Polisi: Ruksa kumrekodi Trafiki anayechukua Rushwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo ametoa ruksa kwa abiria kuwarekodi kwa simu askari wa usalama barabarani wanaochukua rushwa kwa madereva na kisha kumtumia ili awashughulikie.

Kamanda Jongo amesema hayo leo wakati akizungumuza na madereva, abiria na mawakala wa vyombo vya usafiri kituo kikuu cha mabasi Geita katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani.

Amesema imekuwa ni mazoea kwa maaskari wa usalama barabarani (trafiki) wanapokagua na kubaini gari lina mapungufu basi wanachukua pesa kwa madereva badala ya kuandika faini ama kuchukua hatua.

“Askari asipotekeleza wajibu wake, au askari akiwasimamisha, mkaona anachukua rushwa, rushwa ni adui wa haki, rushwa ni chanzo cha ongezeko la ajali, tusikubali.
 
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo ametoa ruksa kwa abiria kuwarekodi kwa simu askari wa usalama barabarani wanaochukua rushwa kwa madereva na kisha kumtumia ili awashughulikie.

Kamanda Jongo amesema hayo leo wakati akizungumuza na madereva, abiria na mawakala wa vyombo vya usafiri kituo kikuu cha mabasi Geita katika uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani.

Amesema imekuwa ni mazoea kwa maaskari wa usalama barabarani wanapokagua na kubaini gari lina Upungufu basi wanachukua fedha kwa madereva badala ya kuandika faini ama kuchukua hatua.

“Askari asipotekeleza wajibu wake, au askari akiwasimamisha, mkaona anachukua rushwa, rushwa ni adui wa haki, rushwa ni chanzo cha ongezeko la ajali, tusikubali.

Dereva ameendesha mwendokasi, askari ameliona hilo, na nyie mmeliona, lakini askari anachukua rushwa, mimi Kamanda wa Polisi na askari wa Mkoa wa Geita hatuvumili askari anayechukua rushwa.

“Kama una zile simu za kisasa (simu janja) tutumie picha (video), na huyo kibarua chake kitakuwa ndio kimeishia hapo, lakini chukueni namba ya simu askari ambaye ataenda kinyume na taratibu nipeni taarifa,” amesema.

Ameagiza kila basi la abiria kubandika namba za simu za makamanda wa mikoa yote wanapopita, ili abiria wanapoona sintofahamu ama ukiukwaji wa sheria ya barabarani watoe taarifa kwa haraka.

Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom