Asilimia 50 ya wanaomaliza STD VII hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asilimia 50 ya wanaomaliza STD VII hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 22, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hayo ni matokeo ya ripoti moja iliyotolewa jana.. HABARI NDIYO HIYO!

  CHANZO: Habari Leo

  UTAFITI wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwezo, umebaini kuwa kati ya wanafunzi 10 wanaomaliza darasa la saba, wanafunzi watatu hawawezi kufanya hesabu za darasa la pili.

  Katika matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa Dar es Salaam jana, taasisi hiyo pia ilibaini kuwa, nusu ya wanafunzi wanaomaliza elimu hiyo ya msingi sawa na asilimia 49.1, hawawezi kusoma hadithi kwa Kiingereza.


  Mkurugenzi wa Uwezo, Grace Soko, alisema jana kwamba utafiti huo ulifanywa kwa wahitimu wa shule za msingi 42,033 waliokuwepo majumbani ambao walifanya majaribio ya darasa la pili katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hesabu.


  Mbali na Kiingereza, somo ambalo utafiti huo umebaini kuwa ni gumu kuliko masomo mengine, pia ilibainika kuwa mhitimu mmoja wa elimu ya msingi kati ya wahitimu watano, hawawezi kusoma hata Kiswahili cha darasa la pili.


  Katika somo la hesabu, Soko alisema, "ingawa stadi za kuzidisha zipo kwenye mtaala wa darasa la pili, hakuna mwanafunzi hata mmoja wa darasa la pili aliyeweza kuzidisha bila shida, huku asilimia 31 ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi wakishindwa kufanya hesabu hizo.


  Alisema jambo hilo linadhihirisha kuwa mhitimu mmoja kati ya wahitimu 10 wanaomaliza elimu ya msingi bila kuwa na stadi ya hisabati hawataweza kufanya masomo ya sayansi na biashara akiwa katika elimu ya sekondari.


  Hata hivyo, Mkurugenzi wa Twaweza, Rakesh Rajani ambaye alikaribishwa wakati wa kutangaza matokeo ya utafiti huo, aliipongeza serikali kwa kuinua kiwango cha elimu kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi.


  "Inasikitisha kuona watoto wanahitimu darasa la saba bila kujua kusoma Kiingereza hata kile alichotakiwa kusoma mtoto wa darasa la pili, watashindwa kumudu masomo ya sekondari ambayo yanafundishwa kwa lugha hiyo," alisema.


  Kutokana na matokeo hayo, taasisi hiyo ya Uwezo imebuni mkakati wa miaka minne wa kuendeleza stadi za kusoma na ujuzi wa hesabu kwa watoto wa umri wa miaka mitano hadi 16 katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  mfanikio makubwa haya ya kikwete..........
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I think this is not newz, nimesikia kadhia kama hizi mara nyingi sana watu wanamaliza Std 7 lakini hajui kusoma kuandika wala kuhesabu. Sasa linganisheni habari na uzi huu..utabaini nchi inahujumiwa na watu wa ndani na nje, wakishirikiana kutunyongea baharini.
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  who cares?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu I have a friend alikuwa ni headmaster wa shule ya kata, anasema kuna wanafunzi wanachaguliwa kuingia sekondari hawajui kusoma wala kuandika katika shule hizo. Just pathetic!
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  kuna hii kitu ilianzishwa ya special schools,ambapo walikuwa wanachaguliwa wanafunzi wenye highest marks.mkifika form I baada ya miezi mitatu kunakuwa na mtihani wa mchujo.

  Kama nakumbuka vizuri mtihani ulikuwa ni wa hesabu tu,tena format ya darasa la saba, ilikuwa shock kwamba kuna waliopata 0%. Na hii innovation ilikuja baada ya baadhi ya wanafunzi kuulizwa 'what is ur name' na kubaki wakishangaa tu.

