Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 132
wakuu hii imekaaje? kwanini serikali isjipange vizuri? Bado tunaupungufu wa askari na upungufu wa waalimu sasa asikari ndio wamekuwa waalimu. Du hii sijui wazee nyie mnaiona je.
Askari Polisi wajitolea kufundisha sekondari Serengeti
Na Anthony Mayunga, Serengeti
ASKARI polisi wenye taaluma ya ualimu wamejitolea kufundisha shule ya Sekondari ya Mugumu ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na uhaba wa walimu wilayani Serengeti.
Akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa mradi wa vyumba vitatu vya madarasa vilivyoibuliwa na kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Mkuu wa shule hiyo, Amon Majura, alisema kuwa askari hao wawili wameziba upungufu wa walimu ulioko katika shule hiyo.
Alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi 850 kwa kidato cha kwanza hadi cha nne lakini ina walimu watano tu wa kuajiriwa wa kujitolea wakiwa saba, miongoni mwao wakiwemo askari polisi ambao pia wana taaluma ya ualimu.
Alisema kwamba uwepo wao umekuwa ni msaada mkubwa kwa masomo ya Jiografia, Historia na Hisabati kwa kidato na cha nne ambayo pia hayakuwa na walimu.
Majura alikiri shule hiyo ina wanafunzi wengi kwa mwaka huu ambapo wamepelekwa 320 kwa mikondo minane lakini wana upungufu mkubwa wa walimu na kuomba juhudi za makusudi zifanywe na serikali kurekebisha hali hiyo.
Hata hivyo alisema kwamba walimu waliopo wamejitahidi kwa kiwango kikubwa ambapo mwaka jana wanafunzi wa Kidato cha Pili 178,kati ya 179 waliofanya mtihani walifaulu, huku mmoja pekee akiwa ameshindwa mtihani wa kuingia kidato cha tatu.
Kwa upande wa madarasa alikiri kuwepo upungufu wa vyumba vya madarasa ya kusomea ambapo kwa sasa vipo vyumba 13 kwamba kutokana na ikama ya watoto vinatakiwa vyumba 21 ambapo kila chumba kitakuwa na watoto 40.
Akizindua mradi huo Diwani wa Kata ya Mugumu mjini, Ryoba Charles alisema utekelezaji wake unatakiwa kufanyika kwa haraka ili kuepuka kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali ambao unaweza kuathiri utekelezaji wa mradi huo