Asilimia kubwa ya watoto kuanzia miaka 10+ wameharibika kimaadili

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
700
Gwala kwa wana Jeifu,

Niende kwenye mada, kwa siku za hivi karibuni nimeshuhudia vituko na vibweka vya watoto wa miaka 10 na kuendelea kwa jinsia zote mbili (kike na kiume). Watoto hawa wana tabia za ajabu na wanayoyaongea na kuyafanya mengi yamewapita umri kabisa.

Shida imeanzia wapi? Ili ndiyo swali la muhimu kujiuliza, jambo la kujua ni kwamba wazazi au walezi wakishindwa kumlea mtoto wao utamlea mtaa, na si kama zamani kwamba mtaani atakutana na watu wataomfunza adabu (hata kwa fimbo) hata huko mitaani na kwenyewe hali ni mbaya. Kwasasa si jambo la kushangaa kukuta mwanaume mwenye miaka 50+ akitembea na binti wa miaka 15.

Tatizo la tabia hizi lina mizizi mikubwa tena mipana kama ile ya mandrake, wazazi nao wamevurugwa kwahiyo wanaacha watoto waige kila kitu na kuangalia kila kitu katika mitandao na Television bila kufanya censorship ya aina yoyote ile.

Scenario: Kuna mtoto wa jirani yangu anayesoma darasa la Tano kwa mwaka huu, huyu mtoto alimfuata mzazi wake hima hima akimtaka aende shuleni " Mwalimu wa darasa anataka aongee na wewe" ili ndiyo jibu alilolitoa alipoulizwa na mzazi wake kuhusu kuitwa shuleni. Baada ya kufika shuleni mwalimu wa darasa amemtaarifu mzazi kwamba bintiye (mtoto wake) anaandika barua za kimapenzi na kuwapa wavulana (she is not even 12) baba aling'aka na kuahidi kulishughulikia hilo jambo. Shuleni wametoa adhabu imeshindikana dogo habadiriki kwa chochote.

Mwezi wa tano mwaka huu dogo alipatwa na kesi ya kuwafunulia wanafunzi wenzie wa kiume sketi na kuwataka watazame uke wake. The case was resolved na mzazi alijua dogo ataacha but still mambo ni yale yale. Shida si kwamba mwenye hiyo issue ya uhuni au uvunjaji wa sheria na ukahaba kidari ni mmoja kakikundi ka wasichana kanaendelea kuongezeka kwenye huo uozo.


NB: Malezi ni ya mzazi, huku duniani kuna kifo, mimba, UKIMWI, kansa ya kizazi na magonjwa yote yatokanayo na ngozo zembe
 
Gwala kwa wana Jeifu,

Niende kwenye mada, kwa siku za hivi karibuni nimeshuhudia vituko na vibweka vya watoto wa miaka 10 na kuendelea kwa
Huwezi kuwalaumu watoto lawama ziende kwa wazazi na jamii kwa ujumla.
 
Bongo fleva ina mchango mkubwa sana hapa hasa hasa wale vijana wa wasafi yaani ukipigwa wimbo wao kama upo na watoto au watu wazima unaowaheshimu inabidi tu ubadilishe chanel
Hii bongo fleva ina shida kubwa, ila sijajua ni kwamba wanalelewa (waimbaji) au Mamlaka husika zimekosa meno yaku-deal na hawa waimbaji
 
Bongo fleva ina mchango mkubwa sana hapa hasa hasa wale vijana wa wasafi yaani ukipigwa wimbo wao kama upo na watoto au watu wazima unaowaheshimu inabidi tu ubadilishe chanel
Hii bongo fleva ina shida kubwa, ila sijajua ni kwamba wanalelewa (waimbaji) au Mamlaka husika zimekosa meno yaku-deal na hawa waimbaji
Kila mtoto anataka awe mkata mauno
Sahvi watoto hawafikiri kuja kuwa walimu,madokta,mafundi,manesi nk
Ukipata wasaa wa kuwahoji watoto 10
Katika hao 10 ,wanane wanataka wawe wakata mauno
Nchi hii mpaka 2030 2035 huko itakuwa kama kongo ,watajaaa wakata mauno tupu ----- type

Ova
 
Tatizo ni kwamba watu wengi siku hizi tume~underrate sana suala zima la maadili.

Ikumbukwe mtoto ummleavyo ndivyo akuavyo.

So core ya mabadiliko haya ya kitabia naweza kusema ni sisi wenyewe
 
Back
Top Bottom