Asilimia 95 machinga Ilala wapata vitambulisho

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
machinga.jpg

machinga.jpg

MWENYEKITI wa machinga Kariakoo Steven Lusinde, amesema asilimia 95 ya machinga katika Wilaya ya Ilala, wameshapewa vitambulisho vilivyozindulia na Rais John Magufuli kwa ajili ya watu wa kada hiyo.

Alisema awamu ya kwanza vitamvulisho vilivyotolewa vilikuwa 5,000 na awamu ya pili 27,000 ambapo jumla ya vitambulusho 32,000 vilitolewa kwa Wilaya ya Ilala huku bado kukiwa na uhitaji wa vitambulisho vingine.

“Vitambulisho vimeisha, wamachinga waliopata ni asilimia 95 tu, tumeshatoa taarifa ili tutengenezewe vingine, vitakapofika zoezi litaendelea, nawashauri wamachinga wafate maelekezo ya mheshimiwa Rais ili kuchangia maendeleo ya nchi,”alisema Lusinde.
 
Back
Top Bottom