Asilimia 100 ya tabaka lililojichokeaga awamu zote, ambalo awamu ya tano linaogopwa na wenye pesa, watampa kura zote Rais John Pombe Magufuli

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
ASILIMIA 100 YA TABAKA LILILOJICHOKEAGA AWAMU ZOTE,AMBALO AWAMU YA TANO LINAOGOPWA NA WENYE PESA, WATAMPA KURA ZOTE RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.

Leo 14:45hrs 06/09/2020

Tabaka la watu wanyonge wasio na chochote cha kujisifu nacho mbele za watu ambalo awamu zote limejichokeaga tu sema safari hii katika awamu hii ya tano wenye pesa wanaosemaga unanijua mimi, wanaogopa kuwanyanyasa na hilo wanalijua,watampa kura zote Rais John Pombe Magufuli ili aweze kumalizia Miaka yake mitano ya mwisho katika Awamu yake ya pili kwa sababu ana muungano na tabaka hilo(bond),na kwa tabaka la kati lenye uwezo wa kula Milo mitatu kwa siku,Matajiri,wasomi watampa kura Rais John Magufuli kwa asilimia 90%.

-Kwanini nasema tabaka la chini litampa kura zote Rais John Pombe Magufuli.

Kwa Ujenzi wa vituo vya afya 480 katika kila Kata na Wilaya nchini kote,Mimi Mluguru wa Tawa Matombo,Morogoro Leo hii nimejengewa Zahanati,kituo cha Afya na hospitali kubwa kama ya Morogoro Mjini,nimeokoa nauli yangu toka Matombo hadi Morogoro,nimeokoa muda wangu kusafiri masaa sita licha ya barabara kuwa nzuri lakini hospitali bora ipo na sina haja tena kutembea au kusafiri kuifuata hospitali.

Kwa Ujenzi wa barabara za lami zinazounganisha miji na vijiji,Mimi Mluguru wa Matombo napita kwenye barabara nzuri ya lami toka Msalabani,Kibungo,Mkuyini,Kiloka,Ng'aro,Pangawe,Misongeni,Bigwa hadi Morogoro Mjini,naokoa muda wa kukaa masaa sita na sasa nakaa masaa mawili hadi matatu hivyo kuwahisha biashara yangu ya Mazao,machingwa,machenza,maembe,mafenesi,katika Soko kuu la Morogoro Mjini,

Ununuzi wa ndege kubwa kumi,Boeing,Airbus na Bomberdier umenifanya Mimi Mluguru wa Matombo kupanda ndege kila siku,kiuhasibu kweli sipandi ndege ila kiuchumi napanda ndege kila siku kwa maana Juice yangu ya Maembe itauzwa kwenye ndege,juice yangu ya machenza na machingwa itauzwa kwenye ndege,korosho yangu itauzwa kwenye ndege,

Kusema Air Tanzania inaleta hasara Kama asemavyo Zitto Kabwe,Tundu Lissu, Freeman Mbowe na Benard Membe ni uongo mkubwa,ukisema Air Tanzania inaleta hasara hii unazungumza kiuhasibu(Accounting) lakini kiuchumi (Economically) Air Tanzania inaleta faida kubwa kwa Tanzania,Watalii wanaletwa na ndege zetu za Air Tanzania,tumeona Tanapa wametoa gawio la bilioni 650 kwa Serikali na hizi hela zimetokana na Watalii wanaoletwa na ndege zetu,

Ndugu zangu wa Matombo, Morogoro wanapanda ndege kila siku kwa huduma za Kijamii wanazopata toka Serikalini,dawa inayopatikana kwenye hospitali imetokana na Watalii wanaoletwa na ndege zetu kulipia kodi ya shilingi bilioni kumi Serikalini kila Mwaka,Ndugu zetu wa Tawa,Kiloka na Mkuyuni Mkoani Morogoro watapata dawa,

Mishahara imepanda kwa kila Mwananchi wa Tanzania,Elimu bure kama ulikuwa unalipa shilingi 15,000 sasa hivi haulipi ada yoyote,Shule ya Msingi bure,Shule ya Sekondari bure,je Mishahara haijapanda kwa kila Mwananchi!? Na kwako wewe Mfanyakazi,pay as you earn yako Rais John Magufuli kaipunguza toka 13% hadi 9% Je mshahara bado haujapanda kwako!?

Reli ya Umeme ina faida kwa kila Mwananchi,ukisema reli ya SGR haina faida unazungumza kiuhasibu(Accounting) lakini kiuchumi(Economically) ni reli ina faida,kiuchumi ndugu za wa Ngererenge mtaniunga mkono,kwa siku Mfanyakazi analipwa shilingi elfu kumi,saa saba mchana anakwenda kula kwa Mama ntilie,Mama ntilie mchele kanunua dukani,Mwenye duka anaendelea na biashara kwa sababu ya Mama ntilie atalipa kodi kwenye kununua mchele na atalipa Mwenye fremu anapouzia na atanunya luku pia,Je Ujenzi wa reli ya Umeme hauna faida bado!?