  Wengine miandiko ilikuwa ni ya std 1!Ili ku-maintain hadhi ya u-special school, wale waliopata below 50% walihamishiwa shule zingine za sekondari. Hili tatizo lipo siku nyingi tu, kwa hiyo tunapojivunia takwimu zetu bila kuangalia kama zinatupeleka popote inabidi kuwa makini:

  Tunaposema idadi ya wanafunzi wanaoanza shule za msingi imeongeze,je ya wahitimu wa shule za msingi nayo imeongezeka kwa kiasi gani? Na je wangapi kati ya hao wanapata utaalamu (diplomas and degrees)? Kama kawaida yetu,lakini haitoshi tu kuandiskisha watoto ili wakakulie huko shuleni bila kufaidi chochote.

  Angalizo: kuna baadhi ya waalimu huko vijijini wanapewa fedha na wazazi kwa ajili ya kuwafanyia mtihani wanafunzi.
   
 7. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Niliiona hiyo taarifa jana kwenye tv.......... ilinisikitisha sana. Halafu mtu anasimama na guts zake za kifisadi ati "nimetekeleza ahadi zangu zote nilizozisema na sina cha kujuta wala mtu hawezi kunihoji kwa hilo" ..........inatia kichefuchefu kwa kweli.
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Pinda amekwisha pokea tuzo kwa hilo!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Aisee....
   
 10. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napunguza kushangaaa, nasubiri Octoba 31
   
 11. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wakati Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo Pinda, jana tarehe 19 Septemba 2010 alipokea Tuzo kutoka Umoja wa Mataifa kwa mafanikio Tanzania iliyopata katika uandikishaji wa watoto wengi zaidi kujiunga na Darasa la Kwanza hapa nchini. Inakadiriwa kuwa zaidi ya 95% ya watoto wote wanaotakiwa kwenda shuleni waliandikishwa kujiunga na Darsala Kwanza hapa nchini

  Tarehe 20 Septemba 2010, Taasisi inayohusika na masuala ya Kielimu hapa nchini iitwayo TENMET, katika mkutano wa ELIMU KWA WOTE imetangaza matokeo ya utafiti wa sekta ya Elimu ya Msingi. Utafiti huo unaonyesha kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa nchini ni ya kiwango cha chini sana, ambapo zaidi ya 50% ya watoto wanaomaliza Elimu ya Msingi (Darasa la Saba) hawawezi Kusoma na Kuandika Kiswahili, Kiingereza na Hisabati.

  Utafuiti huo umeendelea kubainisha kuwa idadi hiyo ya watoto hawawezi kushinda mitihani ya masomo hayo ya Darasa la Pili.

  Hali hii inaripotowa wakati ambapo Tanzania ipo katika kipindi cha Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, na tayari vyama viwili vya CHADEMA na CUF vimeahidi kuboresha sekta ya Elimu kwa kutoa Elimu ya Bure kwa watoto wote kutokea Darasa la Kwanza hadi Kidato cha Sita; na Chuo Kikuu.

  Na wasemaji mbali mbali wa chama tawala CCM wameipinga ahadi hiyo, na kudai kuwa suala hilo haliwezekani kutokana na hali ya kiuchumi ya Tanzania.

  Vyama vinavyoahidi kutoa Elimu bure vinadai kuwa Serikali iliyoko madarakani inawekeza kidogo sana katika sekta ya Elimu hivyo kushindwa kuwapatia waalimu mazingira na mahitaji muhimu ya kufundishia kama vile nyumba za waalimu, vutabu vya kiada, vifaa vya kufundishia n.k; na kuwapatia wanafunzi mazingira huduma muhimu za kuwawezesha kusoma na kupata elimu inavyotakiwa kama vile vyumba bora vya madarasa, madawati, vitabu, waalimu wa kutosha n.k.

