Askari Polisi watatu wafariki dunia katika msafara wa CCM Singida

Askari Polisi watatu wafariki dunia katika msafara wa CCM Singida

R.I.P, Mungu awaweke panapolingana na matendo yao ya upolisi dhidi ya mwananchi wanyonge wa Tanzania.

Next time waelewe yale magari 700 ya Kikwete yana spidi ya ajabu.

Usikute waliambiwa mbele kuna wafuasi wa Ukawa wamejipanga kuzomea msafara.
 
lakini kusema ukweli viongozi wakuu pamoja na magufuli hizi safari za magari zitasababisha ajali apande ndege tu
 
Ukicheki hilo tairi I bet you utakuta ni zile zenye tube ndani. Tairi yenye tube ikitoboka vibaya linapasuka kama puto likichomwa pini! Ndo maana huwezi kusikia nchi za mbele gari limepinduka kwa sababu tairi limepasuka. Na inawezekana ni kamba vile vile, check blood alcohol levels za hao undisciplined njugas si ajabu kukuta they were under the influence of alcohol and contraband.
 
Du! hii ajari mbaya kweli. nimeona gari nikiwa ndani ya basi! Mungu azilaze Roho za marehemu mahali pema peponi

kama wewe uliye ndani ya basi unasema umeiona ikiwa ni mbaya vipi kwa hao wanakijiji wa hapo mkiwa ambao waliiona tokea inaanza, kupinduka na kuua wao wasemeje? kawadanganye watu wengine huko. katika basi unaweza ukaona nini wakati basi lenu lenyewe mlilolipanda linataka kuwahi huko muendako? sema tu au lugha sahihi ulitakiwa useme kuwa umeliona tu gari hilo juu juu. acheni shobo!
 
Sio utani,maana mwendo wanao mpitisha nao kiongozi anaye itwa wa ngazi ya juu ni wa hatari zaidi ya hicho wanacho kiogopa wakipita kwa mwendo wa wastani na mara zote wana usalama ndio wahanga,Mungu apishie, mbali yaliyo tokea kwa Marehemu Sokoine yasije yakajirudia,Askari ndio wanao tukumbusha raia kuwa mwendo kasi unaua ila wao na hasa kwenye misafara huo msemo hauwahusu,Mungu azilaze pema roho za Marehemu na kuwapa wafiwa nyoyo za uvumilivu.


.......Mwendo kasi ni kwa wote ajali haibagui
 
Kua katika msafara wa viongozi lazima magari yakimbizwe?
 
Poleni familia za hao maaskari, Mungu awape nguvu kipindi hiki kigumu
 
Mala awapumzishe kwa amani na awape subra ndugu wa marehemu
 
R.I.P ndugu zangu makamanda ...mmepoteza maisha mkiwa katika kutelekeza majukumu yenu ya kazi..police ni watu muhimu sana katika maisha yetu anayesema police si watu muhimu huenda hajawahi kupata msaada wa police...Kwa sisi ambao polisi walishawah kuokoa maisha yetu..ndugu zetu kamwe hatuwezi kucomment upuuzi kama huu..

Je kwn humu hakuna MTU mwenye ndugu,,Rafki hata jirani police

Lakini hata kama wapepoteza maisha imekuwa kwako nawe ni furaha Tambua hata wewe UTAKUFA..
NAIPENDA KAZI YANGU YA POLICE
 
Always and always wherever you have a tyre bust never ever on earth engage the brakes
Uko sahihi kabisa na pengine katika hili break hazikutumika, ila ni rahisi kucontrol gari uki pata burst na ukaji save ukiwa kwenye mwendo wa wastani kuliko ukiwa kwenye mwendo mkali iki tegemea pia na aina ya burst maana ikiwa kubwa uwezekano wa kupaa upo.
 
Ccm imejenga chuki na raia
Vyombo vya usalama imeshindwa kuvusimamia
Lawama hizi hawawezi kuzikwepa
Imefika kipindi raia tunawachukia polisi
Wakifaariki sisi tunafurahi
 
Back
Top Bottom