Askari wa JWTZ agonga basi la mwendokasi na kulitelekeza gari na kukimbia

Wewe ndiyo unaonyesha ubashite wako hapa, eti hawalali kulinda watu! Hebu tuambie hawalali kulinda watu dhidi ya nani?

Nyinyi mbona mnapenda kuwashushia heshima polisi?
Japo siwapendi kabisa CCM lakini nakiri huwa naona polisi wanapiga doria mitaani kulinda watu wa kawaida kabisa na mpaka wakati mwingine wanauwawa wenyewe.

Hao wengine naona kama vile kazi yao kubwa ni kuulinda utawala.
Kila mmoja na mgawanyiko wa majukumu yake
Polisi - analinda raia na mali zao
Mwanajeshi - analinda nchi na mipaka yake
Ikitokezea siku ukiona wanajeshi nao wako mitaani na magari yao wakifanya doria kama wafanyazo polisi basi ujue kimebuma.
 
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amegonga basi la mwendokasi na kusababisha madhara kwa abiria na basi, huku akikimbia na kutelekeza gari alilokuwa akiliendesha.

Tukio hilo limetokea juzi maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam, baada ya dereva wa gari hilo kuingia kwenye barabara ya mwendokasi kisha kugongana na basi lililokuwa na abiria.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akiwataka madereva wote bila kujali ni taasisi gani kufuata sheria za nchi na kuacha kutumia mabavu.

Mambosasa alisema dereva huyo alifanya makosa kwa kuingia njia ya mabasi yaendayo kasi huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kinyume cha sheria.

"Huyu dereva ana makosa, kwanza alishindwa kuheshimu taa zinazoongoza magari na hairuhusiwi kupita katika njia hizo za mwendokasi. Baada ya kusababisha ajali hiyo, alilitelekeza gari na kukimbia", alisema Mambosasa.

"Namba za gari la jeshi (JWTZ) kwa sasa sizikumbuki kwa kuwa nimetoka ofisini nashughulika na masuala ya mafuriko".

Kuhusu madhara ya ajali hiyo, alisema watu wachache waliumia na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu na baadaye kuruhusiwa.

Mambosasa alisisitiza kuwa madereva wa majeshi wanatakiwa kufuata sheria za nchi bila kutumia mabavu ama cheo.

"Nilishasema hakuna ambaye yuko juu ya sheria. Ni vizuri hao madereva wa Jeshi wakafuata sheria za barabarani na hairuhusiwi kutanua kwenye barabara ambayo si njia yako", alisema Kamanda Mambosasa.

Aidha, alisema kuna magari ambayo ni dharura yaliyoruhusiwa kupita kwenye njia ambayo si yake kinyume cha hapo, mengine yote yanatakiwa kufuata sheria zilizopo.

Gazeti hili lilishuhudia gari ya Jeshi ikipita katika njia ambayo si yake katika eneo la Riverside Ubungo na kumgonga mwendesha bodaboda ambaye alikuwa kwenye njia yake.

Chanzo: Nipashe
Sasa afande Mambosasa ni magari gani hayo yaliyoruhusiwa kupita kwenye hiyo njia ungeyataja pengine ingetusaidia,lakini kuna yale yenye namba PT kwa hakika haya magari yanaendeshwa kitemi sana au ndiyo hayo yenye kibali maalum?
 
Kwahiyo unashauri vipi, waachishwe kazi wote kwa vile umuhimu wao kwasasa haupo? Kisha ile mipaka utakwenda kuilinda wewe? Umemaliza shule lini? Na kidato cha ngapi?
Waendelee na kawaida ila mi sitambui mchango wao.
 
mkuu umepiga viroba kule mpakani nani analinda. doria za baharini nani anafanya kuna vikosi vya rada zanzibar nani anafanya, sema we poyoyo nisije kutoa siri za nchi hapa
Kumbe nawe mlisha mbu ndy maana povu jiingi, Ok sawa mnatulinda nyie na sio mungu.
 
Kama alijaribu kuliwasha ili aondoke likamgomea kwa sababu rejeta ilipasuka ulitaka alibebe? Ati kalitelekeza gari, ni gari lilimtelekeza au yeye?? Acheni maneno juu ya jeshi letu. Mwenye makosa hapo ni huyo wa mwendo kazi, hakupaswa kushindana na gari ya jeshi
Mkuu naona unaturingishia uwezo wako mdogo wa kufikiri...
Sawa tumekuelewa.
 
