Askari Polisi watatu wafariki dunia katika msafara wa CCM Singida

Askari Polisi watatu wafariki dunia katika msafara wa CCM Singida

kazi ya mungu haina makosa japo kila litokealo huwa na sababu na msababishi poleni wafiwa
Kweli Mungu ndo aliwaamuru waende speed ya 120 au yeye ndo aliandaa hiyo sherehe? Mungu hawezi kumlazimisha mtu afe kwa speed au tyle kupasuka tusewe tunamsingizia. RIP maafande.
 
Natamani gari za polis na misafara ya viongozi iendeshwe speed chini ya 80, ili iwe mfano kwa madereva wengine kuiga.
 
vifo vya uzembe utokanao na kutozingatia sheria za barabarani,hasa mwendo kasi.
 
Ni muhimu kuwahurumia kma binadamu, lakini nao hutenda kama si binadamu. hao wanaowapiga na kuwaua wana ndugu pia wanaoumia kwa uchungu wa wapendwa wao. Ifike mahali tuseme tu ukweli polisi mnachukiwa sana na wananchi kwa ukatili mnaowatendea. Kibinadamu ndio maana mnapopata majanga wananchi wanafurahia sana. Hebu badilikeni acheni kufanya kazi kwa mashinikizo ya CCM.
 
Ni huko Singida wakielekea Manyoni.

Ni baada ya tairi ya gari kupasuka na kupoteza muelekeo.


73620de0bc2a775b012cf795a58639c1.jpg


Nimeiangalia hiyo tairi ya mbelekwa ku - zoom, nikakuta kuwa ni kipara cha ajabu!!! Sasa hawa askari hawawezi kuwa wanakamata wananchi kwa tairi zilizokwisha wakati wao wanaendesha gari zao kwa kasi huku tairi zikiwa vipara namna hii!

Hii ajali ni uzembe wa hali ya juu ambao unatakiwa uchunguzi ufanyike na watu kuchukuliwa hatua kali.

Hatuwezi kuwa tunaachia mambo ya kizembe namna hii kuwa yanatugharimu kiasi hiki. Haya ni majipu mengine yanayotakiwa kutumbuliwa.

Iweje gari ya polisi ambayo mara zote iko katika mishe mishe za kwenda kasi kila siku kuwa na tairi kipara namna hii?
 
Mwendokasi unapasua tairi?
Sana tu Mkuu Kwameh. Ikiwa una tairi zilizochoka au za zamani ukaenda kwa mwendo kasi tairi itapasuka. Na pia tairi zina code za maximum speed. Ukienda kasi ya 120km/hr kwa tairi yenye code ya maximum speed 100km/hr itapasuka. Hii Zaidi ni kutokana na forces (centrifugal) ambazo zinaipata tairi inapozunguka, ambazo forces hizo huongezeka kadiri spiidi inavyoongezeka.

Hivyo kabla hujakimbiza sana gari hakikisha tairi zako ni nzuri, mpya, na pia zimetengenezwa kukimbia spidi unayofika, lazivyo utapata burst.

Wakati fulani wenye mabasi ya abiria walinunua sana tairi za spidi ya 100km/hr kwa sababu tairi hizi ni bei rahisi kuliko tairi ya spidi ya juu ya 100km/hr. Sasa kwa kuwa mabasi mengi yanaenda zaidi ya 100km/hr tairi zikawa zinapasuka sana, wakadhani tairi za Michelin zilikuwa na tatizo kumbe ilikuwa agent wa Michelin hapa Tanzania alikuwa anawauzia wenye mabasi tairi zisizofaa kwa spidi ya basi kwa bei poa. Tairi hizi zilikuwa za malori ambayo kwa spidi ya 100km/hr zio tatizo sana. Tatizo ni kwamba huwezi kuona kwa macho tofauti kati ya tairi ya spidi ya juu na chini. Lazima ujue kusoma speed codes kwenye tairi.

Kuna post fulani niliweka yenye kichwa :Tahadhari kwa wale wenye gari binafis, chunga sana waeeze na wengine" niligusia haya mambo.

Katika hii ajali ya gari ya polisi ni wazi kwamba tairi ya mbele iliyopasuka ilikuwa imechakaa na lazima ingepasuka kwa mwendo waliokuwa nao.

Ni ajabu kwamba Polisi wetu wako tayari kutumia mamilioni ya fedha kufukuzana na mambo ya kisiasa yasiyo na msingi kuliko kuhakikisha gazi zao za kazi zina tairi sahihi na mpya.
 
Angalia tairi ambazo hii gari ya Polisi ilikuwa nazo. Nime-kata picha sehemu ya tairi na kuikuza. Kwenda kasi ya 120km/hr na tairi kama hizi, hasa ikiwa gari ina watu au mzigo, ni kukiita kifo. Lazima itapasuka.
 

Attachments

Poleni wafiwa,Raha ya milele awape Bwana na Mwanga wa Milele awaangazie Wapumzike kwa Amani,Amina
 
Hawa si ndio waliingia bungeni kupiga wabunge wa UKAWA? Malipo ni hapahapa duniani!
 
......

......unapokuwa kwenye mwendo kasi then burst ni hatari sana under 80 unaweza kusevu !!!
Hivi vitu ni Mungu tu nadhani siku yako inakua tu haijafika ,natoka Segera naitafuta Wami kulikua na mabasi mawili yame fuatana Ngorika la mbele yake Dar express ,nimeanza ku overtake Ngorika nikaunga na Dar express ile nakaribia kuimaliza Dar express Tairi la nyuma likalia ,bahati nzuri Dereva wa Dar express alikua muungwana akaaanza kupunguza speed na mbele yangu hakukua na gari ndio ikawa salama yangu ila nakumbuka nlikua Kwenye 160-170 Kph
 
Hivi vitu ni Mungu tu nadhani siku yako inakua tu haijafika ,natoka Segera naitafuta Wami kulikua na mabasi mawili yame fuatana Ngorika la mbele yake Dar express ,nimeanza ku overtake Ngorika nikaunga na Dar express ile nakaribia kuimaliza Dar express Tairi la nyuma likalia ,bahati nzuri Dereva wa Dar express alikua muungwana akaaanza kupunguza speed na mbele yangu hakukua na gari ndio ikawa salama yangu ila nakumbuka nlikua Kwenye 160-170 Kph


Naam, kama nilivosema hapo ju, uwezekano mkubwa ni kwamba tairi zako hazikuwa za kwenda spidi ya 160-170km/hr, au zilikuwa zina Zaidi ya miaka mine tangu ununue. Usije fanya kosa kwenda spidi Zaidi ya kiwango cha tairi zako - burst ya tairi lazima itakuja tu.
 
Naam, kama nilivosema hapo ju, uwezekano mkubwa ni kwamba tairi zako hazikuwa za kwenda spidi ya 160-170km/hr, au zilikuwa zina Zaidi ya miaka mine tangu ununue. Usije fanya kosa kwenda spidi Zaidi ya kiwango cha tairi zako - burst ya tairi lazima itakuja tu.
Mkuu top speed ya hiyo gari ilikua 260 ,hivyo tairi zilizofungwa zilikua zinaruhusu kabisa gari kutembea 160 na zaidi bila tatizo ,labda hilo la zaidi ya miaka minne japo sina kumbukumbu sahihi ,baada ya kutoa lile tairi maana Rim yote ilikunjika nikakuta bolt ndani ambayo ndio ilisababisha tairi kupasuka nilipoikanyaga nikiwa kwenye speed
 
Back
Top Bottom