Askari Polisi Afa Maji Akimkimbiza Mtuhumiwa

Mijitu inalaumu sijui askari kutumia nguvu badala ya akili
Badala ya kumuombea apumzuke shujaa wetu mnazungunza ujinga tu. Huyo afande alikua kwenye majukumu ya kulinda raia na amekubali kuhatarisha maisha yake kwa ajili yetu. Mkumbuke ziwa lina mamba lakini askari kaingia kumfuata mtuhumiwa.
Na sababu ni kunaswa na nyavu hata ujue kuogelea vipi ukinaswa na nyavyu chini ya maji hutoki.
Naomba jeshi la poliso limtafute huyo mtuhumiwa kwa nguvu na akili zote na akipatikana apigwe risasi tu sio wa kumkamata mzima mzimaL]
 
Habari mbaya na kuhuzunisha

Gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Askari Polisi nchini Tanzania afande Isaya Kawogo amefariki.dunia akiwa kwenye harakati za kumkimbiza ili kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu

Tukio hilo limetokea Mwisenge Musoma wakati Askari huyo akijaribu kumkamata mtuhumiwa huyo wa Ujambazi aliyejitosa ziwani na polisi huyo aliamua kumfuata na kwa bahati mbaya alinasa kwenye nyavu na kuzama majini kwenye Ziwa Victoria

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara RPC Longinus Tubushibwamu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Taarifa zaidi itatolewa na Jeshi la Polisi

=======

Musoma. Askari polisi, Isaya Kawogo amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Mei 28, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akibainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mwisenge manispaa ya Musoma.

Amesema askari huyo pamoja na wenzake wakiwa doria walikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kumkimbiza.

“Yule mtuhumiwa alijitosa ziwani na askari aliamua kumfuata huko huko ziwani lakini akiwa katika harakati za kumkamata alinasa kwenye nyavu na kuzama. Mtuhumiwa alifanikiwa kuimbia,” amesema kamanda huyo.

Chanzo: Mwananchi
Apumzike salama, ameumaliza mwendo akiwa katika Majukumu yake akika anastahili pongezi japo atunae tena
 
Back
Top Bottom