Askari Polisi Afa Maji Akimkimbiza Mtuhumiwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,156
4,510
Gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Askari Polisi nchini Tanzania afande Isaya Kawogo amefariki.dunia akiwa kwenye harakati za kumkimbiza ili kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu

Tukio hilo limetokea Mwisenge Musoma wakati Askari huyo akijaribu kumkamata mtuhumiwa huyo wa Ujambazi aliyejitosa ziwani na polisi huyo aliamua kumfuata na kwa bahati mbaya alinasa kwenye nyavu na kuzama majini kwenye Ziwa Victoria

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara RPC Longinus Tubushibwamu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Taarifa zaidi itatolewa na Jeshi la Polisi

=======

Musoma. Askari polisi, Isaya Kawogo amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Mei 28, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akibainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mwisenge manispaa ya Musoma.

Amesema askari huyo pamoja na wenzake wakiwa doria walikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kumkimbiza.

“Yule mtuhumiwa alijitosa ziwani na askari aliamua kumfuata huko huko ziwani lakini akiwa katika harakati za kumkamata alinasa kwenye nyavu na kuzama. Mtuhumiwa alifanikiwa kuimbia,” amesema kamanda huyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Habari mbaya na kuhuzunisha

Gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Askari Polisi nchini Tanzania afande Isaya Kawogo amefariki.dunia akiwa kwenye harakati za kumkimbiza ili kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu

Tukio hilo limetokea Mwisenge Musoma wakati Askari huyo akijaribu kumkamata mtuhumiwa huyo na kwa bahati mbaya alizama majini kwenye Ziwa Victoria

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Taarifa zaidi itatolewa na Jeshi la Polisi

MCL
Chadema hawakuhusika kumzamisha kwenye maji huyo afande?
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom