Asilimia 13 fixed bank Vs UTT - kwa sasa wapi bora?

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,337
5,571
Wadau,

Katika kupambana na 45 Million sasa kuna benk imeniahidi kuwa nawezaweka fixed kwa 13%kwa annum. Sasa najiuliza sijui niweke huku au UTT ambapo naambiwa ni pazuri ingawa sijapata ushahidi wa njisi palikopazuri kwa hali ya sasa. Je, kwa wale mliowekeza UTT na kwa kulinganisha na hii fixed wapi unanishauri kawa mazingira ya sasa?
 
Malengo wanayo ila muda wake haujafikia.

Kuna mtu juzi tu kapata hela za mirathi milioni 30.

Ana malengo yake ila muda umembana . Hana muda kwa sasa kuyatekeleza.

Kaamua kununua viwanja 6 vya milioni 5 kila kimoja sehemu tofauti.

Siku akipata muda atauza hivyo viwanja kimoja baada ya kingine na kuanza kutekeleza malengo yake


Wenye hela hawana malenge, wenye malengo hatuna hela..

Yaaani nichukue 45M niziweke fixed??
 
Nimegundua wabongo wengi Financial Literacy ni Zero. Peleka hiyo pesa UTT weka kwenye ule mpango wa Gawio la kila mwezi. Kwa hela hiyohiyo itakupa mkopo mwingine wa fedha isiyopungua 20m sasa hizo 20m ndio zungusha mtaani, mkopo wako utalipwa na Gawio la kila mwezi la uTT!

Hii 20 ya mkopo hata kama utanuwea pombe ile 45 yako ya UTT italipa na deni likiisha unabakiwa na 45 yako. Hii ni elimu ndogo sana ya uwekezaji niliyokupa ila kama upo tayari kwa ushauri zaidi wa bure tu nicheki PM.

45m ukituliza kichwa ni pesa inayokutoa.
 
UTT Liquid fund iko poa, mwaka jana annual interest ilikuwa kama 14pc. Fixed deposit ya bank kwa 13pc hiyo ni nzuri sana kama ukiipata, vinginevyo kanunue bond za serikali, tatizo lake muda unavyokuwa mfupi, faida inazidi kushuka.
Kwa Bongo kwa sasa UTT ndio best choice hayo mabond sijui na fixed ni upuuzi tu labda kama una hela nyingi ambazo huna shida ya pesa za ziada
 
UTT Liquid fund iko poa, mwaka jana annual interest ilikuwa kama 14pc. Fixed deposit ya bank kwa 13pc hiyo ni nzuri sana kama ukiipata, vinginevyo kanunue bond za serikali, tatizo lake muda unavyokuwa mfupi, faida inazidi kushuka.
Kwa mwaka huu rate zikoje??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom