Askari usalama barabarani (Traffic Police) ni halali kupokea rushwa?

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Kwanza nichukue pongezi kuubwa kwa Mheshimiwa Brigedia John Mbungo kuteuliwa kuwa mkuu wa Takukuru baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa muda mrefu. Lakini pia kwa kuonyesha kazi nzuri.

Pamoja na mafanikio hayo bado rushwa ni tatizo kuubwa ndani ya jeshi la Polisi hasa idara ya usalama barabarani, askari wanachukua rushwa pasi na woga. sitaki kuamini km mitego ya TAKUKURU imeshindwa kufanya kazi kuwakamata. mfano Pale kweye taa za Mwenge askari wanachukua pesa mbele za watu. Kwa kifupi highway zote wanachukua rushwa hadharani.

TUNAOMBA KUFAHAMU KAMA WAO NI HALALI KUFANYA HIVYO Kwa sababu ni rahisi sana kuwakamata. wanatia doa nchi yetu kwenye macho ya wageni.
 
Umesahau kuwa awamuhii badohaijawafikia wanaochukuwa pesa kwa ajili ya kununulia kiwi?.

Kwa sasa mziki upo kwa wapiga deal kwenye mikataba ya hovyo na wahujumu wa uchumi na pia wafanya kazi wa taasisi za kodi.

Subiri kipindi cha pili na hawa wachukuwaji wa pesa za kiwi watafikiwa tuu. JPM siyo wa mchezo kwenye wanaokula mlungula hata kidogo mkuu.
 
Rushwa ni adui wa haki-haki ipi hapa barabarani inayopotea??haki ya dereva,mmiliki wa chombo,abiria,serikali ama traffic mwenyewe??

Mtoa rushwa& mpokea rushwa wote ni waharifu-kwa case hii wengi huwa mnamwangalia traffic peke yake,ndipo uzito wa swala hili unapogeuka kuwa jungu zaidi ya crime.

Ili mshitakiwa apatikane na hatia,anatakiwa awe pasi na shaka alishikwa na ushahidi wa pesa yenyewe iliyoitwa rushwa,kwa vigezo gani sasa pesa inakuwa ya rushwa,haina alama wala nembo,sio hizi story za humu.

NOTE:Tanzania ni yetu wote tushirikiane kuijenga badala ya kuihujumu,traffic akikushika kwa kosa la barabarani,hata akuangalie kwa huruma kiasi gani,usimpe buku mbili,mpe 30 elfu akupe risiti.msilee ujinga jaman wananchi.
 
Hiyo ni siri iliyo wazi( open secret). Anayesema hajui haya iwe mtu binafsi au taasisi iwe ya umma au private anadanganya. Period
 
Kiufupi wakale wapi asiyekuwa mwizi humu anyooshe kidole kwanza wizi unatofautiana kuna wale wa kuku mpaka wale wanaotuibia mimi na wewe upoo
 
Hiyo ni siri iliyo wazi( open secret). Anayesema hajui haya iwe mtu binafsi au taasisi iwe ya umma au private anadanganya. Period

Kama PCCB wako seriuos na rushwa wakamate hawa traffic siyo waachwe wachukue pesa hata mbele ya wananchi. hii ni dharau kubwa sana.
 
Serekali Ni ngumu kuwagusa hao jamaa maana Ni sehemu ya taasisi inayokusanya mapato awamu hii ya 5.

Kuna mdau alishauri

"Hawa Askari barabarani wanatakiwa nguo zao zisiwe na mifuko"

Walivyowajanja wataweka takrima kwenye kofia labda na kofia wakatazwe.
 
Kulitenganisha Jeshi letu la Polisi dhidi ya suala zima la Rushwa, nadhani ni mtihani mgumu sana. Kama kuna Askari Polisi wasio pokea rushwa hapa nchini, basi wanahesabika.
 
NDIO!
ASUBUHI TRAFIKI WA KIBAMBA, MBEZI INN, MBEZI MWISHO, KIMARA, WANASIMAMISHA DALADALA NA VITIPA WANACHUKUA HELA MCHANA KWEUPEEEEEEEE
 
Serekali Ni ngumu kuwagusa hao jamaa maana Ni sehemu ya taasisi inayokusanya mapato awamu hii ya 5.

Kuna mdau alishauri

"Hawa Askari barabarani wanatakiwa nguo zao zisiwe na mifuko"

Walivyowajanja wataweka takrima kwenye kofia labda na kofia wakatazwe.

hahaaa zisiwe na mifuko.
 
Kwanza nichukue pongezi kuubwa kwa Mheshimiwa Brigedia John Mbungo kuteuliwa kuwa mkuu wa Takukuru baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa muda mrefu. Lakini pia kwa kuonyesha kazi nzuri.

Pamoja na mafanikio hayo bado rushwa ni tatizo kuubwa ndani ya jeshi la Polisi hasa idara ya usalama barabarani, askari wanachukua rushwa pasi na woga. sitaki kuamini km mitego ya TAKUKURU imeshindwa kufanya kazi kuwakamata. mfano Pale kweye taa za Mwenge askari wanachukua pesa mbele za watu. Kwa kifupi highway zote wanachukua rushwa hadharani.

TUNAOMBA KUFAHAMU KAMA WAO NI HALALI KUFANYA HIVYO Kwa sababu ni rahisi sana kuwakamata. wanatia doa nchi yetu kwenye macho ya wageni.
Rushwa ya polisi usalama barabarani huwa inachangiwa sana na sisi mwenyew.
Mara nyingi sisi wenyewe tunapokamatwa ndio huanza kutaka kutoa kitu kidogo.
Mm nashauri kama ww gari yako ni mbovu au huna leseni au au hata kama umepatikana na makosa matano ww waambie wakuandikie faini ulipe kuliko kuomba uwape elfu kumi au 20 wakusamehe.

Mambo mengne tunayasababisha wenyewe halafu tunakuwa kimbembele kulalamika
 
nakubaliana na wewe lkn pia seyo kila sehemu. wkt mwingine wanaonea raia wema. Traffic wa Kitanzania wanasubiri makosa. Angalia sehemu zote zenye utatat ndiyo utakuta wamejazana. Mfano hapo kwenye taa za mwenge Dar, hakuna taa ya njano hvyo kila taa inapoawaka lazima trafic wakamate watu si chini ya magari 3-5 kwani taa za njano zinwaka dereva akiwa tayari kati kati ya barabara. je dereve asimamisha katikti ya barabara ili atii taa nyekundu? nenda kwenye zebra mnazi mmoja au pale tangi bovu utawakuta wamjeaa. wananchi wanalazimishwa kutoa rushwa. mfano mwingine ukitoka ubungo hapo mwenge Dar ukielekea tegeta unatumia filter road, sheria inaelekeza kuangalia usalama km hakuna gari unaruhiswa kwenda kwa sababu hakuna taa inayoongoza magari yanayo elekea tegeta kutoka ubungo. lkn traffic wanasumbua watu
 
1622102946879.png
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom