Hiyo ni siri iliyo wazi( open secret). Anayesema hajui haya iwe mtu binafsi au taasisi iwe ya umma au private anadanganya. Period
Serekali Ni ngumu kuwagusa hao jamaa maana Ni sehemu ya taasisi inayokusanya mapato awamu hii ya 5.
Kuna mdau alishauri
"Hawa Askari barabarani wanatakiwa nguo zao zisiwe na mifuko"
Walivyowajanja wataweka takrima kwenye kofia labda na kofia wakatazwe.
Rushwa ya polisi usalama barabarani huwa inachangiwa sana na sisi mwenyew.Kwanza nichukue pongezi kuubwa kwa Mheshimiwa Brigedia John Mbungo kuteuliwa kuwa mkuu wa Takukuru baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa muda mrefu. Lakini pia kwa kuonyesha kazi nzuri.
Pamoja na mafanikio hayo bado rushwa ni tatizo kuubwa ndani ya jeshi la Polisi hasa idara ya usalama barabarani, askari wanachukua rushwa pasi na woga. sitaki kuamini km mitego ya TAKUKURU imeshindwa kufanya kazi kuwakamata. mfano Pale kweye taa za Mwenge askari wanachukua pesa mbele za watu. Kwa kifupi highway zote wanachukua rushwa hadharani.
TUNAOMBA KUFAHAMU KAMA WAO NI HALALI KUFANYA HIVYO Kwa sababu ni rahisi sana kuwakamata. wanatia doa nchi yetu kwenye macho ya wageni.
Rushwa ya polisi usalama barabarani huwa inachangiwa sana na sisi mwenyew.
Mara nyingi sisi wenyewe tunapokamatwa ndio huanza kutaka kutoa kitu kidogo.
Mm nashauri kama ww gari yako ni mbovu au huna leseni au au hata kama umepatikana na makosa matano ww waambie wakuandikie faini ulipe kuliko kuomba uwape elfu kumi au 20 wakusamehe.
Mambo mengne tunayasababisha wenyewe halafu tunakuwa kimbembele kulalamika