Bodaboda agonga Basi la Mwendokasi na kufariki dunia

Bodaboda agonga Basi la Mwendokasi na kufariki dunia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,853
Screenshot_2023_09_12_12_25_35_071_com_instagram_android_edit.jpg

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Dereva wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda kuingia katika Barabara ya Mabasi Yaendayo Kasi (DART) kwenye Mataa ya kuelekea Lumumba karibu na Kituo cha Mwendokasi cha Fire na DIT Jijini Dar es Salaam.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam imethibitisha kifo pamoja na kutokea kwa ajali hiyo, ambapo imeeleza taarifa kamili itatolewa baadaye.
 
Boda boda ni tatizo kubwa Sana , huu usafr sio wa kupanda ukiwa highway , na hata barabara za DSM waogope hawa watu , kukuua ni kugusa tuu , labda humo ndani ndani kwenye makazi ya watu unaweza panda akusogeze vituoni
 
Bodaboda bodaboda!!!!!

Nashauri kila Jiji litunge sheria ndogo za kudhibiti waendesha bodaboda.
Zitungwe sheria ndogondogo maalum, inaweza ikawa ya nchi nzima au kwa kila jiji
Halafu kama vile hawa jamaa polisi wamewasusa, wamewaacha wajifie watakavyo.

Nimepita mikoa mingi, hawa jamaa hawafuati sheria za barabarani kabisa wanapoendesha pikipiki zao na polisi wanawaona lakini hawachukui hatua zozote.
 
Back
Top Bottom