  Sababu mbali mbali zintajwa kuifanya Serikali iliyoko madarakani kushindwa kuwekeza ipasavyo katika sekta ya Elimu ikiwemo kuwa na matumizi makubwa sana yasiyokuwa na tija kwa wananchi walio wengi, kutoa misamaha mingi na mikubwa ya kodi kwa wawekezaji hususan kwa sekta ya madini. Inadaiwa kuwa mfano hai ni Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inazoonyesha kuwa Serikali iliyoko madarakani kila mwaka inatoa misamaha ya kodi inayofikia Shilingi Bilioni 700, hali ambayo huchangia kwa kiwango kikubwa kushusha mapato ya Serikali na hivyo kushindwa kuwapatia wananchi huduma za kijamii ikiwemo Elimu.

  Vile vile vyama vinavyoahidi kutoa Elimu bure vinadai kuwa Serikali iliyoko madarakani imeweka kiwango kidogo cha mrahaba kwa wawekezaji wa sekta ya madini cha 3% tu, wakati ambapo nchi ya Afrika ya Kusini inakusanya mrahaba wa 12% kutoka kwa wawekezaji hawa hawa na kwa madini ya aina hiyo hiyo. Na nchi ya Botswana badala ya kuchukua viwango vidogo vya mrahaba, inaingia ubia na wawekezaji wa sekta ya madini na hivyo kupata mapato makubwa sana.
   
 12. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Labda wangetusaidia kutueleza waliofanya utafiti walitumia population za shule za aina gani? hii ingeleta maana zaidi, ni kweli 50% hawajui kusoma lakini kwa picha kubwa zaidi tunahitaji kujua wanatoka kwenye shule za Accademia au kazana twende?

  Wakitoa population waliyotumia kufanya utafiti inawezekana wametumia kazana twende peke yake hii itakuwa na maana nyingine kubwa ambayo watu wanaiopigia kelele ambayo ni tatizo la ujenzi wa matabaka kwenye elimu kwa kutengeneza watawala na watwana wa baadae

  Hawa wanaosoma kwenye kazana twende watakuwa wavuta bangi, wezi na majambazi. Baadae tutawalaumu na kuwachoma moto au kuwapeleka mahakamani ili wahukumiwe na hakimu aliyesoma academia.

  Government need to think twice kwenye mfumo wa elimu tunaoenda nao kwa sasa
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mie ninafahamu kwa miaka mingi watoto wa jirani zangu tena hapa mjini ambao wamemaliza darasa la saba na hawajui kusoma wala kuandika.
  Hili si jambo jipya na nashangaa hizo tafiti wanapotezaje muda wao kutumia na pesa nyingi kwa kitu kilicho wazi kiasi hiki.
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mzee M- Una uhakika kweli na hii habari yako :confused2:
  Maana Juzi tu Tanzania Imechukua Tuzo ya MDGs:becky:
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hali inatisha na kwa raia wa aina hiyo tusitegemee miujiza.............maendeleo tanzania yana parefu
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Proffessor mmoja alisema alikuwa kira mara akisema kuwa illiterace rate imeongezeka nilikuwa sielewi, kwani ni yeye alisema enrollment imeongezeka, nashangaa tuisheni zimezidi kuanzia nursery, na mtoto siku hizi hawi enrolled primary mpaka awe amekwenda nursery, meaning awe anajua kusoma na kuandika, sa sielewi kweli sielewi.
   
 18. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mtoa hoja kapotosha kwa makusudi. Ripoti inasema 49.1 ni wasio jua kusoma kingereza, lakini "mhandisi" wetu anataka tuamini hawajui kusoma kabisa!

  Kazi kweli kweli!
   
 19. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  wewe madrassa kuja hapa nikunong'oneze, kuna tofauti gani kati ya kusoma kingereza na kusoma kwa kawaida ... au ulitaka waseme kusoma kiarabu?
   
 20. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wednesday, 22 September 2010
  Na Edmund Mihale


  SIKU moja baada ya Tanzania kupewa tuzo ya kimataifa kwa kutekeleza vizuri malengo ya elimu pamoja na mafanikio hayo utafiti uliofanywa na Taasisi ya Uwezo Tanzania umeibaini nusu ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika katika masomo ya Kingereza, Kiswahili na ujuzi wa Hesabu.

