Uongozi wa ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya unatia mashaka; Matukio makubwa yaliyotokea Mbeya yanaashilia askari hawasimamiwi vema

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Leo naomba tuimulike mbeya.

Mkoa wa Chalamila na watu wake.

Inakuwaje matukio makubwa yenye misingi ya haki yanatukia mbeya?

Mtakumbuka
Kuna skendo ya muwekezaji wa mifugo hivi majuzi kajinyonga kutokana na mifugo yake zaidi 50 kukamatwa!

Ukitafakari kwa haraka haraka unaweza ona ni tukio la mauaji la kawaida!
lakini kwa wabobezi hili tukio lina misingi ya watu kutowajibika katika nafasi zao kutenda haki,
Kuna uwezekano wa misingi ya rushwa iliyoota mizizi kwa baadhi ya watendaji wa chini!

Haiwezekani mtu aamue kujinyonga kama kuna watu wamewajibika kutenda haki kwa wakati!

Tukio jingine ni lile la dreva wa roli kupokea kipigo kutoka kwa askari wa usalama barabarani!

Pamoja na report ya polisi kuonyesha marehemu alikufa kwa ugonjwa wa kubanwa mbavu, lakini tujiulize!
Mtuhumiwa wa shambulio hilo ni nani? Na aliyetoa repoti ya shambulio ni nani?
Hivi inawezekanaje mtuhumiwa ndiye atoe taarifa za kitabibu?
Kwa msingi wa kesi hii nayo naiweka kwenye kundi la kutowajibika ipasavyo!
Yamkini askari wadogo wameshindwa kusimamiwa vyema kiasi cha matunda haya makubwa mwaka 2021, tukumbuke pia ya 2019/20 yalitukia mbeya!

Haya makubwa yaliyoonekana yatuamshe kuona mengine yaliyofichika mbeya!

Kazi ya polisi ina misingi ya weledi na utii, Ukiona polisi na mgambo wadogo wanaumiza watu ujue kuna mawili, Either hawasimamiwi vyema au wametumwa kufanya hivyo!

Hivyo basi, naomba mamlaka husika, Takukuru, na mamlaka za uteuzi muimulike mbeya kuokoa wanainchi wanyonge!

Kuna haja ya kuwaangalia upya wasimamizi wa ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya wanavyofanya kazi!
 
Rafiki usihukumu kabla ya kufanya uchunguzi.
Neno "inasemakana /inaashiria " sio justification ya kuhoji /kuhusisha matukio na vile unavyoona.
Toa hoja acha wananzengo wajadili ama kwa kuunganisha dots au kwa taarifa utakazo endelea kuzitoa/qoutes.
 
Ambacho hamjaelewa ni kwamba sasa hivi mamlaka inafanya kitu ili kutuma ujumbe fulani mpana sana ya kuogopeshana!kwamba ukizingua tunakuua na hamna mtu atafanya kitu.
 
Rafiki usihukumu kabla ya kufanya uchunguzi.
Neno "inasemakana /inaashiria " sio justification ya kuhoji /kuhusisha matukio na vile unavyoona.
Toa hoja acha wananzengo wajadili ama kwa kuunganisha dots au kwa taarifa utakazo endelea kuzitoa/qoutes.
Ndiyo maana ya kumulika hao watendaji wanahudumiaje wanaichi, kama hayo yameonekana wazi basi kuna mengine
 
ambacho hamjaelewa ni kwamba sasa hivi mamlaka inafanya kitu ili kutuma ujumbe flan mpana sana ya kuogopeshana!kwamba ukizingua tunakuua na hamna mtu atafanya kitu.
Sizani, hakuna mamlaka za hivyo! Ukiona hivyo tambua kuna uzembe mahali!
 
Muangalie chalamila alivo, mara achape wanafunz sasa kama mkuu wa mkoa yuko vile unategemea hawa polis wafananeje? Hata hivo ni janga la taifa zima kiufupi nikama sheria hazifatwi kwasasa. Hasa kwa wenye mamlaka
 
Yaan huyu mkuu wa mkoa mbeya kaiharibu mbeya kabisa, kila kitu anakiweka kisiasa zaidi, anaropoka tuu hata vitu ambavyo sio vya kuongelea Hilo eneo, kiufupi hafai kuwa kiongozi kusifia tuu
 
Yaan huyu mkuu wa mkoa mbeya kaiharibu mbeya kabisa, kila kitu anakiweka kisiasa zaidi, anaropoka tuu hata vitu ambavyo sio vya kuongelea Hilo eneo, kiufupi hafai kuwa kiongozi kusifia tuu
Unaweza weka mfano mkuu
 
CCM inaua watu hovyo kupitia jeshi lake la Polisi halafu wanakuja na majibu mepesi eti ameumwa mapafu.
Kama Polisi ndio wamefundishwa kuwashusha wagonjwa namna ile na Mkuu wa Mkoa haoni tatizo, Basi CCM ni CHANZO CHA MATATIZO, CHAMA CHA MAZEZETA
 
Sizani, hakuna mamlaka za hivyo! Ukiona hivyo tambua kuna uzembe mahali!
Hebu jionee haya. Kama sio uonezi ni Nini?
IMG_20210130_123255.jpg
 
Msimamizi wa haki wa Mbeya ni yule RC aliyewachapa viboko vya kikatili watoto wadogo na kuwafukuza shule
Hana busara wala hekima.
 
Msimamizi wa haki wa Mbeya ni yule RC aliyewachapa viboko vya kikatili watoto wadogo na kuwafukuza shule
Hana busara wala hekima.
Nasikia eti Kaunda tume kuchunguza mauaji ya dereva sijui yamefikia wapi hayo majibu
 
Ni mwendo wa kujitapa kama wanafanya kazi vizuri,kumbe wanaharibu taswira ya nchi,,
 
Back
Top Bottom