Askari wa JWTZ agonga basi la mwendokasi na kulitelekeza gari na kukimbia

Jeshi sio taaluma, labda kama kajiendeleza pia kwa taaluma nyingine za kiraia tofauti na hapo nawafahamu waliofukuzwa au kustafu kazi maisha yao huwa magumu sana huku kitaa na wengi wao ndio hufanya kazi za ulinzi.
NB, binasfi huwa sizalau kazi halali ya mtu maadamu inamuwezesha kupambana na njaa lakini huwa nashaanga wengine kujiweka raia daraja la kwanza.
Mkuu unasema jeshi si taaluma!!!
 
Naangalia ' comments ' za Watu nabaki kushangaa tu. Hakuna Polisi yoyote mwenye ' ubavu ' kwa kuwashughulikia ' Wanajeshi ' Kisheria na yaangalieni / yapimeni sana kiumakini hayo maelezo ya huyo Afande Mambosasa mtaelewa zaidi. Mnapoteza muda wenu bure hao JWTZ ndiyo wenye nchi na kama hilo Gari lilikuwa na number plate ya Jeshi hapo hilo suala ndiyo limekuwa jepesi mno Kwao kwani huyu ' Askari ' Dereva hata akipatikana atasema kuwa alikuwa anawahi suala la ' Kidharula ' na la ' Kijeshi ' na alishatoa taarifa kwa Viongozi wake. Fanyeni tu Kazi zenu msipoteze muda wenu na hili suala kwani hamtaliweza na Mimi naona tayari limeshakwisha.
 
Ujinga mtupu huo kuwabeba hao jamaa
 
Kama alijaribu kuliwasha ili aondoke likamgomea kwa sababu rejeta ilipasuka ulitaka alibebe? Ati kalitelekeza gari, ni gari lilimtelekeza au yeye?? Acheni maneno juu ya jeshi letu. Mwenye makosa hapo ni huyo wa mwendo kazi, hakupaswa kushindana na gari ya jeshi
Duh we jamaa ni noma,mwendokasi tena ndo anamakosa...hahaha
 
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.
Dharura zinaeleweka, zinakubalika, na zina taratibu zake. Tuache kutumia vyeo au taasisi kuhalalisha ujinga. Angekuwa na dharura inayoeleweka ingetolewa order tu na angesafishiwa njia akapita kwa kasi na kwa usalama bila kuhatarisha maisha ya wananchi. Alichofanya huyo dereva ni ubabe wa kipumbavu usio na maana kujiona ni wababe simply wamekabidhiwa maghala ya silaha.
 
Duh we jamaa ni noma,mwendokasi tena ndo anamakosa...hahaha

Sio mwendo kasi tu mazee, wewe ni dereva? Kama ni dereva, ukimwona mwenzio ajaye mbele yako yuko wrong side, mpishe tu, kwa nini uende kuzimu kabla ya siku zako?? Huwezi jua jamaa anakimbia nini, ana mawazo gani au balaa gani. Tunapoendesha barabarani huwa tunapishana na pepo mauti kila dakika. Mwenzio yawezekana ana stress na anatamani kujiua hivyo kakuletea gari umuue.
 
Mkuu unasema jeshi si taaluma!!!
Ndiyo, kwani wewe umeshaga sikia tangazo la ajira serikalini au taasisi binafsi wanawahitaji hao zaidi ya kazi za ulinzi?

Unaweza ukawa mwanajeshi lakini pia ukawa na fani nyingine za kiraia kama ufundi, uwalimu, udaktari, unesi nk tofauti na hapo huku uraiani itakuwa ni kulinda goli
 
Gazeti Lilishuhudia ajali hiyo lakini halikukatiri namba za gari na kuishia kumuuliza Mambosasa ambaye pengine hakuwapo eneo la tukio.
 
Acheni maneno juu ya jeshi letu. Mwenye makosa hapo ni huyo wa mwendo kazi, hakupaswa kushindana na gari ya jeshi
mkuu uko serious au unatania.?yani mwenye bas la mwendo kasi ndo ana makosa?[/QUOTE]
Hadi niandikapo msg hii bado simwelewi huyu jamaa .... nimejitahidi kuifikirisha akili yangu bado simwelewi
 
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.

Kama alikuwa na Haraka mbona amekimbia na kuacha gari?, au huyo MJWTZ alikuwa anakimbilia hiyo haraka?

Hao jamaa ni wavunjifu wakubwa wa sheria za Barabarani, hawataki kabisa kufuata sheria, na siku zote wakiwa na haraka na mambo yao lazima watakuwa na gari la kuwaongoza
 
Daah hawa watu sikuhuzi wanakuta miungu yani.. Jana tulikua tunatoka ferry kuja kinyerezi wakati tunatOka pale... Wakavamia upande wa site yetu hadi almanusra wasababishe ajali sasa yule dereva akawatukana kwasababu hakujua kuwa ni wao... Weee wao ndo walikosea lakin polisi yule alietaka kisababisha ajali akashuka akampa mangumi yule dereva hadi akamtoa madamu then hao wakasepa .... Mm wananikera kwa kweli tabia za ajabu!!
 
Back
Top Bottom