Askari polisi na rushwa ili upewe loss report

Siku nyingine jaribu kufuata protocol ukiona unazungushwa waone viongozi wao unachonisikitisha bado hujatimiza wajibu wako
 
Hivi kweli nimepoteza kitu na bado nitoe rushwa kwa kupewa kibali tu?? Hyo elf tano ww askari una mshahara wa above 4k na posho 3k humuonei huruma maskini ambaye anafnya vibarua apate hela ya kula na hana permanent salary??
Hao hua hawana huruma wala aibu,hataa 200 wanachukua hawaachi
 
Mtoa UZI kuweka mambo sawa na kuwasaidia kazi hao unaoona watasaidia kutatua kero hizo ni vyema ungeweka wazi ni wapi? Ukakasi huo umekupata.
Kuliko kusema kwa ujumla kwa mtatua kero jibu ni jepesi kwa issue kubwa yaani SAWA TUMEKUSIKIA TUTALIFUATILIA.
Mkuu hili swala mbona linajulikana karibu vituo vyote au wewe haupo Tanzania
 
Mjomba tusihukumu kwa kufikirika tutakuwa hatutendi haki.
Umetendewa vibaya kituo Fulani cha polisi kitaje ikiwezekana hata muda uliofika pale ili iwasaidie wa kubwa wao kurekebisha tatizo au we mwenyewe kuona hukusaidiwa vyovyote MF mm sijawahi kwenda polisi kutaka polisi loss report nikienda nikapata kwa urahisi kumbe ni kituo hicho pekee kinachotoa kwa rahisi
 
Katika vituo vyote vya polisi kuna namba ya mkuu wa kituo, mkuu wa polisi wilaya, mkuu wa polisi mkoa,na mkuu wa polisi taifa, umeshimdwa kupiga simu na kuja na thuhuma za kuchafuana...haya kwa kukusaidia ni pm ni wapi lini na kilitokea nini.

Haku -pm we kama Nani? ??jitambulishe kwanza
 
Mjomba tusihukumu kwa kufikirika tutakuwa hatutendi haki.
Umetendewa vibaya kituo Fulani cha polisi kitaje ikiwezekana hata muda uliofika pale ili iwasaidie wa kubwa wao kurekebisha tatizo au we mwenyewe kuona hukusaidiwa vyovyote MF mm sijawahi kwenda polisi kutaka polisi loss report nikienda nikapata kwa urahisi kumbe ni kituo hicho pekee kinachotoa kwa rahisi
Mkuu sina chuki na jeshi la polisi' ila ni taasisi ambayo imeoza kwa rushwa, mimi sizungumzii loss report tu polisi wetu wana msaada umevamiwa na ujambazi lakini issue ndogo kama dhamana lazima utoe rushwa hasa kwa sisi wananchi wa chini
 
Napinga kwa upande wa Arusha mjini unalipia mia 5 unapata Report yako na ndani ya Dakika kama 20 unapata unasepa hakuna cha Rushwa. ila ni kwa Arusha
 
Mkuu sina chuki na jeshi la polisi' ila ni taasisi ambayo imeoza kwa rushwa, mimi sizungumzii loss report tu polisi wetu wana msaada umevamiwa na ujambazi lakini issue ndogo kama dhamana lazima utoe rushwa hasa kwa sisi wananchi wa chini
Mjomba umeona ulivyofunguka zaidi kwahiyo unazungumzia matatizo yaliyoko ktk vituo vya polisi uliyoyashuhudia.
Ambayo majibu yake ni mfumo mzima wa utoaji Huduma ktk taasisi zote za umma urekebishwe ili Huduma ya bure iwe bure ya kulipia ilipwe ili mtaka Huduma aridhishwe binafsi napambana na watu wa ardhi Mkuranga mwaka wa 3 nasubiria kupimiwa eneo langu
 
Mtoa uzi,ni vizur utaje jina la huyo askari na kituo chake cha kazi ili kurahisisha mambo. Mtu wa hvo ni kumpa tu ile pesa ya moto ya Takukuru
 
Inakuwaje jamani mtu mnamzungusha kumpa loss report mnataka mpewe rushwa ya elf 5 wakati gharama ni sh 500? Hamuombi ila mnamzungusha hata masaa 4 mpka ajiongeze atoe kidogo na akitoa tu dkk 5 haziishi anapewa na asipotoa atachoma sana mahindi.....Mwigulu tazama hili

Inakuwaje mtu anatuhumiwa na akibainika hana kosa haachiwi mpaka atoe kidogo?? Au huwa kuna suala gani hapa mimi huwa sielewi.....Mwigulu tusaidie

Inakuwaje unampeleka mtu polisi anashikiliwa lakini mnaanza kushindanishwa kutoa pesa akitoa pesa nyingi kesho utaona anadunda mtaani na ukiuliza longolongo zinakuwa nyingi??....Mwigulu tunaonewa

Askari wachache wanaharibu taswira ya jeshi zima la polisi......Viongozi wa juu wa jeshi hili msikubali.siku Magu akitupa jicho huko itakuwa heri yale ya Muhongo
Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake
 
I fact hawa ppcb wakitaka kuwadaka wala rushwa wawafuate polisi!!!traffic ndo usiseme!
 
Inakuwaje jamani mtu mnamzungusha kumpa loss report mnataka mpewe rushwa ya elf 5 wakati gharama ni sh 500? Hamuombi ila mnamzungusha hata masaa 4 mpka ajiongeze atoe kidogo na akitoa tu dkk 5 haziishi anapewa na asipotoa atachoma sana mahindi.....Mwigulu tazama hili

Inakuwaje mtu anatuhumiwa na akibainika hana kosa haachiwi mpaka atoe kidogo?? Au huwa kuna suala gani hapa mimi huwa sielewi.....Mwigulu tusaidie

Inakuwaje unampeleka mtu polisi anashikiliwa lakini mnaanza kushindanishwa kutoa pesa akitoa pesa nyingi kesho utaona anadunda mtaani na ukiuliza longolongo zinakuwa nyingi??....Mwigulu tunaonewa

Askari wachache wanaharibu taswira ya jeshi zima la polisi......Viongozi wa juu wa jeshi hili msikubali.siku Magu akitupa jicho huko itakuwa heri yale ya Muhongo
Tuwe wakweli katika tunacho andika kama hao Polisi wamekuomba rushwa si ungewaa mbia Takukuru
 
Back
Top Bottom