Askari wa JWTZ agonga basi la mwendokasi na kulitelekeza gari na kukimbia


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,671
Likes
51,839
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,671 51,839 280
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amegonga basi la mwendokasi na kusababisha madhara kwa abiria na basi, huku akikimbia na kutelekeza gari alilokuwa akiliendesha.

Tukio hilo limetokea juzi maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam, baada ya dereva wa gari hilo kuingia kwenye barabara ya mwendokasi kisha kugongana na basi lililokuwa na abiria.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akiwataka madereva wote bila kujali ni taasisi gani kufuata sheria za nchi na kuacha kutumia mabavu.

Mambosasa alisema dereva huyo alifanya makosa kwa kuingia njia ya mabasi yaendayo kasi huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kinyume cha sheria.

"Huyu dereva ana makosa, kwanza alishindwa kuheshimu taa zinazoongoza magari na hairuhusiwi kupita katika njia hizo za mwendokasi. Baada ya kusababisha ajali hiyo, alilitelekeza gari na kukimbia", alisema Mambosasa.

"Namba za gari la jeshi (JWTZ) kwa sasa sizikumbuki kwa kuwa nimetoka ofisini nashughulika na masuala ya mafuriko".

Kuhusu madhara ya ajali hiyo, alisema watu wachache waliumia na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu na baadaye kuruhusiwa.

Mambosasa alisisitiza kuwa madereva wa majeshi wanatakiwa kufuata sheria za nchi bila kutumia mabavu ama cheo.

"Nilishasema hakuna ambaye yuko juu ya sheria. Ni vizuri hao madereva wa Jeshi wakafuata sheria za barabarani na hairuhusiwi kutanua kwenye barabara ambayo si njia yako", alisema Kamanda Mambosasa.

Aidha, alisema kuna magari ambayo ni dharura yaliyoruhusiwa kupita kwenye njia ambayo si yake kinyume cha hapo, mengine yote yanatakiwa kufuata sheria zilizopo.

Gazeti hili lilishuhudia gari ya Jeshi ikipita katika njia ambayo si yake katika eneo la Riverside Ubungo na kumgonga mwendesha bodaboda ambaye alikuwa kwenye njia yake.

Chanzo: Nipashe
 
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Messages
5,230
Likes
10,834
Points
280
Age
30
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined May 17, 2017
5,230 10,834 280
Hawa wanajidaiga wababe na wako juu ya sheria.Njia imewekwa rasmi ya mwendokasi wewe unaingiza gari lako la jeshi sijui la wokovu au.Huu sio utu kabisa maana amehatarisha maisha ya wananchi ambao kimsingi ni watu anaopaswa kuwalinda
 
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Messages
1,613
Likes
853
Points
280
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2017
1,613 853 280
HAWA WANAJIDAIGA WABABE NA WAKO JUU YA SHERIA.NJIA IMEWEKWA RASMI YA MWENDOKASI WEWE UNAINGIZA GARI LAKO LA JESHI SIJUI LA WOKOVU AU.HUU SIO UTU KABISA MAANA AMEHATARISHA MAISHA YA WANANCHI AMBAO KIMSINGI NI WATU ANAOPASWA KUWALINDA
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.
 
M

maiyanga1

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Messages
365
Likes
308
Points
80
Age
55
M

maiyanga1

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2017
365 308 80
Mara ngapi inatokea hata kwa majeshi mengine,? Ni kitu cha kawaida kwa mfano kumuona askari anaendesha gari bila kufunga mkanda au kuendesha pikipiki bila kuvaa helmet, lakini hawachukuliwi hatua yoyote.
 
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Messages
1,613
Likes
853
Points
280
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2017
1,613 853 280
Haya maslahi ya Taifa hata mtu akiwa anawahi mchepuko yanaruhusiwa kama kisingizio?
Kama ni hivyo hata ambulance pengine wanawahi michepuko.gari ilikua ya kazini means jamaa alikua kazini acha fikra potofu kwa jeshi lako
 
D

DON

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2008
Messages
841
Likes
454
Points
80
D

DON

JF-Expert Member
Joined May 6, 2008
841 454 80
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.
Hatuna crisis, ukiangalia mara kwa mara magari ya jeshi huwa hayafuati sheria za barabarani magari yao yanatakiwa yakae kambini tu uraiani yanafuata nini? Siku hizi hakuna movement order?
 
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Messages
1,613
Likes
853
Points
280
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2017
1,613 853 280
Ingekuwa kihalali angetelekeza Gari?
Umeambiwa aliacha gari ameondoka unajua aliwahi wapi ,na kama angechelewa nini kingetokea.unahisi wanajeshi wapowapo tu wanasubiri mishahara tu.unajuaje kama ndio mwenye dhamana ya ghala la silaha na alikua anawahi nini kisitokee ndo mana akapita njia ya mwendo kasi.mbona magari mengine hayapiti njia hyo .
 
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Messages
1,613
Likes
853
Points
280
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2017
1,613 853 280
Hatuna crisis, ukiangalia mara kwa mara magari ya jeshi huwa hayafuati sheria za barabarani magari yao yanatakiwa yakae kambini tu uraiani yanafuata nini? Siku hizi hakuna movement order?
Yakae kambini tu,halafu movement za kijeshi watumie daladala au vp mkuu
 
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Messages
7,520
Likes
7,748
Points
280
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2017
7,520 7,748 280
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.
Unadhani abiria wa mwendo kasi walikuwa sungura wale?Kila mtu anawah anakowahi kwa maslah yake na ya taifa.
Ni kwamba madereva wa majeshi iwe polisi au JWTZ huwa wana vunja sana sheria,sasa huko alikokuwa anawah amefika?Kam kwa maslah ya taifa mbona maekimbia?
 
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Messages
7,520
Likes
7,748
Points
280
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2017
7,520 7,748 280
Umeambiwa aliacha gari ameondoka unajua aliwahi wapi ,na kama angechelewa nini kingetokea.unahisi wanajeshi wapowapo tu wanasubiri mishahara tu.unajuaje kama ndio mwenye dhamana ya ghala la silaha na alikua anawahi nini kisitokee ndo mana akapita njia ya mwendo kasi.mbona magari mengine hayapiti njia hyo .
Mshahara haubebwi kwenye basi la jeshi.
Kumbe hujawah hata kuona mishahara yao wanavyoisafirisha
 
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,209
Likes
48,006
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,209 48,006 280
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.
Kama alikua anawai, kwanini katelekeza gari? Tusifiche upumbavu kwa kuwaona wa maana. Wanajeshi na mapolisi wanaongoza kwa kuvunja sheria za barabarani.
Kwenye mataa wanapita bila ya kujali kama wameruhusiwa au la.
 

Forum statistics

Threads 1,238,895
Members 476,226
Posts 29,336,009