Askari wa barabarani tendeni haki msilazimishe makosa kwa Wananchi

Wewe unaonekana huna gari au unaishi mkoani siyo Dar.askari wa barabarani wanalazimisha sana makosa sijapata kuona.mpka huwa nadhani labda lengo lao kuwa barabarani ni kukusanya hela
Leo wamenipiga mkono wadada 2 matrafic nikasimama bila wasi maana gari iko njema , na mkanda nimefunga... Mmoja akata leseni na kadi , nikampa, akataka fire extinguisher nikamuonyesha.... Akazunguka gari weee then akaniambia hii tairi moja ya nyuma imeanza kuisha wakati iko poa tuu , Nikamwambia tairi zote hazina tatizo....tukavutana wee mwishowe akaniacha baada ya kusimamisha gari zingine. Yaani wasumbufu kweli...
 
Uko sahihi kabisa mleta mada, serikali yenyewe haiko "perfect" kama wanavyotaka madereva tuwe , kwa kweli nawachukia sana japo kuna ndugu zangu wanafanya hiyo kazi. kwa kuwa hatuna muda wa kwenda mahakamani ndio kinawapa kiburi , naona imefika wakati wa kwenda mahakamani kusimamia haki , inakera sana , nimeichukia hadi serikali kwa sababu yao. hapa nilipo nadaiwa 60,000/= ndani ya siku mbili , na zote ni uonevu wa dhairi , (kosa la kwanza , taa moja ya mbele iliungua nikiwa nasafiri usiku , nikamuuliza unajua muda gani taa inaungua hana jibu anasema yeye anasimamia sheria , la pili ni pale external trafic light wanapovizia , taa ya orange imewaka nikiwa katikati ya njia panda , je ningesimama ?? bado wanaandika faini kwa kiburi , inauma sana . Mungu anawaona , hivi wao wako safi 100% !!!!!!!!!!???? ninawachukia sana.
Kilichokupata ndicho kilichonitoke ila acha tu nipite kimya maana nikieleza hapa tukio lililonitokea...!
 
Umeongea ukweli Hata sikukuu wanasimama barabarani kukamata magari.. Gari sasa imekua uadui mkubwa humo barabarani
 
Back
Top Bottom