake zinazopaswa kuzingatiwa na Askari vivyo hivyo Hata mfungwa anahaki zake awapo popote Hata gerezani!
 
Hawa ni askari wa usalama barabarani wakimpiga raia sijui tatizo ni nini, na imekuwa kama kawaida kwa hawa askari wa barabarani kuwavizia watu wenye vyombo vya moto na kuwafanyia mambo kama haya



kisheria sijui limekaaje wakuu?


Ni ujinga wenu ndio unasababisha yote haya

Huu ni uzalilishaji Mimi siwezi kukubali nakufa nao
 
Sijajua Kama kuna idara ya modernization ktk jeshi la polisi !
55 years tangu Uhuru jeshi letu linahitaji mabadiliko yatakayo pelekea uboreshwajwi wa huduma Kwa wananchi !
Askari anamsimamisha raia halafu anaaza kusoma vitu Kwenye nje ya Gari bila kumwambia raia kusudi la kumzuia ni nini hasa?
Halafu raia akimuuliza swali anajibu " usinihoji"
Enzi Za ukoloni ndo ilikuwa hivyo lakini sasa haipaswi kuwa hivyo!
Mtuhumiwa anapaswa kuchukuliwa kuwa raia mwema mpaka pale mahakama itakapothibisha pasina shaka kuwa mtuhumiwa ni mkosa!
 
Kuwa Askari ni mgawanyo wa majukumu tu Kwamba mwingine awe Mwalimu , daktari , Mhandisi , Mhasibu , mkulima, n.k sote tunategemeana!
Siyo kutaka kuogopwa au kujiona Mwamba !
 
Back
Top Bottom