  Hatua hiyo imeelezwa na utafiti huo kuwa inakwamisha safari ya kufikia 'Elimu kwa Wote' na moja ya malengo ya millenia.

  Tuzo hiyo ilipokewa rasmi juzi na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kwenye sherehe ya Tuzo ya Utekelezaji wa Malengo ya Milenia 2010, mjini New York, Marekani.

  Taasisi hiyo yenye mtandao katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania ilifanya utafiti huo katika vijiji 1,140 vya Tanzania vilivyo katika wilaya 38 kati ya 133 kwa kuwahoji wanafunzi 42,033 walio katika kaya 22,800 Mei mwaka huu.

  Akizungumuza katika uzinduzi wa utafiti huo Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt. Grace Soko, alisema utafiti huo ulijikita katika matokeo sita muhimu katika masomo matatu ya Kiingereza, Kiswahili na Hesabu.

  Alisema kuwa pamoja na Kiswahili kuzungumzwa kwa upana zaidi nchini, watoto pungufu ya watatu kati ya kumi wa darasa la tatu hawawezi kusoma hadithi ya Kiswahili baada ya kumaliza darasa la saba na mmoja kati ya watano hawawezi kusoma masomo ya darasa la pili.

  "Asilimia 42 ya watoto wa miaka 5 hadi 16 wanaweza kusoma Kiswahili lakini asilimia 1 ya watoto wenye miaka mitano, asilimia 51 ya watoto wenye umri wa miaka 11 na asilimia 75 ya watoto wenye umri wa miaka 16 hawajui kusoma kabisa," alisema Dkt.
  Soko. Alisema nusu ya wanafunzi wanamaliza darasa la saba hawezi kusoma Kiingereza.

  "Kiingereza ni somo gumu kwa wanafunzi kwa kuwa mtoto mmoja kati ya 10 wa darasa la tatu anaweza kusoma hadithi ya Kiingereza baada ya kumaliza elimu ya msingi, na nusu hawawezi kusoma kwa kiwango cha darasa la pili alisema Dkt. Soko. Alisema katika utafiti huo wamebaini kuwa ingawa stadi za kuzidisha ziko katika mitaala ya darasa la pili lakini hakuna wanafunzi hata mmoja wa darasa la pili aliyeweza kufanya hesabu za kuzidisha bila shida.

  Hata hivyo alisema watoto watatu kati ya 10 (31.5%) wa darasa la saba bado hawezi kufanya hisabati za kuzidisha ngazi ya darasa la pili, mtoto mmoja kati ya 10 anayemaliza shule ya msingi hana stadi za hisabati.

  Alisema watoto wa mjini hufanya kazi zaidi kuliko wa kijijini ambapo wale wa mjini hupata asilimia kati ya saba hadi 10 zaidi kuliko wa vijijini katika masomo yote.

  Alisema asilimia 33 ya watoto wenye umri wa miaka 11 wanaoishi mjini wana uwezo wa kusoma Kiingereza kuliko wale vijijini.

  Dkt. Soko alisema utafiti huo pia umebaini kuwa wasichana hufanya vizuri katika masomo yao kuliko wavulana ambapo wasichana walipata alama nzuri katika masomo waliyopimwa ingawa ni kwa tofauti

  Alisema matokeo yanonesha kuwa katika Kiswahili wasichana walipata asilimia 43.5 na wanaume 40.7 katika somo la kiingereza walipata 18.8 wakati wavulana asilimia 18.7 na hesabu za kuzidisha walipata 30.9 na wavulana 30.6.

  Ukweli kuhusu bora elimu ya na si elimu bora
  .

  Alisema watoto wa wenye mama walisoma elimu ya sekondari wanafanya vizuri zaidi kuliko watoto wengune kuanzia darasa la kwanaza hadi la saba kutoka na kuwa elimu ya mama ni muhimu katika ngazi zote.
   
Loading...