Askari wa barabarani tendeni haki msilazimishe makosa kwa Wananchi

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
458
250
Salamu wandugu,

Kwanza ni wapongeze Askari wa barabarani kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana.

Hoja yangu ni juu ya operation mnazofanya barabarani zimekuwa na usumbufu na kero kubwa yaani, ukamataji magari hata kama huna kosa wanatafuta makosa kwa lazima

Napenda kuwashauri askari wa barabarani ni kweli mnafanya kazi nzuri ila tunawaomba mtende haki msilazimishe makosa sisi ni watanzania wenzeni hatuna mashamba ya hela tunayovuna ili kulipa hizo faini. Wengine wanaandika faini kimyamya unashangaa unakamatwa eti unadaiwa hata ulipofanya kosa hujui.

Jamani muwe na utu mnatutesa na kufanya tuwachukie kiukweli watu wanachukia sana hayo mnayofanya barabarani kama mtu hana kosa muache sio kulazimisha makosa na makosa mengine ni kumuonya mtu sio lazima upige faini mnaumiza watanzani bure na kujijengea chuki. Tambueni nyie ni sehemu ya jamii msijenge uadui na raia kwa kuwabambikia makosa

Imefikia hatua tunaogopa kuendesha gari siku za Jumamosi na Jumapili kwa sababu ya nyakua nyakua kila kona kiukweli mnapata hela kupitia hizo faini ila mnaacha majeraha mioyoni mwa watu.

Kwa hiyo nawashauri mtende haki si vinginevyo kama kosa la faini mwandikie lakini kama hamna kosa mwache dereva sio kulazimisha hata hivyo makosa mengine mnaweza shauri mtu cha kufanya sio kumuandikia faini
 
UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,665
2,000
Salamu wandugu,

kwanza ni wapongeze askari wa barabarani kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana.
Hoja yangu ni juu ya operation mnazofanya barabarani zimekuwa na usumbufu na kero kubwa yani ukamataji magari hata kama huna kosa wanatafuta makosa kwa lazima
Napenda kuwashauri askari wa barabarani ni kweli mnafanya kzi nzuri ila tunawaomba mtende haki msilazimishe makosa sisi ni watanzania wenzeni hatuna mashamba ya hela tunayovuna ili kulipa hizo faini.wengine wanaandika faini kimyamya unashangaa unakamatwa eti unadaiwa hata ulipofanya kosa hujui.Jamani muwe na utu mnatutesa na kufanya tuwachukie.ki ukweli watu wanachukia sana hayo mnayofanya barabarani kama mtu hana kosa muache sio kulazimisha makosa na makosa mengine ni kumuonya mtu sio lazima upige faini mnaumiza watanzani bure na kujijengea chuki.tambueni nyie ni sehemu ya jamii msijenge uadui na raia kwa kuwabambikia makosa.
Imefikia hatua tunaogopa kuendesha gari siku za jumamosi na jumapili kwa sababu ya nyakua nyakua kila kona ,ki ukweli mnapata hela kupitia hizo faini ila mnaacha majeraha mioyoni mwa watu.kwa hiyo nawashauri mtende haki si vinginevyo kama kosa la faini mwandikie lakini kama hamna kosa mwache dereva sio kulazimisha ,hata hivyo makosa mengine mnaweza shauri mtu cha kufanya sio kumuandikia faini.
Fuata sheria acha kulalamika!! Mimi huwa wananisimamisha lakini kwa kuwa na comply na sheria huniacha naendelea na shughuli zangu. Wewe lazima utakuwa na matatizo.
 
uberimae fidei

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,957
2,000
Alafu saivi usiku hawaeleweki sio kama zamani kuanzia sa moja hauwakuti,unaingia dar umezoea kunyoosha bila kuzingatia speed 50 wamejaa kuanzia mlandizi
 
mujungu

Senior Member
Nov 1, 2010
138
225
Uko sahihi kabisa mleta mada, serikali yenyewe haiko "perfect" kama wanavyotaka madereva tuwe , kwa kweli nawachukia sana japo kuna ndugu zangu wanafanya hiyo kazi. kwa kuwa hatuna muda wa kwenda mahakamani ndio kinawapa kiburi , naona imefika wakati wa kwenda mahakamani kusimamia haki , inakera sana , nimeichukia hadi serikali kwa sababu yao. hapa nilipo nadaiwa 60,000/= ndani ya siku mbili , na zote ni uonevu wa dhairi , (kosa la kwanza , taa moja ya mbele iliungua nikiwa nasafiri usiku , nikamuuliza unajua muda gani taa inaungua hana jibu anasema yeye anasimamia sheria , la pili ni pale external trafic light wanapovizia , taa ya orange imewaka nikiwa katikati ya njia panda , je ningesimama ?? bado wanaandika faini kwa kiburi , inauma sana . Mungu anawaona , hivi wao wako safi 100% !!!!!!!!!!???? ninawachukia sana.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,954
2,000
Mimi nakuunga mkono mtoa madam,Mimi nimepigwa faini ya uonevu kabisa .Nanitaendeleaa kulisema Hilo kwani kupita service road pale tangibovu Kama natokea na naishi maeneo ya shule napita wapi Kama naenda mwenge kwa mfano.Yaani yule Askari alitulima 30,000 sijaelewa mpaka Sasa yaani namtafuta Sirro mpaka nimpate kwa kweli
 