Vitambulisho vya Wamachinga kwa shilingi 20,000 na kuuza popote nchini Tanzania bila kusumbuliwa,Nikiwa pale millennium towers naona vijana wauza matunda kwenye matenga wapo na baiskeli zao, nasubiri kuingia tra ndio nikasikiliza story mbili tatu. Mmoja anasema, "Kukaa sehemu kama hii ilikuwa ndoto, leo nauza machungwa yangu hapa hakuna hata polisi wa kunichukulia vitu vyangu, zamani ilikuwa karandinga linapita na kusomba kila kitu, mtaji wote wanauchukua"

Zitto Kabwe,Tundu Lissu,Benard Membe hawakubaliani na kufanya biashara popote, yaani kwao inaweza kuwa kero kubwa sana lakini kwa Rais John Pombe Magufuli na tabaka la chini ni bonge moja la mtaji na faida kwa kila Mwananchi,John Pombe Magufuli has five years more,thus Wamachinga also have five years more,Ambavyo Rais John Magufuli anayo Miaka mitano mingine vivyo hivyo Wamachinga wanayo Miaka mingine mitano ya kufanikiwa kibiashara,kiuchumi kitambulisho cha 20,000 ukigawanya kwa siku 365 unapata senti 54,kwa hiyo Machinga analipa senti 54 kila siku,lakini kwa Serikali ikiwa na Machinga 1,000,000 ukizidisha 54 unapata Milioni 54,Hii ni win win situation,Machinga anapata unafuu na Serikali inapata faida,

Bwawa la Umeme la Julius Nyerere katika mto Rufiji lina faida kubwa ambayo itakuja moja kwa moja kwa tabaka la chini,Bwawa la Umeme analojenga Rais John Magufuli likiisha litashusha bei ya Umeme,kama unatumia luku ya 30,000 kwa mwezi sasa utatumia luku ya shilingi 15,000 tu,hii ni faida kwa kila Mwananchi,na pia faida kwa Serikali kuondokana na kukipa mabilioni ya pesa kila mwezi kwa Umeme wa kukodi ambao umetuletea kashfa nyingi za Ufisadi kama Richmond na Escrow ambazo zilisababisha nchi ikaingia kwenye Umeme wa mgao na Taifa kuingia gizani,Je bei ya Umeme ikishuka bado Bwawa la Umeme analojenga Rais John Pombe Magufuli halitakuwa na maana!?

Nimalizie kwa Wagombea wa upinzani waliokuwa wakiikejeli serikali ya Kikwete kwa kutokuwa na shirika la ndege la taifa leo watu wamegeuka!!.Niwaambie miradi mikubwa unaweza kuahirisha kuifanya leo lakini sio milele yote. Ipo siku utakuja kuiona umuhimu wake,huwezi kukwepa umeme wa uhakika,huwezi kuikwepa treni ya kisasa,wapinzani wanalalamikia hata mema yanayotendwa na Rais John Pombe Magufuli,hakuna namna ya uwepo wa serikali yenye kuweza kumfurahisha kila mtu kila wakati hasa wale vigeugeu leo wanasema Taifa halina ndege kesho ukinunua wanasema bora ungechimba choo shuleni,hivi tukae kila siku kuchimba vyoo tu!?

Ndege zinanunuliwa Madawa yapo mahospitalini na nchi inakwenda vyema kabisa,hakuna anayeishiwa hoja bali dira ya Maendeleo inafuatwa, Kazi inaendelea,Kikwete alikopa sana na pakawa na deni kubwa la ndani na wasio na shukrani wala heshima kina John Mnyika wakamuita dhaifu,Raia hawezi wala hapaswi kumridhisha kila mtu yeye anabaki kutimiza yote anayoagizwa na ilani kuyatimiza,Uwezo wa kukopa na kurejesha ni masuala ya muda tu,Nchi inafunguka kwa ujumla wake na kadri miundo mbinu inavyosambaa ndivyo fursa
zinavyofunguka,madiwani wanaoombewa kura kazi yao,ni kuwa karibu na kero za wananchi,Sekta nyingine zinaendelea kama kawaida lakini ujenzi ni muhimu sana kwani unazo fursa nyingi siku zijazo.

Chadema si wanasemaga majukwaani wakati wanaomba kura kwamba watajenga mabarabara. wataleta Umeme,wataboresha huduma za Afya na nk,Wakishapewa kura wakapita wanaanza kusema Chadema haikusanyi kodi sasa kama ulijua hukusanyi kodi kwa nini uliwaongopea wananchi,hapa wananchi wanapaswa kuwapima hawa wahuni wanaotafuta madaraka kwa kuwa hadaa wananchi,Naipongeza sana Serikali yangu ya chama cha mapinduzi kwa kuwa wahungwana wa kupeleka Maendeleo hata kwa wale wananchi hambao hawakuichagua.

Nimalizie kwa kusema silimia angalau 90 ya wanaohudhuria kampeni za Rais John Pombe Magufuli ni wapiga kura wakati wanaohudhuria kampeni za Lissu ni wahini angalau asilimia 10 wanaweza kuwa wapiga kura,katika Mazingira haya you need to be Comical Ally of this era kusimama na kusema Tundu lissu au Benard Membe atapata angalau hata 10% ya kura zote,Nitabiri Ushindi wa asilimia tisini 90% kwa Rais John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Una degree ya biashara ya kimataifa lakini hata genge la mboga mboga huna
 
Wenzako wakitaja viwango vyao vya elimu huwa wanaweka ma chuo alichosoma

Mfano MSc finance Hull University

Sasa wewe inaelekea elimu yako ni ya hapa na pale yaani ya kuunga unga kama mwenyekiti wako
 
Unaona sifa kusema kuwa kuna tabaka lilojichokeaga?

Nani kasababisha uchovu huo?
 
Back
Top Bottom