Maswala yao ya nidhamu ni jeshini sio barabarani, vile vile kila chombo na mamlaka yake, elewa hilo.
Acha kutete upumbavu. Kama wadhani alikuwa sahihi kwanini alikimbia, na swali alikuwa na nani garini acha kutetea ugoro
 
mkuu umepiga viroba kule mpakani nani analinda. doria za baharini nani anafanya kuna vikosi vya rada zanzibar nani anafanya, sema we poyoyo nisije kutoa siri za nchi hapa
Mkuu hiyo ndiyo ajira waliyo chagua.Ukisema hawalali sio kweli kila mtu ana zamu (shifti) yake hakuna anayefanya kazi masaa 24. Labda wakuu tu nao hulipwa kwa kuwa tayari kuitwa au kutoa mwongozo (stand by) kama iwavyo hata kwa kampuni binafsi pia. Hata hospitali 24/7 na sio wao tu hata Airport , bandarini n.k kazi zao ni za zamu (shifti).Dharura za kijeshi au polisi wana ving'ora maalumu au taa za gari ambazo hata raia wa kawaida unaweza kutumia na trafiki polisi akakuelewa na sio yeye tu, hata madereva wengine waka kupisha bila kusababisha ajari kama amburance,fire force n.k.
 
Mkuu alisema gari itayo pita njia ya mabasi yaendayo kasi wafungue matairi ya gari hiyo, Je hiyo gari ya JWTZ namba ( hazijulikani) imefunguliwa matairi au bado ?
 
Acha kutete upumbavu. Kama wadhani alikuwa sahihi kwanini alikimbia, na swali alikuwa na nani garini acha kutetea ugoro
Hivi huwa unasoma kilichoandikwa au unaandika ukiwa umefumba macho?
Soma nilichoandika hapo kulingana na post yako
Naelewa zaidi ya ujuavyo wewe, sheria za nchi ziko pale pale, gari litakwenda kituo cha polisi na hao Mp watafatilia mchoro wa ajali kwa polisi, kisha ndio gari litachukuliwa huko jeshini. Kuwa na akili
 
Acha kutete upumbavu. Kama wadhani alikuwa sahihi kwanini alikimbia, na swali alikuwa na nani garini acha kutetea ugoro
Niliongelea sheria za nchi na sijatetea ujinga, sheria za nchi ziko pale pale hakuna cha jwtz wala nani, kama gari limepata ajali polisi watakuja kupima ajali, gari litachukuliwa kituoni then hao wenye gari watakwenda kulifuata huko, kama una kumbukumbu nimequote aliposema kuwa "gari litachukuliwa jeshini then uone kama hao polisi watalifuata"
 
Tusubiri mrejesho kama gari hilo litapelekwa kituo cha Polisi au jeshini.Na ni nani ataye kwenda kulitoa. Wao wana husika na masuala ya nidhamu jeshini pia, sio escot tu.
Narejea tena, gari litakwenda polisi hiyo ni "traffic case"
 
mkuu umepiga viroba kule mpakani nani analinda. doria za baharini nani anafanya kuna vikosi vya rada zanzibar nani anafanya, sema we poyoyo nisije kutoa siri za nchi hapa
Kwani hapa kazi tu, hapahitaji zile dhama za ukweli na uwazi. Maana enzi zile hata hizo rada unazo zitaja taja zilipo kuwa mbovu na ni zile zilizo kuwa zina tulinda akina sisi, tuli juzwa kuwa ni mbovu ndipo mkulu wa mwendo kasi akanunua zingine,nayo sio siri? Na tuna mshukuru moto yake ya "Hali mpya na kasi mpya" imeleta mwendo kasi iliyo gongwa.Gharama ya barabara zile sio mchezo,chini ya zege lake kuna nondo zilizo sukwa si chini ya 16mm.
 
Wewe ndiyo unaonyesha ubashite wako hapa, eti hawalali kulinda watu! Hebu tuambie hawalali kulinda watu dhidi ya nani?

Nyinyi mbona mnapenda kuwashushia heshima polisi?
Japo siwapendi kabisa CCM lakini nakiri huwa naona polisi wanapiga doria mitaani kulinda watu wa kawaida kabisa na mpaka wakati mwingine wanauwawa wenyewe.

Hao wengine naona kama vile kazi yao kubwa ni kuulinda utawala.
Acha kuropoka kama hujui kaa kimya.
Ulitaka wanajeshi nao wapige doria?
Kama hujui, polisi ndo wana jukumu la kulinda raia na mali zake ndo maana wanafanya doria physically lakini wanajeshi wana linda mipaka.... Kwa hiyo kila mtu na majukumu yake
 
Back
Top Bottom