Examiner

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
587
500
Uko sahihi kabisa mleta mada, serikali yenyewe haiko "perfect" kama wanavyotaka madereva tuwe , kwa kweli nawachukia sana japo kuna ndugu zangu wanafanya hiyo kazi. kwa kuwa hatuna muda wa kwenda mahakamani ndio kinawapa kiburi , naona imefika wakati wa kwenda mahakamani kusimamia haki , inakera sana , nimeichukia hadi serikali kwa sababu yao. hapa nilipo nadaiwa 60,000/= ndani ya siku mbili , na zote ni uonevu wa dhairi , (kosa la kwanza , taa moja ya mbele iliungua nikiwa nasafiri usiku , nikamuuliza unajua muda gani taa inaungua hana jibu anasema yeye anasimamia sheria , la pili ni pale external trafic light wanapovizia , taa ya orange imewaka nikiwa katikati ya njia panda , je ningesimama ?? bado wanaandika faini kwa kiburi , inauma sana . Mungu anawaona , hivi wao wako safi 100% !!!!!!!!!!???? ninawachukia sana.
Dah,pole Mkuu inaonekana unawachkia Sana maana umeandika Kwa hisia Sana,hata Mimi siwapend kwakweli
 
Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,474
2,000
Mi hata nikikuta afande anataka lift siwezi mpandisha kwenye gari yangu. Make wamesha niandikia makosa kama matatu ya kulazimisha, hakika yanaumiza eiseh!
 
Rugaiyulula

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,479
2,000
Mi hata nikikuta afande anataka lift siwezi mpandisha kwenye gari yangu. Make wamesha niandikia makosa kama matatu ya kulazimisha, hakika yanaumiza eiseh!
Yangu siaminikabisa kama kuna anayeweza panda yaana hata kama ni mwanangu kaamua kuwa traffic. yaani wanaonea sana. Anaandika faini hata kabla hujasimama kukueleza kosa lako! Ohooh mara gari mbona ina michirizi mingi.
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
1,873
2,000
Fuata sheria acha kulalamika!! Mimi huwa wananisimamisha lakini kwa kuwa na comply na sheria huniacha naendelea na shughuli zangu. Wewe lazima utakuwa na matatizo.
Wewe unaonekana huna gari au unaishi mkoani siyo Dar.askari wa barabarani wanalazimisha sana makosa sijapata kuona.mpka huwa nadhani labda lengo lao kuwa barabarani ni kukusanya hela
 
Iruru

JF-Expert Member
Jan 27, 2014
787
1,000
Poleni wote mnaopatwa na hii kadhia. Polisi wetu hasa dar wanakera na kuumiza sana. Tangia wapewe hivi vimachine jamaa wao wanachojua ni kukupa risiti tu! Hapo buguruni kwenye mataa waliwahi kunipiga 60000, kosa la kwanza ni kupita red traffic na la pili kusimama kwenye zebra. Jamaa mpumbavu sana, yaani unaniadhibu kwa kupita red light na hapo hapo kusimama kwa zebra crossing!!???. Nilipmuuliza hapa uliponisimamisha kuna zebra crossing ama wapi niliposimama zaidi ya hapa...jamaa likaondoka likechekacheka. It pained me, na kamwe hili halitaondoka kwa akili yangu kama kitendo cha uonevu cha hali ya juu kufanyiwa mtu mzima na askari wetu tena mchana mweupe kabisaaaaa
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
62,774
2,000
Fuata sheria acha kulalamika!! Mimi huwa wananisimamisha lakini kwa kuwa na comply na sheria huniacha naendelea na shughuli zangu. Wewe lazima utakuwa na matatizo.
Sasa kwa mfano huyu anaongoza magari... tena kwa ishara kwamba uende kwa kasi... ghafla anasimamisha unajikuta huna namna unasimama kwenye zebra crossing... anakuja mwenzake anakulamba fine kwanini umesimama kwenye kivuko cha wavuka kwa miguu....

Hapo unasemaje?
 
jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
458
250
Fuata sheria acha kulalamika!! Mimi huwa wananisimamisha lakini kwa kuwa na comply na sheria huniacha naendelea na shughuli zangu. Wewe lazima utakuwa na matatizo.
Uko sahihi kabisa mleta mada, serikali yenyewe haiko "perfect" kama wanavyotaka madereva tuwe , kwa kweli nawachukia sana japo kuna ndugu zangu wanafanya hiyo kazi. kwa kuwa hatuna muda wa kwenda mahakamani ndio kinawapa kiburi , naona imefika wakati wa kwenda mahakamani kusimamia haki , inakera sana , nimeichukia hadi serikali kwa sababu yao. hapa nilipo nadaiwa 60,000/= ndani ya siku mbili , na zote ni uonevu wa dhairi , (kosa la kwanza , taa moja ya mbele iliungua nikiwa nasafiri usiku , nikamuuliza unajua muda gani taa inaungua hana jibu anasema yeye anasimamia sheria , la pili ni pale external trafic light wanapovizia , taa ya orange imewaka nikiwa katikati ya njia panda , je ningesimama ?? bado wanaandika faini kwa kiburi , inauma sana . Mungu anawaona , hivi wao wako safi 100% !!!!!!!!!!???? ninawachukia sana.

sawa mimi nina matatizo hongera kwa kufuata sheria ipo siku utakuja nielewa
 
Tena kwa uongozi huu tulionao wamezidi, imekuwa kero sasa.
acha ndugu yangu leo jumamosi ndo nyakua nyakua kila mahali tunaogopa hata kutembea na private car kila mahali ukaguzi mara lete leseni anaanza maswali mara kadi ooh taa inanyufa nakuandikia ukipanic wanakuja wengi kukukomesha faini imekuwa dili sijui kuna bonus wanapata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom