Asiyekujua hakuibii mke/mme

Asiyekujua hakuibii mke/mme

Hahaha umenifurahisha.
Ni kweli aisee, ukiona mtu anaiba nyumbani ujue anakaribia kugradyuate

Wanaokamatwa ni hao rafiki wa karibu lakini kuna msururu mkubwa nyuma ya pazia. Hata mateja huanza kuiba mbali mwisho huiba nyumbani kwao.
 
Hivi hii kitu ina kanuni kweli? Umeufikiria uwezekano wa mwanamke kuflirt na mtu asiemjua njiani,kwenye basi,sokoni, safarini au mazingira mengine ambayo yanamkutanisha na watu wasiokujua wala kumjua na kuishia kuwa wapenzi?
 
Hata ni afadhari nikaibiwa na mtu nisiyemfaham wala yeye hanifahamu, huwa inauma sana pale mbaya wako unamjua na yeye anakujua. Sikaribishi urafiki kwa mke wangu.
 
Lakini pia itategemea huyo mwanamke ulimtoa akiwa kwenye mazingira gani na wewe ukamuweka kwenye mazingira gani baada ya kumuoa, mazingira nayo ni mchawi tosha ndio maana nashauri kijana anapooa ni vizuri akabadillisha mazingira na kutoyapa nafasi maisha yako ya u-single ikiwemo ukaribu wa marafiki kwenye familia yako(nyumbani). Wale wanaenda kunywa bia, soda pub, club nk. wananitengenezea mazjngira ambayo baadae yatazaa ushawishi kutoka maeneo hayo hayo ambayo ni rahisi kuelezea ni aina gani ya watu wanaokuwepo maeneo hayo na tabia zao.
 
Hata ni afadhari nikaibiwa na mtu nisiyemfaham wala yeye hanifahamu, huwa inauma sana pale mbaya wako unamjua na yeye anakujua. Sikaribishi urafiki kwa mke wangu.
Huyo asiyekufahamu hakuibii na akikuibia atakuwa hakufahamu au mkeo alimdanganya bado hajaolewa.
 
Kwa asiekujua kuelezea mtu/watu changamoto za mahusiano yenu let say ugomvi, ukata wa hela kwa mtu ni fursa ya kuiandaa chup**i yako ianze kuagana na mwili
Sasa hayo huwa yanasemwa kwa watu wa karibu na familia ya wahusika, hivyo kuzuia hilo dawa ni kuondoa mazoeano kati ya familia yako na watu wengi isipokuwa ndugu zako tu
 
Mkuu, wanawake wa siku hizi ni rahisi sana kukukana pindi anapokutana na mwanaume asiyemjua.
Hakuna cha wanawake wa siku hizi wala siku zile, ukiona mwanamke anakusaliti ujue anakudharau, akikuheshimu hawezi kufanya hayo, na kama hakueshimu ni bora ujenge mazingira ya yeye kukuogopa tu kunatosha.
 
Mkuu, ujumbe wako mzuri ila unauma na mbaya zaidi ukute unampenda bado huyo mke. Tehe tehee... Naogopa kupenda kupindukia maana wanawake hawatabiriki.
 
Mkuu, ujumbe wako mzuri ila unauma na mbaya zaidi ukute unampenda bado huyo mke. Tehe tehee... Naogopa kupenda kupindukia maana wanawake hawatabiriki.
Tatizo sio wanawake tu bali wanaume pia nao wako hivyo.
 
Haijalishi mtu anakujua au hakujui. Mtu akiwa sio mwamini either ata NYOSOA au ata NYOSOLEWA. Live your life usiogope mwenzio ata nyosolewa au la
 
Back
Top Bottom